Swali
Je! Ni nini kipawa cha kiroho cha roho wa kutambua?
Jibu
Kipawa cha roho wa kutambua, au "kutofautisha" roho, ni mojawapo ya vipawa vya Roho Mtakatifu vilivyoelezwa katika 1 Wakorintho 12: 4-11. Kama vipawa hivi vyote, kipawa cha roho wa kutambua hutolewa na Roho Mtakatifu, ambaye hugawa vipawa hivi kwa waumini kwa ajili ya huduma katika mwili wa Kristo. Kila muumini ana uwezo wa kiroho kwa huduma maalum, lakini hakuna nafasi ya kujichagulia mwenyewe. Roho hugawa vipawa vya kiroho kulingana na mamlaka ya Mungu na kwa mujibu wa mpango Wake wa kuadilisha mwili wa Kristo. Anatoa vipawa Vyake "kama vile anavyoamua" (1 Wakorintho 12:11).
Wakati tunakuja kwa kipawa cha roho wa kutambua, kila muumini aliyeokoka ana kiasi fulani cha ufahamu, ambao huongezeka vile muumini anavyokomaa katika Roho. Katika Waebrania 5:13-14 tunasoma kwamba muumini ambaye amekomaa zaidi ya kutumia maziwa ya Neno kama mtoto katika Kristo anaweza kutambua yote mema na mabaya. Muumini anayekomaa anapewa nguvu na Roho wa Mungu kupitia Maandiko ili kujua tofauti kati ya mema na mabaya, na, zaidi ya hayo, anaweza pia kutofautisha kati ya kile kizuri na kile kilicho bora. Kwa maneno mengine, muumini yeyote aliyeokoka ambaye anachagua kuzingatia Neno la Mungu ni mtambuzi wa kiroho.
Kuna waumini fulani, hata hivyo, ambao wana kipawa cha kiroho cha roho wa kutambua-yaani, uwezo uliotolewa na Mungu kutofautisha kati ya ukweli wa Neno na mafundisho ya udanganyifu yanayoenezwa na pepo. Sisi sote tunahimizwa kuwa watambuzi wa kiroho (Matendo 17:11; 1 Yohana 4:1), lakini wengine katika mwili wa Kristo wamepewa uwezo wa pekee wa kutambua mafundisho "ughushi" ambayo yamesumbua kanisa tangu karne ya kwanza . Utambuzi huu hauhusishi mafumbo, mafunuo zaidi ya kibiblia au sauti kutoka kwa Mungu. Badala yake, watambuzi wa kiroho wana ufahamu sana na Neno la Mungu kwamba wao wanatambua mara moja lililo kinyume na Neno. Hawapokei ujumbe maalum kutoka kwa Mungu; wanatumia Neno la Mungu "kujaribu roho" ili kuona ambayo inaambatana na Mungu na ambayo ni kinyume Naye. Watambuzi wa kiroho ni wa bidii "kugawanywa kwa haki" (2 Timotheo 2:15) Neno la Mungu.
Kuna tofauti ya vipawa katika kuimarisha mwili wa Kristo, lakini tofauti hizo zina maana ya kuadilisha na kujenga mwili huo kwa ujumla (Waefeso 4:12). Na mafanikio ya mwili huo yanategemea sehemu zote za mwili kutekeleza kazi zao kwa uaminifu vile Mungu ameziwezesha. Hakuna kipawa cha kiroho kinapaswa kutumiwa kukandamiza wengine au kudai yenyewe upako wa pekee kutoka kwa Mungu. Badala yake, upendo wa Mungu unaongoza matumizi yetu ya vipawa vya kiroho kuadilisha kila mmoja katika Bwana.
English
Je! Ni nini kipawa cha kiroho cha roho wa kutambua?