settings icon
share icon
Swali

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Timotheo?

Jibu


Timotheo, mpokeaji wa barua mbili za Agano Jipya ambazo zinaitwa kwa jina lake, alikuwa mwana wa baba Mgiriki na mama Myahudi. Alijiunga na Paulo wakati wa safari za baadaye za umishonari wa Paulo. Paulo anamwita Timotheo "mwanangu hasa katika imani" (1 Timotheo 1:2). Huenda hakuwa mkubwa kuliko ujana/mapema ya miaka ishirini wakati alijiunga na Paulo lakini tayari alikuwa amejipatia sifa kama mwaminifu, na wazee walimwona. Pengine alisikia na kuitikia injili wakati Paulo alipitia eneo la Derbe na Listra kwenye safari yake ya kwanza ya umishonari, lakini hatujui kwa hakika. Timotheo alitumikia kama mwakilishi wa Paulo kwa makanisa kadhaa (1 Wakorintho 4:17, Wafilipi 2:19), na baadaye alikuwa mchungaji huko Efeso (1 Timotheo 1:3). Timotheo pia anatajwa kuwa pamoja na Paulo wakati Paulo aliandika barua nyingi za Agano Jipya-2 Wakorintho, Wafilipi, Wakolosai, 1 na 2 Wathesalonike, na Filemoni.

Paulo anasema Timotheo alikuwa na "imani ya kweli," sawa na ile iliyoishi ndani ya mamake na bibi (2 Timotheo 1:1-5). Eunice na Lois walitayarisha moyo wa Timotheo kumkubali Kristo kwa kumfundisha Timotheo Maandiko Matakatifu ya Agano la Kale na kumtengeneza "kutoka ukembe" ili kumtambua Masihi wakati atakapotokea (2 Timotheo 3:15). Wakati Paulo alikuja kumhubiri Kristo, wote watatu walikubali mafundisho yake na wakawasilisha maisha yao kwa Mwokozi. Sisi, pia, tunatakiwa kuwaandaa watoto wetu kuwa tayari wakati Kristo ataingia ndani ya mioyo yao. Wanapaswa kujua jinsi ya kutambua mvuto huo kwa roho zao kama unaotoka kutoka kwa Mwokozi, na njia pekee ya kufanya hivyo ni kufuata mfano wa Eunice na Lois na kuwafundisha watoto wetu Neno la Mungu.

Katika barua ya kwanza ya Paulo kwa Timotheo, alimpa maagizo na ushauri kwa kuongoza kanisa. Pia alimsihi Timotheo hasiruhusu wengine kumdharau kwa sababu ya ujana wake, bali kuweka mfano kwa waumini wengine "katika hotuba, katika mwenendo, katika upendo, katika imani na katika usafi" (1 Timotheo 4:12). Paulo alimwambia Timotheo kujitolea kusoma Maandiko, kuhimiza, na kufundisha, na hasipuuze kipawa alichopewa. Paulo pia alimshauri Timotheo kujiangalia mwenyewe. Maagizo haya yanaendelea kuwa muhimu kwa waumini leo. Sisi pia, tumeitwa "kufuata haki, utauwa, imani, upendo, saburi na upole. Piga vita vile vizuri vya Imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele mbele ya mashahidi wengi "(1 Timotheo 6:11-12).

Inaonekana kwamba Timotheo alikuwa na ugonjwa wa kudumu ambao ulihitaji uangalifu fulani (1 Timotheo 5:23). Paulo alimshauri juu ya mabadiliko ya mlo ili kutuliza hali yake. Kutokana na mfano huu tunajifunza kwamba sio mapenzi ya Mungu kumponya mtu kimuujiza; wakati mwingine, uponyaji unakuja kupitia "asili" zaidi, inamaanisha, ikiwa utakuja kwa vyovyote.

Katika barua yake ya pili kwa Timotheo, Paulo alimwonya Timotheo kuhusu walimu wa uongo kwamba atakutana na kumwambia aendelee katika mambo aliyojifunza kwa sababu anajua tabia ya wale aliojifunza kutoka kwao, yaani Paulo mwenyewe na mamake na bibi yake (2 Timotheo 3:14-15). Ukweli Timotheo alifundishwa tangu ukembe — ukweli juu ya dhambi na mahitaji yetu ya Mwokozi-alikuwa na uwezo wa kumfanya mwenye "hekima kwa ajili ya wokovu" (2 Timotheo 3:15). Kama wazazi, tunapaswa kuwaandaa watoto wetu ili kutofautisha ukweli kutoka kwa kosa. Na kama waumini, tunapaswa kusimama imara katika ukweli tuliojifunza, si kushangaa au kuyumbishwa na upinzani na walimu wa uongo.

Paulo pia alimwambia Timotheo, "jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli" (2 Timotheo 2:15). Ushauri huu ni muhimu kwa Wakristo wote. "Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makossa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema" (2 Timotheo 3:16-17). Paulo alimshauri Timotheo, "mwanawe mpendwa" (2 Timotheo 1:2), kutoka kwa moyo wa upendo, akimtaka Timotheo kusimama imara katika imani yake mwenyewe na kuwaongoza waumini wengine vyema. Timotheo hakika anaonekana kuwa mwaminifu; tunapaswa kufuata mfano wake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Timotheo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries