settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inasema nini kuhusu kawaida ya ibada na sala ya dini? Je! Mkristo anapaswa kushiriki katika ibada ya kawaida na sala ya dini?

Jibu


Liturujia ni muundo wa kawaida wa ushirika wa kidini. Maandiko hayaweki mfano wa kiwango cha ibada ya kanisa. Katika wakati huo huo, vifungu vingi vya Agano Jipya vinatupa viungo muhimu ambavyo vinapaswa kuwa sehemu ya kanisa lenye afya. Miongoni mwa hivi ni yafuatayo:

Ushirika wa kweli: kuwatendea waumini wengine jinsi walivyo-familia, Pamoja na upendo, umoja utokao kwa moyo, kutoa kwa ajili ya wengine hiyo ni kawaida kwa familia (Matendo 2:44-46).

Utunzaji wa maagizo: ubatizo wa waumini na ukumbusho wa Meza ya Bwana / ushirika Mtakatifu (Matendo 2:41, 42, 46; 1 Wakorintho 11: 23-32).

Kutunza kwa thabiti mafundisho ya mitume, usomaji wa Neno la Mungu, na mafundisho / mahubiri ya Neno la Mungu (Matendo 2:42; 1 Timotheo 4: 13-16; 2 Timotheo 4: 2).

Maombi na sifa, kwa kutegemea uongozi wa Roho Mtakatifu (Matendo 2: 42,47; Matendo 13: 1-4; 1 Timotheo 2: 1-8; Waefeso 6:18).

Uinjilishaji na uanafunzi, washiriki wote wa kanisa wakitumia vipaji vyao vya kiroho kumtumikia Kristo kama sehemu ya Mwili wa Kristo (Mathayo 28: 18-20; Matendo 1: 8; 1 Timotheo 4: 5; Waefeso 4: 11-16; Warumi 12: 3-8).

Huku makanisa mengine yakibandikwa kuwa ya "liturujia" kwa sababu ya utaratibu rasmi uliopangwa tayari na njia ya ibada, makanisa yote kwa kiwango fulani yana muundo ambao yanafuata kwa kawaida. Tofauti yao kubwa itakuwa kiwango ambacho hii ni kweli, na uwezekano wa kubadilisha muundo huo wa kawaida ikiwa ni lazima. Ni dhahiri kutokana na Matendo 13 kwamba kanisa katika mji wa Antiokia lilikuwa tayari kubadilika kwa kuwa walikuwa wamejiajilia kwa uongozi wa Roho Mtakatifu. Ikiwa kanisa ni la kiliturujia kiwango kwamba mabadiliko kulingana na uongozi Wake sio jambo ni la uwezekano, liturujia imekiuka mipaka. Kanisa ambalo ni la mpangilio haliwezi kuruhusu mwongozo wa Roho-tayari wana "ajenda" yao; hawahitaji Roho Mtakatifu.

Kuna hatari mbili za ziada zinazohusiana na ibada ya kiliturujia: (1) Ibada zilizobuniwa na mwanadamu zina makosa na kwa hivyo zinahitaji kuchunguzwa ili kuona ikiwa ni za kimaandiko. Lakini hii pia ni kweli kwa wote wanaoitwa makanisa ya kiliturujia na pia kwa wale ambao hawajapewa jina hilo. Katika visa vyote viwili wanadamu wenye makosa huweka muundo wa huduma. (2) Ibada ambazo zinataka kusoma kwa kurudia rudia sala, itikio, n.k., zinaweza kuanza kufanywa kwa kukariri bila kufikiria au ibada ya kweli kutoka moyoni. Na hii inapofanyika inakuwa "marudio ya bure." Lakini, hata hivyo, bado inawezekana sana kwa moyo mmoja wa dhati kumwabudu Mungu kwa maombi ya kurudia-rudia, n.k., anapofikiria kile kinachosemwa na hivyo kuingia katika maombi hayo kutoka moyoni. Kando na hayo, hata katika makanisa yasiyo ya kiliturujia, nyimbo fulani na kwaya kadhaa huimbwa kwa kurudiwa rudiwa wakati na bubeba hatari hiyo hiyo ya kuimbwa vizuri badala ya kutafakari juu ya kile kinachosemwa na kuimbwa.

Iwe kanisa ni la kuliturijia sio kitu cha maana kama vile mafundisho ya kanisan a ubora wa mchungaji kuwa kweli kimafunzo na wa kiroho (1 Timotheo 4:16; Matendo 2:42). Kukubaliana na maandiko sio kiliturijia, kinaamua ikiwa matendo ya kanisa yanaambatana na yale kanisa lililo na afya na la kibiblia.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inasema nini kuhusu kawaida ya ibada na sala ya dini? Je! Mkristo anapaswa kushiriki katika ibada ya kawaida na sala ya dini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries