settings icon
share icon
Swali

Tunapaswa kujifunza nini kutoka kwa maisha ya Daniel?

Jibu


Tunasoma kuhusu maisha ya Danieli katika maandiko aliyoyaandika yeye mwenyewe katika kitabu cha Danieli na pia tunasoma kumhusu katika Ezekieli 14:14, 20 na 28: 3. Kuna ukinzano wa kushangaza kati ya maisha ya Danieli na ya ule wa Yusufu mwanawe Yakobo. Wote wawili walifanikiwa wakiwa katika nchi za kigeni baada ya kutafsiri ndoto kwa wafalme wa nchi hizo, na wote wawili walipandishwa mamlaka hadi ofisi kuu kwa sababu ya uaminifu wao kwa Mungu.

Baada ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, aliifamia Yerusalemu, aliwachagua wanaume wajaziri kutoka nyumba za kifalme wa Israeli ambao walikuwa wa kupendeza na walionyesha uwezo wa kujifunza, kufundishwa tamaduni za Wababeli. Baada ya mafunzo yao ya miaka mitatu, wangewepewa nafasi ya kumhudumia mfalme (Danieli 1: 1-6). Daniel, ambaye jina lake linamaanisha "Mungu ndiye hakimu wangu," na marafikize watatu wa kutoka Yudea naye walichaguliwa na kupewa jina mapya. Danieli akawa "Belteshazzar," Huku Hananiah, Mishaeli, na Azaria wakitwa "Shadraki," "Meshaki," na "Abednego." Kuna uwezekano kuwa Wababeli waliwapa majina mapya ambayo hayakuwa na uhusiano wowote mizizi yao ya Kiebrania ili kuharakisha uzoefu wa Danieli na marafiki zake kuingiliana an tamaduni za Babeli.

Daniel na wenzake walioneka kuwa wenye hekima zaidi ya wasomi wote, na, mwisho wa mafunzo yao, waliingizwa katika huduma kwa mfalme Nebukadreza. Dalili ya kwanza ya uaminifu wa Danieli ilikua wakati yeye na marafikize watatu walikataa chakula kitamu na divai kutoka mezani ya mfalme, kwa sababu waliona kuwa ni kujitia doa, na wakawa kula mboga. Afya yao ilipoboreka, waliruhusiwa kuendelea kula chakula cha chaguo lao. Katika masomo yao, hawa wanaume wanne kutoka Yuda walipata ujuzi katika mambo yote ya Babeli, na Danieli akapewa uwezo na Mungu wa kuelewa ndoto na maono ya aina zote (Danieli 1:17).

Katika mwaka wa pili wa utawala wake, Nebukadreza alisumbuliwa na ndoto ambayo hangeweza kuitafsiri. Zaidi ya kuitafsiri, Nebukadreza aliwaagiza wachawi wake, wapiga ramli, wachawi, waganga wachanganusi wa anga kuielezea ndoto yake. Wanaume hawa walikuwa tayari kujaribu kuitafsiri ndoto ikiwa Nebukadreza angewaambia ndoto hiyo, lakini wakasema kuwa itakuwa vigumu sana kwa mwanadamu yeyote kufafanua ndoto yenyewe. Mfalme alitoa amri kuwa watu wote wenye hekima, ikiwa ni pamoja na Danieli na wenzake, wauawe. Hata hivyo, baada ya Danieli alimuuliza Mungu katika sala, siri ya ndoto ya mfalme ilifunuliwa kwake Danieli, naye akapelekwa kwa mfalme ili kumtafsiria. Danieli mara hiyo hiyo alilimbikizia uwezo wake wa kutafsiri ndoto kwa Mungu mmoja wa kweli (Danieli 2:28). Lengo kuu la ndoto ilikuwa kwamba siku moja kutakuwa na ufalme utakaowekwa na Mungu ambao utakaa wa milele, na kwamba ufalme wa Mungu utaharibu falme zote zilizokuwepo, za binadamu (Danieli 2: 44-45). Kwa sababu ya hekima yake, Danieli aliheshimiwa na mfalme Nebukadreza na kuwekwa katika mamlaka juu ya kusimamia watu wote wenye hekima katika Babeli. Kupitia kwa ombi la Danieli, wenzake watatu pia waliwekwa katika nafasi za mamlaka kama wasimamizi katika Babeli.

Baadaye, Mfalme Nebukadreza akawa na ndoto nyingine, nayo pia Daniel akawa na uwezo wa kuitafsiri. Mfalme alikiri kwamba Danieli alikuwa na roho ndani yake wa Mungu wake mtakatifu (Danieli 4: 9). Tafsiri ya Danieli ya ndoto ilikuwa sahihi. Baada ya kupungukiwa na akili kwa kipindi, Nebukadreza alirejeshwa afya yake, na akamsifu na kumheshimu Mungu wa Danieli kama Aliye Mkuu (Danieli 4: 34-37).

Belshaza, mwanawe Nebukadreza, akawa mfalme mpya, na wakati karamu kuu akaagiza vifuniko vya dhahabu na fedha ambavyo vilikuwa vinatumika katika hekalu takatifu kule Yerusalemu viletwe ili vitumike kwa kazi havikutengewa. Matokeo ya kuvichafua vyombo hivyo takatifu ni Belshaza kuona mkono ukiandika juu ya ukuta. Waganga wake hawakuweza kumsaidia kuyatafsiri maandiko, na kwa hiyo Danieli akaitwa ili kutafsiri maandiko (Danieli 5: 13-16). Kama tuzo kwa kutafsiri maandiko, Danieli akapandishwa cheo na Mfalme Belshaza hadi kuwa wa katika ngazi za ufalme wa Babeli (mstari wa 29). Usiku huo, jinsi vile Danieli alivyokuwa ametabiri, mfalme aliuawa katika vita, na ufalme wake ulichukuliwa na Dario Mmedi Mkuu wa Kiajemi, na Dario Mmedi alifanyika kuwa mfalme.

Chini ya kiongozi mpya, Danieli alifanikiwa katika kazi zake kama mmoja wa watawala kiwango Mfalme Dario aliwaza kumfanya awe mkuu ufalme wake wote (Danieli 6: 1-3). Hii iliwakasirisha watawala wengine sana kiwango walipanga njia ya kumwangusha Daniel. Hawakuweza kupata ubaya wowote upande wa Danieli, kwa hivyo waliangazia suala la dini ya Danieli. Wakitumia maneno ya ushawishi, na na walifanikiwa kumshawishi mfalme Dario na akatoa amri ili kuzuia sala kwa mungu yeyote isipokuwa mfalme kwa siku thelathini. Adhabu ya kutotii ilikuwa kutupwa kwenye shimo la simba. Danieli alikaidi amri, aliendelea kuomba wa Mungu wa kweli kwa uwazi. Kwa vile Danieli hakujaribu kuficha shughuli zake za mombi, alionekana akiomba hadharani na alikamatwa. Kwa majuto mengi mfalme alitoa amri Danieli atupwe ndani ya shimo la simba, lakini aliendelea kuomba na Mungu wa Danieli aliweza kumwokoa (Danieli 6:16). Siku iliyofuatia, wakati Danieli alikuwa bado hai na wa afya nzuri, alimwambia mfalme kwamba Mungu alituma malaika wake akafunga simba kinywa na hivyo hakuweza kuadhiriwa. Muujiza huu ulimfanya Mfalme Dario kutoa amri kuwa watu wote wamwabudu Mungu wa Danieli. Danieli aliendelea kuwa na ufanisi katika utawala wa Mfalme Dario.

Danieli pia anajulikana pia kwa ndoto za unabii na maono ambayo Mungu alimpa, ambayo yaliyoandikwa katika kitabu cha Danieli. Unabii wa Danieli unalenga muda mrefu wa historia za mwanadamu, kama alivyotabiri kuinuka na kuanguka kwa Ufalme wa Kigiriki na Kirumi na kuchibuka kwa mfalme mwenye nguvu ambaye "atafanya kama apendavyo; naye atajitukuza na kujiadhimisha juu ya kila mungu, naye atanena maneno ya ajabu juu ya Mungu wa miungu" (Danieli 11:36). Unabii wa Danieli wa "majuma sabini" ulizungumza kuhusu Masihi ambaye angeuawa (Danieli 9: 24-27). Tuliona unabii huu ukitimia wakati wa Yesu. Salio ya unabii-juma la sabini -utatimia wakati wa mwisho. Danieli alikuwa na maono mengine ya ufunuo pia, na kuelewa unabii wake ni muhimu kwa som la nyakati za mwisho.

Danieli alikuwa na heshim kubwa, kwa kufanya hivyo, alipokea heshima na upendo wa watawala wenye nguvu aliowahudumia. Hata hivyo, uaminifu wake na udhabiti kwa mabwana wake haukuwahi kumsababisha kuacha imani yake katika Mungu mmoja wa kweli. Badala ya hiyo kuwa kizuizi kwa mafanikio yake, kuendelea kujitolea kwake kwa Mungu kulimleta sifa ya wasioamini walio kuwa naye. Wakati wa kutoa tafsiri yake, alimpa Mungu sifa zote kwa kumuwezeza kufanya hivyo (Danieli 2:28).

Uaminifu wa Danieli kama mtu wa Mungu ulipatia neema na ulimwengu wa kidunia, bali alikataa kuikana imani yake kwa Mungu. Hata chini ya hofu ya wafalme na watawala, Danieli aliendelea kuwa imara katika kujitolea kwake kwa Mungu. Danieli pia anatufundisha kwamba, haijalishi ni nani ambaye tunakabiliana naye, hali yao ya kijamii haijalishi, tunastahili kuwa na huruma kwao. Angalia jinsi alivyokuwa na haja wakati wa alikua anatoa tafsiri kwa ndoto ya pili ya Nebukadreza (Danieli 4:19). Kama Wakristo, tumeitwa kuwaitii viongozi na mamlaka ambayo Mungu ameyaweka, kuwatendea kwa heshima na huruma; hata hivyo, jinsi tunavyoona kutokana na mfano wa Danieli, kuzingatia sheria ya Mungu lazima daima kuchukue nafasi ya kwanza mbele ya kutii wanadamu (Warumi 13: 1-7; Matendo 5:29).

Matokeo ya kujitolea kwake, Danieli alipata kibali kwa wanadamu na Mungu (Danieli 9: 20-23). Kumbuka katika aya hizo kile malaika Gabrieli alichomwambia Danieli jinsi jibu la maombi yake lilivyotolewa kwa utaratibu. Hii inatuonyesha jinsi Bwana yu tayari kusikia maombi ya watu wake. Nguvu za Danieli ziko katika kujitolea kwake kwa sala na ni somo kwetu sisi. Sio tu katika majira ya hali mbaya bali tunapaswa kuja kwa Mungu kila siku katika sala.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tunapaswa kujifunza nini kutoka kwa maisha ya Daniel?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries