Swali
Wazazi Wakristo wanapaswa kushughulikia kifo cha mtoto namna gani?
Jibu
Kama wazazi, hatuwezi kufikiri uzoefu zaidi wa kutisha kuliko kupoteza mtoto. Kwa kawaida wazazi wote wanatarajia watoto wao kuishi kuwaliko. Hasara hiyo ni tukio la ajabu ambalo huja na hisia kubwa ya maumivu na huzuni. Ni uzoefu unaobadili maisha ambayo huwa na changamoto za kipekee kwa wazazi wanapojaribu kujenga upya maisha yao bila mtoto wao.
Ingekuwa kiburi kwa mtu yeyote kuwaambia wazazi jinsi ya kushughulikia kifo cha mtoto wao. Hata hivyo, tunajua kwamba wale ambao hutoa maisha yao kwa Mungu wanaweza kufarijika tena kutokana na pigo hilo kwa namna ya haraka kuliko wale ambao hawana imani halisi na nzuri katika Muumba wetu. Sasa, wazazi wa Kikristo wanapaswa shughulikia kifo cha mtoto namna gani? Je! Biblia inasema jambo hilo, na ikiwa ni hivyo, kwa njia gani?
Kwanza, tunapaswa kutambua kwamba kila mtu hukabili huzuni kwa njia tofauti. Maumivu hutofautiana sana katika kiwango chao. Hisia hizi ni za kawaida na za asili. Pili, hakuna mzazi yeyote anayefarijika kikamilifu kutokana na kupoteza mtoto. Sio kama ugonjwa ambao tunapona kwalo. Washauri wengi wanaifananisha na uharibifu ya ubadilisho wa kimwili wa maisha. Hata hivyo, tunapaswa pia kujua kwamba hata ingawa daima tunaweza kuhisi pigo hilo, kiwango chake kinapungua kwa muda.
Ni imani katika Mungu mwenye upendo na milele ambaye hutuwezesha kuvumilia na kupona kutokana na kumpoteza mtoto, wakati mwingine kwa njia ambazo wengine hupata kuwa ya ajabu. Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwa Daudi katika hali ya kupoteza mtoto wake ambaye alikufa siku saba baada ya kuzaliwa (2 Samweli 12: 18-19). Kuna masomo kadhaa ya thamani tunayoweza kujifunza kutokana na kifungu hiki cha Maandiko ambacho kinaweza kuwasaidia wazazi wenye huzuni kukabiliana na wakati ujao kwa tumaini.
Moja ni kwamba Daudi aliomba kwa bidii kwa maisha ya mtoto wake (2 Samweli 12:16). Hii inapaswa kuwa kweli kwa wazazi wote wakati wote, na si katika wakati mgumu pekee. Wazazi tunapaswa kuomba kila siku kwa ajili ya watoto wetu, wakiomba Mungu awaangalie na kuwahifadhi. Vivyo hivyo, wazazi wanapaswa kuomba kwamba Mungu awape hekima na uongozi wa kiungu ili watoto wetu waweze kukua na maonyo ya Bwana (Waamuzi 13:12; Mithali 22: 6; Waefeso 6: 4).
Somo jingine tunalojifunza kutoka kwa Daudi ni jinsi alivyo kabiliana na kifo cha mtoto wake. Baada ya kugundua kuwa mtoto huyo amekufa, kuna uitikio unaonekana katika matendo Yake wakati "akainuka pale chini akaoga, akajipaka mafuta, akabadili mavazi yake; akaingia nyumbani mwa Bwana, akasali; kisha akaenda nyumbani kwake, na alipotaka wakamwandalia chakula, naye akala" (2 Samweli 12:20). Chakushangaza katika kifungu hiki ni kwamba Daudi "aliingia nyumbani mwa Bwana na kuabudu." Kwa maneno mengine, Daudi hakukubali tu kifo cha mtoto wake, lakini alipeana suala hili kwa Mungu katika ibada. Uwezo wa kuabudu na kumheshimu Mungu wakati wa majaribio au mgogoro ni maonyesho yenye nguvu ya ujasiri wetu wa kiroho katika Mungu wetu. Kufanya hivyo kunatuwezesha kukubali ukweli wa hasara yetu. Na hii ndiyo jinsi Mungu anatuachilia sisi kuendelea kuishi.
Somo linalofuata ni la ufunuo zaidi. Ni ujasiri katika ujuzi kwamba watoto ambao hufa kabla ya kufikia umri wa uwajibikaji wanaenda mbinguni. Jibu la Daudi kwa wale wanaojiuliza jinsi alivyoitikia kifo cha mtoto wake daima imekuwa chanzo kizuri cha faraja kwa wazazi waumini ambao wamepoteza watoto na watoto wadogo: "Lakini sasa amekufa nifungie nini? Je! Naweza kumrudisha tena? Mimi nitakwenda kwake lakini yeye hatanirudia mimi." (2 Samweli 12:23). Daudi alikuwa na hakika kabisa kwamba angekutana na mwanawe mbinguni. Kifungu hiki ni dalili yenye nguvu kwamba watoto wadogo ambao hufa kutoka dunia hii wataenda mbinguni.
Kuomboleza kufa kwa mtoto ni safari ya kusikitisha. Hakuna miongozo ya kuweka ili kutufundisha jinsi ya kushughulikia maombolezo yetu. Hata hivyo, washauri na wale ambao wamepata kupoteza mtoto wao wametoa ushauri muhimu:
• Jua kuwa hauko peke yako. Una Mungu. Una ndugu na dada zako katika Kristo. Una marafiki wa karibu na familia. Wategemee. Wao wako ili wakukusaidie.
• Usiweke mipaka ya muda juu ya kupona kwako. Usitarajie siku kupita bila kufikiri juu ya mtoto wako, wala usijizuie.
• Ongea kuhusu mtoto wako. Ni muhimu kwamba ushiriki hadithi ya mtoto wako na wengine.
• Jihadharishe mwenyewe na watoto wako wengine. Wao, pia, wanateseka. Wanaomboleza kumpoteza ndugu yao na kuwa na wasiwasi wa ziada wakiona wazazi wao wakiwa na huzuni.
• Jaribu kufanya maamuzi yoyote makubwa angalau kwa mwaka wa kwanza.
• Tarajia kuwa kushinda "makumbusho" baada ya kifo cha mtoto mdogo-siku ya kuzaliwa ya kwanza, Krismasi ya kwanza, nk — kuwa chungu.
Na mwisho, Wakristo ambao wamempoteza mtoto wana ahadi kuu na ya uaminifu ya Neno la Mungu: "Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita"(Ufunuo 21: 4).
English
Wazazi Wakristo wanapaswa kushughulikia kifo cha mtoto namna gani?