Swali
Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa maisha ya Daudi?
Jibu
Tunaweza kujifunza mengi kutoka kwa maisha ya Daudi. Daudi alikuwa mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu (1 Samweli 13: 13-14; Matendo 13:22)! Kwanza tunaelezwa juu ya Daudi baada ya Sauli, baada ya watu kulazimisha, alifanywa kuwa mfalme (1 Samweli 8: 5, 10: 1). Sauli hakuwa wa kiwango cha mfalme ambacho Mungu alitaka. Wakati Mfalme Sauli alikuwa akifanya kosa moja juu ya lingine, Mungu alimtuma Samweli kumtafuta mchungaji wake aliyechaguliwa, Daudi, mwana wa Yese (1 Samweli 16:10, 13).
Daudi anakisiwa kuwa na umri wa kati ya miaka kumi na miwili hadi kumi na sita wakati alitiwa wakufu kama mfalme wa Israeli. Alikuwa kitinda mimba wa wana wa Yese na basi hakukuwa na uwezakano wake kuwa mfalme, wakati tunazungumza kiubinadamu. Samweli alidhani Eliabu, ndugu mkubwa wa Daudi, hakika alikuwa mafuta. Lakini Mungu akamwambia Samweli, "Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo" (1) Samweli 16: 7). Wana saba wa Yese walipita mbele ya Samweli, lakini Mungu hakuchagua hata mmoja wao. Samweli alimuuliza Yese ikiwa ana wana wengine zaidi. Kijana Daudi, alikuwa nje akilichunga kondoo. Basi wakamwita huyo mvulana ndani ya jumba naye Samweli akamtia Daudi mafuta "na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile" (1 Samweli 16:13).
Biblia pia inasema kwamba Roho wa Bwana alimwondoka Mfalme Sauli na roho mbaya ukamteza (1 Samweli 16:14). Watumishi wa Sauli walipendekeza mcheza ngoma, na mtumishi mmoja akampendekeza Daudi, akisema, "Tazama, nimemwona mwana mmoja wa Yese, Mbethlehemi, aliye stadi wa kupiga kinubi, tena ni mtu shujaa, hodari wa vita, anenaye kwa busara, mtu mzuri, ambaye Bwana yu pamoja naye"(1 Samweli 16:18). Hivyo ndivyo Daudi aliingia katika utumishi kwa mfalme (1 Samweli 16:21). Sauli alifurahishwa Daudi, naye akawa mmoja wa kumchukulia Silaha zake.
Upendo wa Sauli kwa Daudi ulipotea haraka pindi Daudi aliapoanza kuwa mshupafu na sifa zake kuenea. Katika hadithi moja ya kibiblia zinazojulikana zaidi, Daudi alimuua Goliathi. Wafilisti walikuwa wanapigana na Waisraeli na wakacheka majeshi ya Israeli juu ya ubingwa wa Goliathi kutoka Gathi. Walipendekeza vita kati ya Goliati na yeyote angeweza kupigana naye. Lakini hakuna mtu yeyote katika Israeli alijitokeza kupigana na jitu hili. Kaka zake Daudi wakubwa walikuwa sehemu ya jeshi la Sauli; baada ya Goliathi kuwadharau Waisraeli kwa siku arobaini, Daudi akawatembelea ndugu zake kwenye uwanja wa vita na kusikia majivuno ya Wafilisiti. Mchungaji kondoo mdogo akauliza, " Daudi akaongea na watu waliosimama karibu, akisema, Je! Atafanyiwaje yeye atakayemwua Mfilisti huyo, na kuwaondolea Israeli aibu hii? Maana Mfilisti huyu asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya Mungu aliye hai?" (1 Samweli 17:26). Kakaze wakubwa wa Daudi walikasirika na kumwona Daudi kuwa na kiburi na alikuwa amekuja tu kuangalia vita. Lakini Daudi aliendelea kuzungumzia suala hilo.
Sauli aliposikia yale Daudi alikuwa anasema alitumana aitwe. Daudi akamwambia Sauli, "Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu" (1 Samweli 17:32). Sauli hakumwamini; Daudi hakuwa askari aliyefusu. Daudi alitoa sifa zake za uchungaji, akiwa makini kutoa utukufu kwa Mungu. Daudi alikuwa amewaua simba na dubu waliwavamia kondoo wake, na akasema kuwa Mfilisti huyo angekufa kama wao kwa sababu alikuwa "amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai." Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu" (1 Samweli 17: 36-37). Sauli alikubali shingo upande, na akataka kuwa Daudi avae silaha za Sauli katika vita. Lakini Daudi hakuwa ameizoea silaha hiyo na aliiacha nyuma. Daudi alichukua pamoja naye fimbo yake, mawe laini matano, mfuko wa kichungaji wake, na kombeo. Mfilisti hakushutushwa hata kidogo na Daudi, hata Daudi vile vile hakuogopa jitu lile. "Daudi akamwambia Mfilisti huyo," Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu " (1 Samweli 17: 45-46). Tumaini la Daudi kwa Mungu na bidii yake kwa ajili ya utukufu wa Mungu ni za ajabu. Daudi alimwua yule Mfilisti. Pia aliingia katika utumishi wa Sauli wakati wote, hakurudi tena kuchunga kondoo wa baba yake.
Ilikuwa ni wakati huu Yonathani mwana wa Sauli, "akawa mmoja rohoni na Daudi" (1 Samweli 18: 1). Urafiki wa Daudi na Yonathani ni funzo kwa urafiki mwingi hii leo. Ingawa baba yake alikuwa mfalme na Yonathani kwa kawaida angekuwa mrithi wa kiti cha ufalme, Yonathani alichagua kumuunga Daudi. Alielewa na kukubali mpango wa Mungu na kutunza urafiki wake kutokana na ule wa baba yake mauaji (1 Samweli 18: 1-4, 19-20). Yonathani anaonyesha upendo wa unyenyekevu usio na ubinafsi (1 Samweli 18: 3, 20:17). Wakati wa utawala wa Daudi, baada ya kifo cha Sauli na Yonathani, Daudi alitafuta mtu yeyote wa uzao wa nyumba ya Sauli ambaye alikuwa amebaki ili aweze kuonyesha wema kwa Yonathani (2 Samweli 9: 1). Kwa hakika, hawa marafiki wawili walijali masilahi ya mwingine sana na kuheshimiana.
Baada ya tukio na Goliathi, umaarufu wa Daudi uliendelea kuenea. Shangwe na nderemo katika kambi ya Sauli ilikuwa ya kutetemesha watu walipokuwa wakiimba nyimbo za sifa za Daudi na kumtukana Mfalme Sauli, na kusababisha wivu mkali ndani ya Sauli ambao haukuisha (1 Samweli 18: 7-8).
Wivu wa Sauli kwa Daudi uligeuka na kuwa mauaji. Kwanza alijaribu kumfanya Daudi auawe kwa mikono ya Wafilisti kwa kumuuliza Daudi awe mwana-mkwe. Mfalme akamuoza bintiye kwa Daudi kama tuzo kwake Daudi la kutumikia jeshi lake. Daudi, kwa unyenyekevu alikataa, na bintiye Sauli akaozwa kwa mwingine (1 Samweli 18: 17-19). Bintiye Sauli mwingine, Mikali, alikuwa amempenda Daudi, hivyo Sauli akamsii Daudi amwoe. Daudi tena alikataa kwa sababu ya uchochore wake na kutoweza kumudu kulipa mahari kwa binti wa mfalme. Sauli aliitisha Ngozi mia moja za Wafilisti, akitumaini Daudi atauawa na adui hao. Wakati Daudi aliwaua Wafilisti mia mbili, idadi ikiwa mara mbili ya malipo aliyohitajika, Sauli aligundua kwamba mpango wake ulishindwa, na hofu yake kwa Daudi iliongezeka (1 Samweli 18: 17-29). Yonathani na Mikali walimwonya Daudi dhidi nia ya mauaji ya baba yao, na Daudi akatoroka kutoka kwa mfalme kwa mwaka uliofuatia. Wakati huu akiwa ametoroka Daudi alitunga nyimbo nyingi, ikiwa ni pamoja na Zaburi 57, 59, na 142.
Ingawa Sauli hakuacha kumfuata Daudi kwa nia ya kumwua, Daudi kamwe hakuinua mkono dhidi ya mfalme wake na mtiwa mafuta wa Mungu (1 Samweli 19: 1-2; 24: 5-7). Sauli alipokufa, Daudi aliomboleza (2 Samweli 1). Hata akijua kwamba Sauli alikuwa mtiwa mafuta wa Mungu, Daudi hakulazimiza kupata kwake kiti cha ufalme. Aliheshimu ukuu wa Mungu na kuheshimu mamlaka ambayo Mungu alikwisha weka wakati huo, akiamini kwamba Mungu atatimiza mapenzi Yake wakati wake.
Akiwa mtoro, Daudi alianzisha jeshi kubwa na nguvu kutoka kwa Mungu alishinda kila mtu aliye simama kumpinga, na aliwomba Mungu idhini na maagizo kabla ya kwenda vitani, tabia aliyoendeleza hata akiwa mfalme (1 Samweli 23: 2-6) ; 9-13; 2 Samweli 5: 22-23). Mara tu alipotawazwa kuwa mfalme, Daudi alizalia kuwa kamanda mwenye nguvu wa kijeshi na askari. Samweli wa pili 23 inaelezea baadhi ya matendo ya ushindi ya Daudi "watu wenye nguvu." Mungu alimheshimu na kutuza utiifu wake na akampa Daudi mafanikio katika kila kitu alichofanya (2 Samweli 8: 6).
Daudi akaanza kuoa wake wengine. Alioa Abigaili, mjane mji wa Karmeli, wakati alipokuwa ametoroka kutoka kwa Sauli (1 Samweli 25). Daudi pia alikuwa amemwoa Ahinoamu wa Yezreeli. Sauli alikuwa amemwoza Mikali aliyefaa kuwa mke wa Daudi kwa bwana mwinginge (1 Samweli 25: 43-44). Baada ya kifo cha Sauli Daudi alipakwa mafuta na kuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda (2 Samweli 2: 4), na basi ikabidi apishane na nyumba ya Sauli kabla yake kutiwa mafuta juu ya Israeli akiwa na umri wa miaka thelathini (2 Samweli 5: 3-4). Sasa akiwa mfalme, Daudi alimchukua Mikali tena awe mkewe tena (2 Samweli 3:14). Daudi pia aliikomboa Yerusalemu, akiuchukua kutoka kwa Wayebusi, na akawa na nguvu zaidi kwa kuwa Bwana Mwenyezi-Mungu alikuwa pamoja naye (2 Samweli 5: 7).
Sanduku la Agano lilikuwa limechukuliwa hapo awali na Wafilisti (1 Samweli 4). Baada ya kurudishwa kwake Israeli, sanduku liliwekwa katika Kiriath Yearimu (1 Samweli 7: 1). Daudi alitaka kurudisha sanduku la agano kule Yerusalemu. Lakini Daudi hakufuata baadhi ya maelezo ya Mungu jinsi ya kuisafirisha sanduku na ni nani angeibeba. Hii ilisababisha kifo cha Uza ambaye wakiwa katikati harakati ya maadhimisho yote, alitaka kulikaza lile sanduku kwa mkono wake. Mungu akampiga Uza, naye akakufia kando ya lile sanduku (2 Samweli 6: 1-7). Kwa kumwogopa Bwana, Daudi aliacha uhamisho wa sanduku na kuliacha likae kwa Obed-edomu (2 Samweli 6:11).
Miezi mitatu baadaye, Daudi alianzisha tena mpango wa kuileta sanduku Yerusalemu. Wakati huu, alifuata maelezo. Pia "alicheza kwa nguvu zake zote mbele ya Mwenyezi-Mungu" (2 Samweli 6:14). Wakati Mikali alipoona Daudi akiabudu kwa njia hiyo, "akamdharau moyoni mwake" (2 Samweli 6:16). Alimuuliza Daudi yeye kama mfalme anawezaje kufanya hivyo bila heshima ya cheo chake mbele ya watu wake. "Daudi akamwambia Mikali, "Nilikuwa mbele ya Mwenyezi-Mungu ambaye alinichagua mimi badala ya baba yako, na jamaa yake, ili kuniteua kuwa mkuu juu ya Israeli, watu wake Mwenyezi-Mungu, kwa hiyo mimi nitacheza tu mbele ya Mwenyezi-Mungu. Nitajishusha mwenyewe Zaidi kuliko sasa. Wewe utaniona kuwa si kitu, lakini hao watumishi wa kike uliowasema wataniheshimu" (2 Samweli 6: 21-22). Daudi alielewa kwamba ibada ya kweli inapaswa kuwa ya Mungu pekee. Hatumwabudu kwa manufaa ya maoni ya wengine bali kwa mjibu wa itikio la unyenyekevu kwa Mungu (Yohana 4:24).
Baada ya Daudi kukaa katika ikulu yake na kuwa na amani na adui zake, alitaka kumjengea Mungu hekalu kwa (2 Samweli 7: 1-2). Nabii Nathani akamwambia Daudi kufanya jinsi alivyotaka. Lakini Mungu akamwambia Nathani kwamba Daudi hatakuwa ndiye atakayejengea hekalu lake. Badala yake, Mungu akaahidi kunjenga nyumba Daudi. Ahadi hii ni pamoja na utabiri kwamba Sulemani angejenga hekalu. Lakini pia ilisungumzia juu ya Masihi aliyekuwa aje, Mwana wa Daudi ambaye angeongoza kutawala milele (2 Samweli 7: 4-17). Daudi akajibu kwa unyenyekevu na hofu: "Mimi ni nani, ee Bwana Mungu, na jamaa yangu ni nini hata ukaniinua mpaka hapa nilipo leo!" (2 Samweli 7:18, angalia 2 Samweli 7: 18-29 kwa sala nzima ya Daudi). Kabla ya kifo chake, Daudi alifanya maandalizi ya kujengwa kwa hekalu. Sababu ya Mungu ya kutomruhusu Daudi kujenga hekalu ni kwamba alikuwa amemwaga damu nyingi, lakini mwanawe Daudi angekuwa mtu wa amani na sio mtu wa vita. Sulemani angejenga hekalu (1 Mambo ya Nyakati 22).
Daudi alimwaga damu nyingi kwa sababu ya vita. Lakini, katika tukio la uovu, Daudi pia alikuwa mmoja wa watu ambaye alikuwa na wapiga vita shupavu. Ijapokuwa Daudi alikuwa mtu aliyependwa sana na Mungu, alikuwa mwanadamu na mwenye dhambi. Wakati majeshi yake yalipokuwa vitani wakati mmoja, Daudi akabaki nyumbani. Kutoka juu ya dari yake aliona mwanamke mzuri akioga. Akaona kwamba alikuwa Bath-sheba, mke wa Uria Mhiti, mmoja wa watu wake wenye nguvu waliokuwa katika vita, naye Daudi akatuma wajumbe kwake. Daudi akafanya ngono na Bathsheba, naye akashika mimba. Daudi alimwita Uria kutoka kwenye vita, akiwa na tumaini kuwa Uria atachumbiana na mkewe na kumwamini kuwa mtoto ni wake, lakini Uria alikataa kwenda nyumbani huku wapiganaji wenzi wangali vitani. Basi Daudi alipanga Uria kuuawa katika vita. Daudi kisha akaoa Bath-sheba (2 Samweli 11). Tukio hili katika maisha ya Daudi linatuonyesha kwamba kila mtu, hata kama ni wale tunaowaheshimu sana, hupambana na dhambi. Pia hutumika kama hadithi ya tahadhari kuhusu majaribu na jinsi dhambi inaweza kuongezeka kwa haraka.
Nabii Nathani alimkabili Daudi juu ya dhambi yake na Bath-sheba. Daudi aliitikia kwa kutubu. Aliandika Zaburi 51 wakati huu. Hapa tunaona unyenyekevu wa Daudi na moyo wake wa kweli kwa Bwana. Ingawa Nathani alimwambia Daudi kwamba mwanawe atakufa kutokana na dhambi yake, Daudi aliomba kwa Bwana ili mwanawe aweze kuishi. Uhusiano wa Daudi na Mungu ulikuwa kwamba alikuwa tayari kuendeleza imani na kutumaini kwamba Mungu anaweza kumsamehe. Mungu alipotekeleza hukumu yake, Daudi alikubali kabisa (2 Samweli 12). Katika hadithi hii tunaona pia neema na uhuru wa Mungu. Sulemani, mwanawe Daudi ambaye alimrithi na kupitia yeye Yesu alikuja, alizaliwa na Daudi na Bath-sheba.
Mungu alikuwa amemwambia Daudi, kupitia nabii Nathani, kwamba upanga hautaondoka nyumbani kwake. Hakika, nyumba ya Daudi ikawa na shida nyingi tangu wakati huo. Tunaona hili kati ya watoto wa Daudi wakati Amnoni alivyomnajisi Tamari, na kusababisha Absalomu kumwua Amnoni, na njama ya Absalomu dhidi ya Daudi. Nathani alikuwa amemwambia Daudi kwamba wake wake watapeanwa kwa mtu aliye wa karibu naye; hii haingetokea kwa siri kama vile dhambi ya Daudi na Bath-sheba ilikuwa, bali itakuwa hadharani. Unabii huu ulitimizwa wakati Abisalomu alilala na masuria wa baba yake juu ya paa ili watu wote waone (2 Samweli 16).
Daudi ndiye mtunzi wa Zaburi nyingi. Katika zaburi hizo tunaona jinsi alivyotami kumtukuza Mungu. Mara nyingi alichukuliwa kuwa mfalme mchungaji na mtunga mashairi. Maandiko humwita "Mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye kupendeza" (2 Samweli 23: 1). Maisha ya Daudi yalionekana kuwa na hisia nyingi za kibinadamu-kijana mchungaji wa kawaida aliye na ujasiri mkubwa katika uaminifu wa Mungu ambaye aliheshimu mamlaka, alikimbilia usalama wake, na akawa mfalme dhidi ya wafalme wote wa Israeli wa baadaye. Aliona ushindi mwingi wa kijeshi. Pia akaanguka katika dhambi kubwa, na familia yake ikatezeka kwa sababu hiyo. Lakini kwa njia yote Daudi alimgeuka kwa Mungu na kumtumaini. Hata katika Zaburi wakati Daudi anapokufa moyo au amekata tamaa, tunamwona anainua macho yake kwa Muumba wake na kumpa sifa. Kumtegeme na Mungu huku na kuendelea kutafuta uhusiano na Mungu ni baadhi ya mambo ambayo humfanya Daudi awe mtu ambaye amependwa na Mungu.
Mungu alimwahidi Daudi kuwa mzao wake atatawala katika kiti cha enzi milele. Mfalme wa milele ni Yesu, Masihi na Mwana wa Daudi.
English
Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa maisha ya Daudi?