Swali
Teolojia ya Kikristo ni nini?
Jibu
Neno "teolojia" linatokana na maneno mawili ya Kiyunani yenye maana ya "Mungu" na "neno." Maneno hayo yakiunganishwa, neno "teologia" linamaanisha "mafundisho ya Mungu." Teolojia ya Kikristo ni utafiti wa kile Biblia inafundisha na kile Wakristo wanaamini. Waumini wengi huchukulia teolojia ya Kikristo kama jambo linalogawanyisha, jambo ambalo linapaswa kuepukwa. Kwa kweli, teolojia ya Kikristo inapaswa kuunganisha! Neno la Mungu linafundisha ukweli na tunapaswa kuungana katika ukweli huo. Ndiyo, kuna kutofautiana na migogoro katika teolojia ya Kikristo. Ndiyo, kuna uhuru wa kutokubaliana juu ya yasiyo muhimu katika teolojia ya Kikristo. Wakati huo huo, kuna mengi ambayo yanapaswa kuunganisha Wakristo. Teolojia ya Kikristo ya msingi ya Biblia itatusaidia kuelewa Mungu vizuri, wokovu, na huduma yetu katika ulimwengu huu.
Kwa wengine, neno "wateolojia" inaleta picha za wazee wanaosoma maandiko ya kale katika vyumba visivyo na mwanga wa kutosha, huku wakisoma mambo ambayo yameondolewa kabisa kutoka kwa maisha halisi. Inaweza kuwa ni ukweli. Pili Timotheo 3: 16-17 inatuambia kwamba kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.Kuwa mtaalamu teolojia ni kuwa mmoja anayetafuta uso wa Mungu ili akutane na Muumba wa ulimwengu na Mwanawe, Yesu Kristo, na kumkubali Yeye kama Bwana wa maisha yetu, ili Yeye awe katikati ya mapenzi yetu, upendo , na hekima. Urafiki huu unaenea katika nyanja zote za maisha yetu-hutufurahisha kwa baraka zake, kutufariji wakati wa kupoteza, kutuimarisha katika udhaifu wetu, na kutushikilia hadi mwisho wa maisha yetu wakati tutamwona uso kwa uso. Maandiko ni hadithi ya Mungu, na tunapojifunza Neno Lake zaidi, tunapata kumjua Yeye vizuri.
Kuna aina mbalimbali za teolojia ya Kikristo. Kuelewa kile Biblia inasema juu ya maeneo mbalimbali ya teolojia ya Kikristo ni muhimu kwa ukuaji wa kiroho katika maisha ya Kikristo.
Teolojia sahihi / Paterolojia — kujifunza juu ya Mungu Baba.
Kristolojia — utafiti wa Mtu na kazi ya Yesu Kristo.
Neumatolojia — utafiti wa Mtu na kazi ya Roho Mtakatifu.
Bibliolojia — kujifunza Neno la Mungu.
Soterolojia — utafiti wa wokovu kupitia Yesu Kristo.
Anthropolojia ya Kikristo — utafiti wa asili ya ubinadamu.
Hamatiolojia — utafiti wa asili na madhara ya dhambi.
Umalaika — utafiti wa malaika.
Dimonolojia ya Kikristo — utafiti wa mapepo.
Eklesiolojia — kujifunza asili na utume wa kanisa.
Esikatolojia — utafiti wa nyakati za mwisho / siku za mwisho.
English
Teolojia ya Kikristo ni nini?