settings icon
share icon
Swali

Je, ni matukio gani makuu katika maisha ya Yesu Kristo (sehemu ya 2)?

Jibu


Yafuatayo ni mambo ya maana kwenye uhai wa Yesu na nakala za Maandiko kwenye kila tukio limechanganuliwa: (Sehemu ya 2)

Kulishwa kwa 5,000: (Mathayo 14: 15-21; Marko 6: 34-44; Luka 9: 12-17; Yohana 6: 5-13) – Kristo alianya lishe la kutosha kushibisha takribani 5,000 na zaidi, kutoka kwa mikate midogo mitano na samaki mbili. Injili inanakiri kwamba kulikuwako halaiki 5,000 wakiume waliokuwapo, ila Mathayo anaandika kwamba kulikuwako pia wakike na wachanga pia. Halaiki inayokadiriwa ni zaidi ya 20,000. Ila Bwana wetu ni Mungu wa kutoa utajiri mwingi, na kichache ni kingi kwenye kiganja cha Mungu. Ni mengi ya kujifunza kutazama kuwa, kabla hajaongeza boflu na samaki, Kristo aliwaamuru halaiki kuketi. Hii ni taswira mwafaka ya uwezo wa Bwana kutimiza yale tusiyoweza, pamoja na kujipumzisha kwake. Watu hawakuwa na la kufanya ili kujishibisha; ila Yeye tu angetenda hayo. Walimiliki kichache ila kwa kwa kigancha cha Bwana ikageuka sherehe si tu nyingi — ilikuwa ya maana.

Kugeuzwa: (Luka 9: 26-36) – Jambo hili linatambulika kuwa "kugeuzwa," kumaanisha "kugeuka kwa maumbile," maanake Kristo aligeuzwa kwenye uwepo wa Petro, Yakobo, na Yohana na kuchukua maumbile yake ya awali. Ukuu wake ukang'aa kutoka kwa Mungu, kugeuza uso na mavazi yake kwa namna kwamba walioandika Injili walipata ugumu kuifananisha. Jinsi mtume Yohana alitumia maonyesho kadhaa kuchanganua yale aliona akiwa kizingani katika Ufunuo, ndivyo, hata, Mathayo, Marko na Luka walifaa kuhusisha taswira ikiwemo "umeme," "jua" na "mwanga" kudhihirisha alivyoonekana Kristo. Kwa kweli, ni dunia nyingine. Kuonyeshwa kwa Musa na Eliya kunongonezana na Kristo kunadhihirisha vitu viwili. Mosi, wanaume wawili wanasimamia torati na watawala, na manabii, wote waliotatabiri kurejea kwa kristo na mauti yake. Pili, ingawa waliongelea kuhusu mauti yake kule Yerusalemu (Luka 9:31) inadhihirisha kufahamu kwao kuhusu mambo hayo na mipangilio ya Bwana iliyokuwa inadhihirika kama alivyokusudia. Bwana alizungumza kutoka mbinguni na akawambia wafuasi "Msikilize!" hivyo kumaanisha kuwa Kristo, wala si Musa ama Eliya, ndiye alimiliki ukuu na uwezo wakuamuru.

Kuamshwa kwa Lazaro: (Yohana 11: 1-44) — Lazaro, nduguye Maria na Martha wa Bethania, alikuwa mwandani wa Yesu, maanake Kristo aliitwa na jamii pale Lazaro alishikwa na ugonjwa. Yesu alikawia masiku mingi kama hajaenda Bethania, akifahamu kuwa Lazaro angekuwa ameaga wakati usio mchache ili kwamba kuonyesha ukuu wa aina yake. Mungu tu ana mamlaka katika kuishi na mauti, na kwa kumwamsha Lazaro kutoka kaburini, Yesu alionyesha ukuu wake kama Mungu na ushindi wake dhidi ya mauti. Kupitia kwa tndo hili, Mwana wa Mungu angepewa utukufu kwa namna ya kutochanganyikiwa. Na kama miujiza ingine na matendo,moja ya mathumuni ikawa ni wafuasi- na sisi — "tuamini" (Yohana 20:31). Kristo aliyesema Yeye ndiye, na mojawapo ya muujiza wake unonyesha ilivyo kweli. Yesu akamnenea Martha, "Mimi ndimi huo ufufuo na uzima" (Yohana 11:25) na akamwuliza kama aliyaamini yale aliyoyasema. Huu ndio msingi wa uhai wa Kikristo. Tuna imini kuwa Kristo ni nguzo ya ufufuo, na tunamwamini Yeye kutujalia uzima wa milele kupitia kwa nguvu hiyo. Tumekufa pamoja Naye na kuufuliwa na nguvu Yake dhidi ya mauti. Ni kwa uwezo wake tu tutakombolewa.

Kuja kwake Yerusalemu: (Mathayo 21: 1-11, 14-17, Marko 11: 1-11; Luka 19: 29-44; Yohana 12: 12-19) – Kuja kwa Yesu kwa nguvu Yerusalemu juma moja kabla ya kusulubiwa ni chanzo cha kile kinachotambulika kuwa Jumapili ya mitende. Halaiki iliyomsalimia ilitandaza matawi ya mitende kwenye njia kwa sababu yake, ila walimuabudu kwa wakati mchache. Kwa siku kidogo tu, halaiki hiyo tena iliitana mauti yake, wakiinua sauti, "Msulubishe! Msulubishe! "(Luka 23: 20-21). Ila alipoingia Yerusalemu akitumia mwana-punda kuonyesha hali yake ya kujishusha na kunyenyeke-Alipata kutukuzwa na mkusanyiko na kumuitikia kuwa ndiye messaya. Watoto wachanga pia walimlaki, wakidhihirisha kuwa waliahamu wakuu wa Kiyahudi hawakutenda vile, kuwa Yesu alikuwa Masihi. Kuja kwa Kristo katika Yerusalemu kulikamilisha unabii wa Agano la Kale wa Zakaria ilivyorudiwa kwenye Yohana 12:15: "Tazama, mfalme wako anakuja, amepanda mwana punda."

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni matukio gani makuu katika maisha ya Yesu Kristo (sehemu ya 2)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries