settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu kifo?

Jibu


Biblia huelezea kifo kama kutenganishwa: kifo cha kimwili ni kujitenga nafsi kutoka kwa mwili, na kifo cha kiroho ni kutenganisha nafsi kutoka kwa Mungu.

Kifo ni matokeo ya dhambi. "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti," Warumi 6: 23a. Dunia nzima inakabiliwa na kifo, kwa sababu wote wamefanya dhambi. "Kwa kupitia mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kifo na dhambi, na hivyo kifo kiliwafikia watu wote, kwa kuwa wote wamefanya dhambi" (Warumi 5:12). Katika Mwanzo 2:17, Bwana alimwambia Adamu kwamba adhabu ya kutotii ingekuwa kifo — "hakika utakufa." Adamu alipokosa kumtii, alipata kifo cha kiroho cha haraka, ambacho kilimfanya ajifiche "kwa Bwana Mungu kati ya miti ya bustani "(Mwanzo 3: 8). Baadaye, Adamu alipata kifo cha kimwili (Mwanzo 5: 5).

Katika msalaba, Yesu pia alipata kifo cha kimwili (Mathayo 27:50). Tofauti ni kwamba Adamu alikufa kwa sababu alikuwa mwenye dhambi, na Yesu, ambaye hakuwa amefanya dhambi, alichagua kufa kwa ajii ya ya wenye dhambi (Waebrania 2: 9). Yesu alionyesha nguvu zake juu ya kifo na dhambi kwa kufufuka kutoka kwa wafu siku ya tatu (Mathayo 28; Ufunuo 1:18). Kwa sababu ya Kristo, kifo ni adui aliyeshindwa. "Ku wapi ewe mauti kushinda kwako? U wapi, ewe mauti uchungu wako? "(1 Wakorintho 15:55; Hosea 13:14).

Kwa wale ambao hawajaokoka, kifo husababisha mwisho wa nafasi ya kukubali sadaka ya neema ya wokovu wa Mungu. "Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, lakini baada ya kufa hukumu" (Waebrania 9:27). Kwa walio okoka, kifo kinatuweka mbele ya Kristo: "Kutokuwamo katika mwili, na kukaa pamoja na Bwana" (2 Wakorintho 5: 8; Wafilipi 1:23). Kwa kweli ni ahadi ya ufufuo wa waumini kwamba mauti ya kimwili ya Mkristo inaitwa "usingizi" (1 Wakorintho 15:51, 1 Wathesalonike 5:10). Tunatarajia wakati huo ambapo "hakutakuwa na kifo tena" (Ufunuo 21: 4).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu kifo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries