Swali
Filipo alikuwa katiak Biblia?
Jibu
Kuna wanaume wanne tofauti wanaoitwa Filipo waliotajwa katika Biblia. Filipo ilikuwa jina la wana wawili wa Mfalme Mkuu Herode aliowazaa na wanawake tofauti (Luka 3: 1 na Mathayo 14: 3). Wanaume wengine wawili waliokuwa wanaitwa Filipo katika Biblia walikuwa watumishi wa Kristo na walikuwa wa msaada sana katika kanisa la kwanza: Filipo aliyekuwa mwanafunzi na mtume wa Kristo, na Filipo mwinjilisti.
Mwanafunzi aliyeitwa Filipo alikuwa pamoja na Petro na Andrea, kutoka Bethsaida huko Galilaya (Yohana 1:44, 12:21). Yesu alimwita Filipo, ambaye alikuwa mwanafunzi wa Yohana Mbatizaji (Yohana 1:43), kisha Filipo akaenda na kumwona Nathanaeli na kumwambia kuhusu Yesu. Nathanaeli pia akawa mwanafunzi wa Yesu. Biblia haina maelezo mengi kuhusu maisha ya Filipo au wanafunzi wengine, lakini Yohana ameandika mara kadhaa kuhusu Filipo akizungumza na Yesu.
Kitendo cha kwanza katika kumbukumbu ya Filipo kama mwanafunzi wa Yesu kilikuwa ni kwenda kumwambia rafiki yake Nathanaeli. Baadaye, Wagiriki wengine, hasa, Wagiriki kutoka Bethsaida walimwendea Filipo na kumwomba awajulishe kuhusu Yesu (Yohana 12: 20-22). Filipo ndiye mwanafunzi ambaye alihesabu kiasi cha pesa ambacho kingeweza kulisha watu 5,000 (Yohana 6: 7). Baada ya Mlo wa Mwisho, Filipo aliomba kwamba Yesu awaonyeshe Baba, na kusababisha maneno ya Yesu, "Aliyeniona mimi amemwona Baba" (Yohana 14: 8-9). Kwa mara ya mwisho Biblia inamtaja mwanafunzi Filipo wakati alipokusanyika na wanafunzi wengine huko Yerusalemu ili kuomba baada ya Bwana kupaa mbinguni (Matendo 1:13). Maandiko yanasema kwamba Filipo alikwenda Frigia (katika Uturuki wa leo) kama mishonari na akauawa huko Hierapoli.
Tunapata kutofautisha Filipo aliyekuwa mwanafunzi na mwenzake aliyeitwa jina lilo hilo kwa kumpa jina "Filipo mhubiri" au "Filipo shemasi." Mara nyingi hufikiriwa kuwa Filipo huyu alikuwa mmoja wa watu sabini na wawili ambao Yesu aliwatuma katika Luka 10 : 1, ingawa Biblia haionyeshi uhusiano huo. Tunajua kwamba Filipo alikuwa mmoja wa mashemasi saba wa awali waliochaguliwa kutumikia kanisa la Yerusalemu (Matendo 6: 5). Filipo alikuwa na moyo kwa uinjilisti, na, wakati "mateso makubwa" yalipotokea katika Matendo 8: 1, Filipo aliondoka Yerusalemu kuwa mwinjilisti huko Samaria (Matendo 8: 5-12). Baada ya kanisa la Samaria kuanzishwa, Filipo alitumika na Roho Mtakatifu kuleta injili kwa mtu wa kushi, towashi mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi. Filipo alimpata ameketi garini mwake akisoma na kujaribu kuelewa chuo cha nabii Isaya. Filipo alijitolea kumuelezea, na huyo mtu towashi akamwomba aje na kukaa pamoja naye. Hatimaye, towashi aliokolewa na kubatizwa (Matendo 8: 26-39). Mara baada ya kubatizwa, Roho wa Bwana alimchukua Filipo kwenda Azoto, ambako aliendelea kuhubiri injili katika miji yote hata akafikia Kaisaria (Matendo 8:40).
Miaka ishirini baadaye, Filipo ametajwa tena, bado huko Kaisaria (Mdo. 21: 8-9). Paulo, Luka na wengine walikuwa wakienda Yerusalemu, na wakafika kwa nyumba ya Filipo huko Kaisaria. Walikaa na Filipo kwa siku kadhaa. Filipo alikuwa na binti wanne ambao hawakuwa wameolewa wakati huo, wote walikuwa na karama ya unabii. Hiyo ndiyo mara ya mwisho Biblia inamtaja mhubiri Filipo.
English
Filipo alikuwa katiak Biblia?