settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nini kipawa cha kiroho cha kutafsiri lugha?

Jibu


Pamoja na kipawa cha kuzungumza kwa lugha ni kipawa kingine cha kiroho kilichotajwa katika 1 Wakorintho 12:10-kipawa cha kutafsiri lugha. Kipawa cha kutafsiri lugha ni uwezo wa kutafsiri lugha ya kigeni katika lugha ya wasikilizaji. Kipawa cha kutafsiri lugha ni kipawa tofauti, lakini inaonekana kuwa kilitumika pamoja na kipawa cha kuzungumza kwa lugha.

Kipawa cha lugha ilikuwa uwezo usio wa kawaida wa kuzungumza lugha ya kigeni ambayo msemaji wa lugha hajawahi kujifunza. Tunaona kipawa hiki kikitumika katika Matendo 2:4-12, kama Wayahudi huko Yerusalemu waliposikia injili ikihubiriwa katika lugha nyingi mbalimbali. Mtu mwenye kipawa cha kutafsiri lugha, basi, anaweza kuelewa kile msemaji wa lugha anasema hata ingawa hakujua lugha inayozungumzwa. Ukosefu wa ujuzi wa awali wa lugha ndio unatofautisha kipawa cha kiroho kutoka kwa kipawa cha asili cha kuwa na uwezo wa kuelewa na kuzungumza lugha mbalimbali. Mkalimani wa lugha anaweza sikia msemaji wa lugha na kisha kuwasiliana ujumbe kwa mtu yeyote yupo ambaye hawezi kuelewa lugha. Lengo lilikuwa ni kwamba wote wangeweza kuelewa na kufaidika na ukweli ulioongelewa. Kulingana na Mtume Paulo, na kwa kukubaliana na lugha zilizoelezwa katika Matendo, kipawa cha lugha kilikuwa na maana ya kuwasiliana ujumbe wa Mungu moja kwa moja kwa mtu mwingine katika lugha yake ya asili. Bila shaka, ikiwa wale waliokuwepo hawakuweza kuelewa lugha iliyozungumzwa, lugha haikuwa na maana-na hicho ndicho kilifanya wakalimani wa lugha, au watafsiri wa lugha, muhimu. Lengo lilikuwa ni kuadilishasha kanisa (1 Wakorintho 14:5, 12).

Mojawapo ya matatizo katika kanisa la Korintho ilikuwa kwamba wasemaji wa lugha walizungumza katika huduma, wakitumia kipawa chao cha lugha bila mkalimani na bila mtu aliyekuwepo anazungumza lugha hiyo. Matokeo yalikuwa kwamba msemaji wa lugha alikuwa anaamuru makini, lakini maneno yake hayakuwa na maana, kwa kuwa hakuna mtu angeweza kumelewa. Paulo alishauri kwa nguvu sana kwamba matumizi yote ya lugha katika kanisa sharti itafsiriwe: "Katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, Zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha" (1 Wakorintho 14:19). Hapakuwa na manufaa kwa wafuasi wengine wa kanisa katika kusikia kitu ambacho hawangeweza kuelewa. Kutumia kipawa cha lugha kanisani, kwa ajili tu ya kuonyesha kila mtu kwamba ulikuwa na kipawa, ulikuwa majivuno na usio na manufaa. Paulo aliwaambia Wakorintho kwamba, ikiwa wasemaji wa lugha wawili au watatu walitaka kuzungumza katika mkutano, basi, mkalimani wa lugha aliyetunukiwa kiroho lazima pia akuwepo. Kwa kweli, "lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu" (1 Wakorintho 14:28).

Hali ya asili ya kipawa cha lugha inaonyesha kuwa kipawa cha kutafsiri wa lugha pia ilikuwa hali ya asili. Ikiwa kipawa cha kuzungumza kwa lugha kilikuwa kinafanya kazi katika kanisa leo, kingefanyika kulingana na Maandiko. Ingekuwa lugha halisi na yenye akili (1 Wakorintho 14:10). Ingekuwa kwa lengo la kuwasiliana Neno la Mungu kwa mtu wa lugha nyingine (Matendo 2:6-12), na ingefanyika "kwa njia inayofaa na ya utaratibu" (1 Wakorintho 14:40), "kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa Amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu"(1 Wakorintho 14:33).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nini kipawa cha kiroho cha kutafsiri lugha?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries