settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kuwa katika Kristo?

Jibu


Wagalatia 3: 26-28 inatupa ufahamu juu ya maneno "katika Kristo" na maana yake. "Katika Yesu Kristo ninyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu kwa njia ya imani, kwa maana ninyi nyote mliobatizwa kwa Kristo mmevaa Kristo. Hakuna Myahudi wala watu wa Mataifa, wala mtumwa wala huru, wala

hakuna mwanamme na mwanamke, kwa maana nyinyi wote ni kitu kimoja katika Kristo Yesu. " Paulo anazungumza na Wakristo huko Galatia, akiwakumbusha utambulisho wao mpya tangu waliweka imani yao kwa Yesu Kristo. Ili "kubatizwa ndani ya Kristo" inamaanisha kwamba walijitambulisha pamoja na Kristo, wakiacha maisha yao ya zamani ya dhambi na kukubali kikamilifu maisha mapya ndani ya Kristo (Marko 8:34; Luka 9:23). Tunapopata kukaribia kwake Roho Mtakatifu, Yeye"hubatiza" ndani ya familia ya Mungu. Wakorintho wa Kwanza 12:13 inasema, "Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja."

Mahali kadhaa katika Maandiko yanaelezea mwamini "kuwa ndani ya Kristo" (1 Petro 5:14; Wafilipi 1: 1; Waroma 8: 1). Wakolosai 3: 3 inasema, "Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu." Mungu ni haki kamili. Hatuwezi kucgukulia dhambi kwa urahisi au kuruhusu dhambi zetu; hio haitakuwa sawa. Dhambi ilitakiwa kugharamiwa. Hasira zote Mungu anazokua nazo juu ya uovu zilimwagika juu ya Mwanawe. Wakati Yesu alichukua nafasi yetu msalabani, alipata adhabu ya dhambi yetu. Maneno yake ya mwisho kabla ya kufa, "Imekamilishwa" (Yohana 19:30). Nini kilichokamilika? Si tu maisha yake duniani. Kama alipothibitisha siku tatu baadaye, hiyo haikuwa imekamilika (Mathayo 28: 7, Marko 16: 6; 1 Wakorintho 15: 6). Alichomaliza msalabani ilikuwa mpango wa Mungu wa kuukomboa ulimwengu Wake ulioanguka. Wakati Yesu akasema, "Imekamilishwa," Alikuwa akisema kuwa Alifanikiwa kulipa kikamilifu kwa kila tendo la uasi, wa zamani, wa sasa, na wa baadaye.

Kuwa "katika Kristo" inamaanisha tumekubali dhabihu yake kama malipo ya dhambi zetu wenyewe.Rekodi za makossa yetu zina mawazo yenye dhambi, tabia au matendo tuliyofanya. Hakuna kiasi cha kujitakasa kunaweza kutufanya tuwe safi ya kutosha msamaha na uhusiano na Mungu mtakatifu (Warumi 3: 10-12). Biblia inasema kwamba katika hali yetu ya asili ya dhambi sisi ni maadui wa Mungu (Warumi 5:10). Tunapokubali dhabihu yake kwa niaba yetu, Yeye hubadilisha rekodi zetu zetu za dhambi. Yeye hubadilisha orodha yetu ya dhambi kwa ajili ya akaunti Yake kamili ambayo inampendeza Mungu kabisa (2 Wakorintho 5:21). Mageuzi haya ya Kimungu hufanyika chini ya msalaba: tabia yetu ya zamani ya dhambi kwa ajili ya asili yake kamilifu (2 Wakorintho 5:17).

Kuenda mbele ya Mungu Mtakatifu, lazima tufiche katika haki ya Kristo. Kuwa "ndani ya Kristo" inamaanisha kwamba Mungu haoni tena udhaifu wetu; Anaona haki ya Mwanawe mwenyewe (Waefeso 2:13; Waebrania 8:12). Ni "katika Kristo" ambapo deni la dhambi ilifutwa, uhusiano wetu na Mungu hurejeshwa, na uzima wetu wa kudumu ulitekelezwa (Yohana 3: 16-18, 20:31).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kuwa katika Kristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries