settings icon
share icon
Swali

Yohana Marko alikuwa nani katika Biblia?

Jibu


Yohana Marko, mara nyingi anaitwa Marko, ndiye mwandishi wa Injili ya Marko. Alikuwa muumini katika kanisa la kwanza ambalo linazungumziwa zaidi katika kitabu cha Matendo. Yohana Marko mara ya kwanza anatajwa, anatajwa kuwa mwana wa mwanamke mmoja aitwaye Mariamu (Mdo. 12:12), ambaye nyumba yake ilikuwa inatumika na waumini kukusanyika ili kuomba. Baadaye, Marko anatajwa kuwa rafiki mwenza wa Barnaba na Paulo wakati wa safari zao pamoja (Matendo 12:25). Yohana Marko pia alikuwa binamuye Barnaba (Wakolosai 4:10).

Yohana Marko alikuwa msaidizi wa safari ya kwanza ya Paulo na Barnaba ya umisionari (Matendo 13: 5). Hata hivyo, hakukaa nao safari nzima. Yohana Marko aliachana na Paulo na Barnaba huko Pamfulia na kuacha kazi (Matendo 15:38). Biblia haisemi ni kwa nini Marko aliwaacha, lakini kuondoka kwake kulikuja baada ya kipindi kisicho na mafanikio huko Kipro (Matendo 13: 4-12). Ni mtu mmoja tu amenakiliwa kuoka huko Kipro, lakini kulikuwano na upinzani mkali wa pepo. Inawezekana kwamba kijana Yohana Marko alikuwa amekata tamaa kwa ugumu wa kazi na akaamua kurudi nyumbani kwenye faraja.

Wakati mwingine baadaye, baada ya Paulo na Barnaba walikuwa wamerudi kutoka safari yao ya kwanza, Paulo alionyesha hamu ya kurudi kwa wapendwa katika miji ambayo walikuwa wameishaimbelea hapo awali ili kuona jinsi kila mtu alikuwa anaendelea (Matendo 15:36). Barnaba alikubali, kwa masharti kuwa watamchukua Yohana Marko. Paulo alikataa kuwa na Marko kwenye safari hiyo, hata hivyo, huku akitoa mfano wa jinsi alivyowatenga hapo awali. Paulo na Barnaba walikuwa na "mashindani makali" juu ya Yohana Marko (Mdo. 15:39) na wakatofautiana na wao wawili wakaenda safari tofauti. Barnaba alimchukua Yohana Marko na kwelekea Kipro, na Paulo akachukua Sila pamoja naye kupitia Shamu na Kilikia ili kuwahamasisha waumini katika makanisa ya maeneo hayo (Matendo 15: 39-41).

Barnaba, "mwana wa faraja" (Matendo 4:36), alitaka kusamehe Yohana Marko makossa yake na kumpa fursa nyingine. Paulo alichukua mtazamo mkali kidogo: akishikilia kuwa huduma ya umisionari inahitaji kujitolea, uamuzi, na uvumilivu. Paulo alimwona Yohana Marko kuwa hatari kwa utume wao. Luka, mwandishi wa Matendo, haungi upande wowote au kuwasilisha Paulo au Barnaba kuwa sawa. Ameandika ukweli tu. Ni muhimu kutambua kwamba, mwishoni, makundi mawili ya wamisionari yalitumwa- Zaidi ya eneo moja wamisionari walieneza injili.

Yohana Marko aliondoka kwenda Kipro na binamuye Barnaba, lakini huo sio mwisho wa hidhiti yake. Miaka mingi baadaye, yeye aliungana na pamoja na Paulo, ambaye anamwita "mfanyakazi mwenza" (Filemoni 1:24). Na karibu na mwisho wa maisha ya Paulo, Paulo anatuma ombi kwa Timotheo kutoka gerezani Roma: "Umtwae Marko, umlete pamoja nawe, maana anifaa kwa utumishi" (2 Timotheo 4:11). Kwa wazi, Yohana Marko alikuwa amekomaa katika miaka hiyo mingi na alikuwa mtumishi mwaminifu wa Bwana. Paulo alitambua ukuaji wake na akamwona kuwa rafiki mwema.

Yohana Marko aliandika Injili inayoitwa kwa jina lake kati yam waka wa AD 55 na 59. Kunaweza kuwa na kumbukumbu ya Yohana Marko katika Marko 14: 51-52. Katika kifungu hicho kijana mdogo, aliinuka kutoka usingizi usiku ambao Yesu alikamatwa, akajaribu kufuata Bwana, huku kundi la watu waliokuwa wamemtia Yesu jela walijaribu kumkimbiza. Huyo kijana alitoroka na kupotelea gizani. Ukweli kwamba tukio hili limetajwa katika Injili ya Marko tu na ukweli kwamba kijana huyo haijulikani-imesababisha wasomi wengine kuhitimiza kwamba kijana huyo anayetorekea gizani ni Yohana Marko.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Yohana Marko alikuwa nani katika Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries