settings icon
share icon
Swali

Je! Ni kipi cha maana, kifo cha Yesu au ufufuo Wake?

Jibu


Kufa na kufufuka kwa Kristo vyote ni vya maana. Kifo cha Yesu na ufufuo wake vilitimilika kando ya kingine lakini kwa umuhimu mkubwa vinahusiana. Kufa na kufufuka kwa Bwana wetu haviwezi tenganishwa, kama vile upindo na utando wa nyusi za nguo.

Msalaba wa Yesu ulitunyakulia ushindi ambao hatungeushinda sisi wenyewe. "Mungu akiisha kuzivua enzi na mamlaka, alizifanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuziburura kwa ujasiri, akizishinda katika msalaba wa Kristo" (Wakolosai 2:15). Msalabani Mungu alishinisha dhambi zetu juu ya Yesu, na akabeba adhabu tuliyostahili (Isaya 53:4-8). Katika kifo chake Yesu alichukua mwenyewe laana ambayo ililetwa na Adamu (angalia Wagalatia 3:13).

Kwa kifo cha Kristo, dhambi zilikosa uwezo wa kututawala (Warumi 6). Kwa kifo chake, Yesu aliharibu kazi ya shetani (Yohana 12:31; Waebrania 2:14; 1Yohana 3:8), alimhukumu Shetani (Yohana 16:11), na aliponda kichwa cha nyoka (Mwanzo 3:15).

Bila kifo cha dhabihu cha Kristo, bado tungalikuwa dhambini, bila msamaha, wasiokombolewa, bila wokovu, na kutopendwa. Msalaba wa Yesu ni kiungo muhimu katika wokovu wetu na kuwa mada kuu katika mahubiri ya mitume (Matendo 2:23,36; 1 Wakorintho 1:23; 2:2; Wagalatia 6:14).

Lakini habari juu ya Yesu haikuisha na kifo chake. Ufufuo wa Kristo pia ni la muhimu sana kwa ujumbe wa injili. Wokovu wetu unadumu au kuanguka kwa msingi wa ufufuo wa kimwili wa Yesu Kristo, vile Paulo anaiweka wazi katika 1 Wakorintho 15:12-19. Ikiwa Kristo hakufufuliwa kutoka kwa wafu, basi sisi wenyewe hatuna tumaini la ufufuo, mahubiri ya mitume yangekuwa bure, na waumini wote wanapaswa kuhurumiwa. Bila ufufuo bado tungali tunakaa "gizani na katika uvuli wa mauti" tukingoja jua lijomoshe (Luka 1:78-79).

Kwa sababu ya ufufuo wa Yesu, ahadi yake inabaki kuwa kweli kwetu: "kwa kuwa mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai" (Yohana 14:19). Adui wetu mkuu atashindwa (1 Wakorintho 15:26, 54-55). Ufufuo wa Yesu ni muhimu pia kwa sababu ni kupitia kwa tukio hilo Mungu alitutangaza kuwa wenye haki: Yesu "Alitolewa afe kwa ajili ya dhambi zetu, naye alifufuliwa kutoka mauti ili tuhesabiwe haki" (Warumi 4:25). Karama ya Roho Mtakatifu kutoka kwa Bwana Yesu aliyefufuka na kupaa mbinguni (Yohana 16:7).

Angalau mara tatu katika huduma Yake duniani Yesu alitabiri kuwa atakufa na afufuke tena baada ya siku tatu (Marko 8:31; 9:31; 10:34). Ikiwa Yesu hakufufuliwa toka kwa wafu, basi angekuwa Amekosea katika unabii wake-angalikuwa nabii mwingine wa uongo ambaye atapuuzwa. Jinsi ilivyo, walakini, tunaye Bwana aliye hai, mwaminifu kwa Neno Lake. Malaika katika kaburi tupu la Yesu aliweza kuelekeza katika unabii uliotimia: "Hayupo hapa, kwa kuwa amefufuka, kama vile alivyosema" (Mathayo 28:6).

Maandiko yanaambatanisha kifo na ufufuo wa Kristo, na ni lazima tudumishe ambatanisho hilo. Kuingia kwake Yesu katika kaburi vile vile ni muhimu sawa na kutoka kwake. Katika 1 Wakorintho 15:3-5, Paulo anafafanua injili kuwa kweli mbili, kwanza Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu (inathibitishwa na kuzikwa kwake) na kwamba alifufuka tena siku ya tatu (inathibitishwa na kuonekana kwake na mashahidi wengi). Ukweli huu wa injili ni "umuhimu wa kwanza" (aya 3).

Ni vigumu kutenganisha kifo cha Kristo toka kwa ufufuo Wake. Kuamini katika moja bila lingine ni kuamini katika injili potovu ambayo haiwezi okoa. Ndiposa Yesu awe alifufuka kutoka kwa wafu, lazima awe alikufa kwa kweli. Na ndiposa kifo chake kiwe na maana ya kweli kwetu, lazima awe alifufuka. Hatuwezi kuwa na moja bila lingine.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni kipi cha maana, kifo cha Yesu au ufufuo Wake?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries