Swali
Je, ni matukio gani makuu katika maisha ya Yesu Kristo (sehemu ya 1)?
Jibu
Yafuatazo ni matukio muhimu katika maisha ya Kristo na vitabu vya Biblia ambapo kila tukio limeelezewa (Sehemu ya 1):
Kuzaliwa: (Mathayo 1-2; Luka 2) — Katika vifungu hivi kuna mambo yote ya hadithi inayojulikana ya Krismasi, mwanzo wa maisha ya kidunia ya Kristo. Maria na Yusufu hawakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni, mtoto aliyelazwa katika hori, wachungaji na mifugo wao, malaika wengi wakishangilia. Tunaona pia mamajusi kutoka Mashariki ambao walifuata nyota kuelekea Bethlehemu huku wakibeba zawadi kwa ajili ya mtoto Kristo. Tunaona pia Yusufu, Maria, na Yesu wakimbia Misri na baadaye kurudi Nazareti. Vifungu hivi pia hujumuisha Yesu akiwasilishwa kwa hekalu akiwa na umri wa siku nane na, akiwa na umri wa miaka kumi na miwili. Pia vinaonyesha Yesu akisalia katika hekalu akizungumza na walimu huko. Hadithi ya kuzaliwa kwa Mwokozi miaka elfu mbili zilizopita ni ya kushangaza, imejawa na maelezo mazuri na yenye maana yaliyothaminiwa na wale walioshudia na waamini baada ya maelfu ya miaka. Lakini hadithi ya Mungu kuja duniani kama mwanadamu ilianza maelfu ya miaka hapo awali pamoja na unabii wa kuja kwa Masihi. Mungu alizungumza juu ya Mwokozi katika Mwanzo 3:15. Karne kadhaa baadaye, Isaya alitabiri juu ya bikira ambaye angeweza kuchukua mimba na kumzaa mwana na kumwita jina lake lmanueli, maana yake ni "Mungu pamoja nasi" (Isaya 7:14).Matukio ya kwanza muhimu katika maisha ya Kristo yalianza kwa unyenyekevu katika hori, wakati Mungu alikuja kuwa na sisi, alizaliwa kuwaweka watu wake huru na kutuokoa kutoka kwa dhambi zetu.
Ubatizo: (Mathayo 3: 13-17; Marko 1: 9-11; Luka 3: 21-23) — Ubatizo wa Yesu na Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani ni tendo la kwanza la huduma yake ya umma. Ubazizi wa Yohana ulikuwa ubatizo wa toba, na ingawa Yesu hakuhitaji ubatizo kama huo, alikubali ili atambulike na wenye dhambi. Kwa kweli, wakati Yohana aliposita kubaziza Yesu, alisema kwamba alikuwa yeye, Yohana, ambaye angepaswa kubatizwa na Yesu, lakini Yesu alisisitiza. Yesu alisema, "Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote." Basi Yohana alifanya kama alivyoomba (Mathayo 3: 13-15). Katika ubatizo wake, Yesu alijitambulisha na wenye dhambi ambao dhambi zao angezichukua msalabani ambako angebadilisha haki yake kwa dhambi zao (2 Wakorintho 5:21). Ubatizo wa Kristo ulionyesha kifo na ufufuo wake, kuonyesha umuhimu wa ubatizo kwa Kikristo, na kumtambua kwa uwazi Kristo na wale ambao angekufa kwa ajili yao. Zaidi ya hayo, utambulisho wake kama Masihi aliyekuwa akisubiriwa kwa muda mrefu ulithibitishwa na Mungu mwenyewe ambaye alinena kutoka mbinguni: "Huyu ni Mwanangu, ambaye ninampenda; ninayependezwa naye"(Mathayo 3:17). Hatimaye, ubatizo wa Yesu ilikuwa tukio la kuonekana kwa mara ya kwanza kwa Utatu kwa mwanadamu. Mwana alibatizwa, Baba aliongea, na Roho Mtakatifu akashuka kama hua. Amri ya Baba, utii wa Mwana, na uwezeshaji wa Roho Mtakatifu huonyesha picha nzuri ya huduma na maisha ya Kristo.
Muujiza wa kwanza: (Yohana 2: 1-11) — Ni ya kufaa kwamba injili ya Yohana ndiyo pekee inayoandika muujiza kwanza ya Yesu. Simulizi ya Yohana ya maisha ya Kristo ina mada na madhumuni ya kufunua uungu wa Kristo. Tukio hili, ambapo Yesu anageuzai maji kuwa divai, inaonyesha uwezo wake wa Kiungu juu ya mambo ya dunia, nguvu ambazo zingefunuliwa tena katika miujiza mingi ya uponyaji na udhibiti wa vipengele kama upepo na bahari. Yohana anaendelea kutuambia kwamba muujiza huu wa kwanza ulikuwa na matokeo mawili — utukufu wa Kristo uliwekwa wazi na wanafunzi walimwamini (Yohana 2:11). Asili ya Kiungu na utukufu wa Kristo ulikuwa imefichwa wakati alipoivaa asili ya kibinadamu, lakini katika matukio kama vile muujiza huu, hali yake ya kweli iliwekwa wazi kwa wote waliokuwa na macho ya kuona (Mathayo 13:16). Wanafunzi daima walimwamini Yesu, lakini miujiza iliwasaidia kuimarisha imani yao na kuwatayarisha kwa wakati mgumu uliokuwa mbele yao.
Mahubiri ya Mlimani: (Mathayo 5: 1-7: 29) — Mahubiri maarufu zaidi ilihubiriwa na Yesu kwa wanafunzi Wake hapo awali katika huduma yake ya umma. Maneno mengi maarufu ambayo tunajua leo yanatoka kwenye mahubiri haya, ikiwa ni pamoja na "Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. ," "chumvi ya dunia," "jicho kwa jicho," "maua ya shamba," " omba na utapokea, "na" mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo, "na vilevile dhana za kwenda kufanya zaidi, kugeuza shavu la pili, na mkono wa kushoto usijue ufanyalo mkono wa kuume. Pia katika mahubiri hayo kuna Sala ya Bwana. Jambo la muhimu zaidi, hata hivyo, Mahubiri ya Mlimani yalipinga Mafarisayo na dini yao ya kufanyika haki kwa kupitia matendo tu. Kwa kuelezea roho ya Sheria na sio tu barua, Yesu alitoaka shaka kuwa sheria haifai kwa ajili ya wokovu na kwamba, kwa kweli, ni vigumu kutekeleza shinikizo za Sheria. Anahitimisha mahubiri kwa wito kwa imani ya kweli kwa ajili ya wokovu na onyo kwamba njia ya wokovu huo ni nyembamba na wachache huipata. Yesu anawafananisha wale wanaosikia maneno Yake na kuyatekeleza kwa wajenzi wa hekima wanaojenga nyumba zao kwenye msingi imara; wakati dhoruba zinakuja, nyumba zao zinasimama.
English
Je, ni matukio gani makuu katika maisha ya Yesu Kristo (sehemu ya 1)?