settings icon
share icon
Swali

Hawa alikuwa nani katika Biblia?

Jibu


Hawa katika Biblia alikuwa mke wa Adamu, mwanaume wa kwanza ambaye Mungu aliumba. Hawa alikuwa mamake Kaini, Abeli, Seti na "wana wengine na binti" (Mwanzo 4: 1-2, 25; 5: 4). Hawa alikuwa mwanamke wa kwanza, mke wa kwanza, na mama wa kwanza ulimwenguni.

Jina Hawa linatokana na neno la Kiebrania chavâh, ambalo linamaanisha "walio hai" au "maisha". Aliitwa "Hawa" kwa sababu alikuwa mama wa wote wanaoishi (Mwanzo 3:20). Mungu alimuumba baada ya kumruhusu Adamu kuona kwamba hakuwa na mwenzi aliyefaa kati ya wanyama-yaani, hakukuwa na kiumbe mwingine kama yeye mwenyewe. Kwa hivyo Mungu aliumba Hawa kama mwenzi wa Adamu. Hawa aliumbwa kwa mfano wa Mungu na vilevile Adamu (Mwanzo 1:27).

Mungu alitoa amri kwa Adamu na Hawa wakati walipokuwa wanaishi katika bustani ya Edeni. Aliwaambia wasile mti unaoitwa "mti wa ujuzi wa mema na mabaya" kwa sababu, alionya, siku watakayokula matunda ya mti huo, bila shaka watakufa (Mwanzo 2:17). Biblia haituelezi ni kwa muda gani Adamu na Hawa waliishi katika bustani bila ya tukio, lakini kwa wakati mmoja Hawa alijaribiwa na kula kutoka kwenye mti huo waliokatazwa. Alidanganywa na nyoka (1 Timotheo 2: 13-14) ambaye, kwa ujumla inaaminika kuwa alikuwa kiumbe aliyetumiwa na Shetani. Nyoka alimfanya Hawa kuwa na shaka shaka katika mawazo kwa kumuuliza kwamba Mungu alimaanisha kweli alichosema katika kuzuia kula matunda kutoka kwenye mti huo (Mwanzo 3: 1). Kisha nyoka akamdanganya Hawa: "Hakika hamtakufa. . . . Kwa maana Mungu anajua kwamba mtakayokula matunda ya mti huo macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya "(Mwanzo 3: 4-5). Hawa alitwaa tunda na kulila na kisha akampa mumewe Adamu, ambaye pia alikula. Adamu na Hawa walielewa mara moja yale waliyokuwa hawajapata kuelewa-macho yao yalifumbuliwa na kuona wema na mabaya. Lakini Mungu hakusema uongo -kifo kikawa matokeo ya uasi wa Hawa na Adamu.

Kifo kikaja kwa wanadamu wote kama matokeo ya kile Hawa alichochewa kufanya na chaguo la Adamu la kutenda dhambi. Laana mbili zilitolewa kwa Hawa na binti zake zote. Kwanza, Mungu alizidisha maumivu ya Hawa katika kuzaa. Pili, Mungu alisema kuwa uhusiano kati ya mwanaume na mwanamke utakwa migogoro (Mwanzo 3:16). Laana mbili yameonekana kuwa ya kweli katika maisha ya kila mwanamke katika historia. Bila kujali maendeleo mengi ya matibabu tunayopata, uzazi ni daima maumivu na maumivu kwa mwanamke. Haijalishi maendeleo katika sekta ya afya, kujifungua mtoto huwa ni uchungu kwa mwanamke yeyote. Haijalishi jinsi jamii inavyozidi kuendelea, uhusiano wa mwanaume na mwanamke bado ni mapambano ya nguvu, vita vya jinsia na ugomvi.

Hawa alikuwa mama wa wanaoishi wote na pia alikuwa wa kwanza kupokea laana hizi maalum. Hata hivyo, Hawa atakombolewa pamoja na Adamu kwa sababu ya Adamu wa pili, Kristo, ambaye hakuwa na dhambi (Warumi 5: 12-14). "Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. . . . 'mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. uzima "(1 Wakorintho 15:22, 45).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Hawa alikuwa nani katika Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries