Swali
Je! Ni nini kipawa cha kiroho cha imani?
Jibu
Kipawa cha kiroho cha imani kinapatikana katika orodha ya vipawa vya Roho katika 1 Wakorintho 12. Mstari wa 9 inasema kwamba baadhi ya watu hupewa kipawa cha imani, lakini kipawa hakichaelezewa kwa uwazi. Waumini wote wamepewa imani ya kuokoa na Mungu kama njia pekee ya wokovu (Waefeso 2:8-9), lakini sio waumini wote wanaopewa kipawa cha kiroho cha imani. Kama vipawa vyote vya Roho Mtakatifu, kipwa cha kiroho cha imani kilitolewa kwa "manufaa ya kawaida," ambayo inamaanisha kuadilisha mwili wa Kristo (1 Wakorintho 12:7).
Kipawa cha imani kinaweza kuelezewa kama kipawa maalum ambapo Roho huwapa Wakristo ujasiri usio wa kawaida katika ahadi za Mungu, nguvu ya Mungu, na uwepo wa Mungu ili waweze kuchukua msimamo wa kishujaa kwa ajili ya baadaye ya kazi ya Mungu kanisani. Kipawa cha kiroho cha imani inaonyeshwa na mtu mwenye ujasiri thabiti na usio na shaka katika Mungu, Neno Lake, na ahadi Zake. Mifano ya watu wenye kipawa cha imani ni wale walioorodheshwa katika Waebrania sura ya 11. Sura hii, ambayo mara nyingi huitwa "ukumbi wa imani," inaelezea wale ambao imani yao ilikuwa ya ajabu, iliyowawezesha kufanya mambo ya ajabu, vitu visivyo vya kibinadamu. Hapa tunamwona Noa akitumia miaka 120 kujenga mashua kubwa wakati, hadi wakati huo, mvua haikuwepo na Ibrahimu anaamini kwamba angekuwa na mtoto wakati uwezo asili wa mke kufanya hivyo ulikuwa umeisha. Bila kipawa cha pekee cha imani kutoka kwa Mungu, mambo hayo yangekuwa hayawezekani.
Kama ilivyo na vipawa vyote vya kiroho, kipawa cha imani hutolewa kwa Wakristo wengine ambao basi huitumia kuadilisha wengine katika mwili wa Kristo. Wale walio na kipawa cha imani ni msukumo kwa waumini wenzake, wakionyesha ujasiri rahisi kwa Mungu ambao unajionyesha katika kila wanachosema na kufanya. Watu waaminifu ajabu huonyesha uungu wa unyenyekevu na kutegemea ahadi za Mungu, mara nyingi sana ili waweze kujulikana kuwa wasiogopa na wenye raghba kimya. Wao wana hakika kwamba vikwazo vyote kwa injili na madhumuni ya Mungu vitashindwa na hivyo na uhakika kwamba Mungu atapata maendeleo ya sababu yake, kwamba mara nyingi watafanya mbali zaidi katika kukuza Ufalme Wake kuliko wahubiri wengi wenye ujuzi na maarifa na walimu.
Kwa kujumlisha, Mungu huwapa Wakristo wote Imani ya kuokoa. Kipawa cha kiroho cha imani hutolewa kwa wengine, ambao wanaonyesha kiasi kikubwa cha Imani ya ajabu katika safari yao ya Kikristo na ambao, kwa imani yao, ni furaha na himizo kwa wengine.
English
Je! Ni nini kipawa cha kiroho cha imani?