settings icon
share icon
Swali

Ni ni maana ya Kipindi cha miaka elfu moja kabla Yesu arudi?

Jibu


Kipindi cha miaka elfu moja kabla Yesu arudi ni mtazamo wa kurudi kwa Yesu mara ya pili ambao utatokea kabla ya ufalme wa miaka elfu moja, na huo ufalme ni utawala wa Kristo kwa miaka 1000 duniani. Ili uelewe na kufasiri ukurasa wa Bibilia ambao wahuzisha matukio ya nyakati za mwisho, kuna mambo mawili ambayo lazima yaieleweke: Mtindo mwafaka wa kufasiri bibilia na tafauti ilioko kati ya Israeli (Wayahudi) na kanisa (Mwili wa Wakristo katika Yesu Kristo).

Kwanza, mfumo mzuri wa kufasiri bibilia wahitaji hiyo bibilia ifasiriwe kwa njia inayoambatana na mazingara/muktadha. Hii inamaanisha kwamba ukurasa lazima ufasiriwe namna inayoambatana na wasikilizaji ambao umeandikiwa, wale umeandikwa kuhusu, ule ameuandika na kadhalika. Wakati mwingine ni vigumu kujua mwandishi, wasikilizaji, na historia ya masingara wa kila ukurasa ambao mtu anafasiri. Mandhari ya kihistoria na kitamaduni kila mara zaonyesha maana kamili ya ukurasa. Pia ni muimu kukumbuka kwamba maandiko yanafasiri maandiko. Hiyo ni kuwa, kila mara ukurasa utakua na mada ambayo pia imezungumziwa kwingine katika bibilia. Ni muhimu kufasiri hizi kurasa zote kuambatana na zingine.

Mwisho na la maana sana, ukurasa lazima uchukuliwe kila mara lazima uchukuliwa njia inayofaa, ya kawaida, ya wazi, maana ya neno kwa neno isipokuwa kama mazingara ya ukurasa yaonyesha kuwa ni mafumbo katika hali yake. Fasiri ya neno kwa neno haiondoi uwezekano wa thamatali ya usemi. Huwa inamtia moyo anayefasiri kusoma lugha ya thamatali kwa maana ya ukurasa ikiwa inaambatana na masingira ya ujumbe. Ni muimu kamwe kutotafuta maana ya “ndani sana au ya kiroho” mbali na ile imependekezwa. Kufanya ukuraza uwe wa kiroho ni jambo la hatari sana, kwa sababu linasongesha msingi wa fasiri kamili kutoka kwa maandiko hadi kwa mawazo ya msomaji. Kwa hivyo, hakutakuwa na kiwango cha kadri ya kufasiri; badala, bibilia itakua mada kwa mtu binafsi jinsi inavyo leta maana ya picha. 2 Petero 1:20-21 yatukumbusha kwamba, “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”

Kwa kuutumia msimamo huu wa fasiri ya kibibilia, lazima ionekane kwamba Israeli (uzao wa Abrahamu uanoonekana) na kanisa (waumini wote wa agano jipya) ni makundi mawili tofauti. Ni muimu kutambua kwamba Israeli na kanisa ni tafauti kwa sababu, ikiwa litaeleweka vipaya, maandiko yatafasiriwa vipaya. Hasa fasiri zinazohatarika ni zile kurasa zinahusu ahadi walizoahidiwa Waisraeli (zote zilizotimizwa na zenye hazikutimizwa). Ahadi kama hizo zizitumike kwa kanisa. Kumbuka masingira ya ujumbe yataamua ni nani anaandikiwa na itaelekeza kwa fasiri inayofaa.

Kwa wazo hili katika akili, tunaweza kuangalia kurasa tofauti za maandiko ambazo zinatoa mitazamo ya miaka elfu moja kabla Yesu arudi ulimwenguni. Mwanzo 12:1-3: “Bwana akamwambia Abramu, toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe Baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.”’

Mungu aliahidi Abrahamu mambo matatu: atakuwa na uzao, taifa hili litarithi nchi na Baraka kwa watu wote kupitia kwa uzao wa Abrahamu (Wayahudi). Katika Mwanzo 15:9-17 Mungu anathibitisha ahadi zake kwa Abrahamu. Na kwa kweli hii ilifanyika, Mungu anajitwika jukumu kwa ahadi hii. Hiyo ni kusema kwamba, hakukuwa na kitu chochote Abrahamu angefanya au angekosa kufanya ili ahadi ifutiliwe mbali ambayo Mungu alikuwa ameweka. Pia katika ukurasa huu, mipaka imewekwa kwa nchi ambayo Wayahudi wataridhi. Kwa orodha kamili ya mipaka angalia Kumbukumbu La Torati 20:42-44.

Katika 2 Samweli 7:10-17, tunaona Mungu akimwahidi mfalme Daudi. Hapa, Mungu anamwahidi Daudi kwamba atakua na uzao, na kutoka kwa uzao huo Mungu atanzisha ufalme wa milele. Hii inataja utawala wa Kristo wakati wa karne moja na milele. Ni muimu kuweka hili katika akili kwamba ahadi hizi lazima zitimizwe na bado hazijatokea. Wengine wataamini kuwa utawala wa Suleimani ulikuwa utimizo wa unabii, lakini kuna kasoro na hiyo. Ngome ambazo Suleimani alitawala haitwaliwi na Waisraeli hii leo, na hata Suleimani hatawali Israeli hii leo. Kumbuka kwamba Mungu alimwahidi Abrahamu kwamba uzao wake watairidhi nchi milele yote. Pia, 2 Samweli 7 yasema kwamba Mungu atamweka mfalme ambaye atatawala milele yote. Suleimani hatakuwa hitimizo kwa ahadi aliyoahidiwa Daudi. Kwa hivyo, hii ni ahadi ambayo bado haijatimizwa.

Sasa, haya yote yakiwa kwa akili, chunguza chenye kimenakiliwa katika Ufunuo 20:1-7. Miaka elfu moja ambayo imerudiwa rudiwa katika ukurasa huu inaambatana na miaka 1000 ya utawala wa Kristo duniani. Kumbuka kwamba ahadi alizoahidiwa Daudi kuhusu mfalme ambazo hazijatimizwa bado hazijatokea. Waaminio miaka elfu moja kabla Yesu arudi wanauona ukurasa huu ukielezea utimizo wa ahadi hiyo Kristo akiwa enzini. Mungu aliweka agano lisilo na masharti kwa Abrahamu na Daudi. Kati ya ahadi hizi mbili hakuna hata moja imetimia. Ule utawala wa Kristo ndio njia pekee ahadi inaweza timizwa vile Mungu aliahdi itakuwa.

Kwa kutumia fasiri ya neno kwa neno kwa maandiko yaipua vipande vya vitendawili ambao vimewekwa pamoja. Unabii wote wa Agano La Kale kuhusu kuja kwa Yesu mara ya kwanza ulitimia. Kwa hivyo lazima tutarajie unabii kuhusu kuja kwa Yesu mara ya pili pia utimizwe vile vile. Wanaoshikilia utawala wa miaka elfu moja kabla Yesu arudi ndio mfumo uanokubaliana na fasiri ya neno kwa neno ya agano la Mungu na unabii wa nyakati za mwisho.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni ni maana ya Kipindi cha miaka elfu moja kabla Yesu arudi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries