Swali
Je! Biblia inasema nini juu ya jukumu la kasisi mwandamizi?
Jibu
Kuhusu jukumu la mchungaji, Biblia inasema mengi. Maneno ya msingi ambayo yanaelezea jukumu la mchungaji ni "mzee," "askofu," na "mwalimu" (1 Timotheo 3: 1-13). "Mzee," au episkopos (ambalo tunapata neno letu maaskofu) linalorejelea usimamizi wa waumini, na inajumuisha kufundisha, kuhubiri, kutunza, na kutumia mamlaka pale inapohitajika. Mzee pia hutumika kanisani kama kiongozi na mwalimu. Katika Tito 1: 5-9, Paulo anamhimiza Tito "kuwateua wazee wa kanisa katika kila mji." Watafundisha na kuongoza makanisa katika ukuaji wao wa kiroho. Pia, katika 1 Petro 5: 1-4, Petro anawahutubia "wazee wenzake" na kuwaambia "mlichunge lile kundi la Mungu mlilokabidhiwa; mlitunze si kwa kulazimika, bali kwa hiari kama atakavyo Mungu. Fanyeni kazi hiyo si kwa tamaa ya fedha, bali kwa moyo wenu wote" (1 Petro 5: 2).
Kwa hivyo kuhusu jukumu la mchungaji mwandamizi Biblia haisungumzii cheo hicho haswa. Limekuwepo pindi kanisa linapokua na kuhitaji wafanyikazi wa ziada. Cheo cha mchungaji mwandamizi linarejelea mtu anayeongoza kanisa, kwa jumla anatoa mahubiri na mafundisho mengi kutoka kwenye mimbari katika ibada na kufanya kazi ya kusimamia kanisa. Baadhi ya makanisa mengine makubwa yanaweza hata kuwa na mchungaji mtendaji anayesimamia shughuli za kila siku za kanisa, huku mchungaji mwandamizi wakati huo atakuwa na jukumu la kufanya kazi na bodi ya kanisa, pamoja na huduma za kuhubiri, kufundisha, na ushauri ambazo huandamana na jukumu la mchungaji.
Kila kanisa, liwe kubwa au dogo, linahitaji mchungaji ambaye atalichunga, kuliongoza, kulilisha, na kuelekeza watu kwa ukuaji wa kiroho na kumtumikia Bwana Yesu. Katika makanisa makubwa, mchungaji mwandamizi mara nyingi huchunga kikosi cha wachungaji pamoja na kuchunga kanisa. Kama matokeo, mchungaji mwandamizi anapaswa kushikiliwa kwa kiwango cha juu zaidi kulingana na 1 Timotheo 3: 1-13 na Tito 1: 6-9 kuliko majukumu mengine ya kichungaji.
English
Je! Biblia inasema nini juu ya jukumu la kasisi mwandamizi?