Kitabu cha 1 Petro
Mwandishi: 1 Petro 1: 1 inatambua mwandishi wa kitabu cha 1 Petro kama mtume Petro.Tarehe ya kuandikwa: kitabu cha 1 Petro huenda kiliandikwa kati ya 60 na 65 BK.
Kusudi la Kuandika: 1 Petro ni barua kutoka kwa Petro kwa Waumini ambao walikuwa wametawanyika katika ulimwengu wa kale na walikuwa chini ya mateso makali. Ikiwa kuna aliyeelewa mateso, ni Petro. Yeye alipigwa, kutishiwa, kuadhibiwa na kufungwa jela kwa kuhubiri neno la Mungu. Yeye alijua nini ilichukua kuvumilia bila ukali/uchungu, bila ya kupoteza matumaini na katika imani kubwa akaishi maisha ya utiifu na ya ushindi. Elimu hii ya matumaini yaliyo hai katika Yesu ilikuwa ndio ujumbe na mfano wa Kristo ulipaswa kufuatwa.
Mistari muhimu: 1 Petro 1: 3, "Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye Kwa rehema yake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu!."
1 Petro 2: 9, "Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu."
1 Petro 2:24, "Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki, na kwa kupigwa kwake mliponywa."
1 Petro 5: 8-9, "Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani."
Muhtasari kwa kifupi: Ingawa wakati huu wa mateso ulikuwa wa kukatiza tamaa, lakini Petro anaonyesha kwamba kweli ulikuwa wakati wa kufurahi. Anasema kuwa anahesabu kuwa faida kuteseka kwa ajili ya Kristo, kama Mwokozi wao aliteseka kwa ajili yao. Hii barua inarejelea mazoefu binafsi ya Petro na Yesu na mahubiri yake kutoka katika kitabu cha Matendo. Petro anathibitisha Shetani kama adui mkubwa wa kila Mkristo lakini uhakika wa kurudi kwa Kristo unatoa motisha ya matumaini.
Mashirikisho: Ufahamu wa Petro wa sheria ya Agano la Kale na manabii ulimwezesha kueleza vifungu mbalimbali vya Agano la kale katika mwanga wa maisha na kazi ya Masihi, Yesu Kristo. Katika 1 Petro 1:16, alinukuu Mambo ya Walawi 11:44: "Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu." Lakini anautanguliza kwa kueleza kwamba utakatifu haupatikani kwa kushika sheria, bali kwa neema iliyotawazwa kwa wote wanaoamini katika Kristo (mst. 13). Zaidi ya hayo, Petro anaeleza marejeleo ya "jiwe la msingi" katika Isaya 28:16 na Zaburi 118: 22 kama Kristo, ambaye alikataliwa na Wayahudi kwa kuasi na kutoamini. Marejeleo ya ziada ya Agano la Kale ni pamoja na Kristo asiye na dhambi (1 Petro 2:22 / Isaya 53: 9) na maonyo madogo kwa kuishi maisha matakatifu kwa uwezo wa Mungu ambayo unazalisha baraka (1 Petro 3:10:12, Zaburi 34: 12-16; 1 Petro 5: 5; Mithali 3:34).
Vitendo Tekelezi: Uhakika wa uzima wa milele umetolewa kwa Wakristo wote. Njia moja ya kujitambulisha na Kristo ni kushiriki katika mateso yake. Kwetu itakuwa kuvumilia matusi na fedheha kutoka kwa wale ambao wanatuita "watu wanaojifanya kuwa watakatifu" au "kujifanya kuwa bora kimaadili kuliko wengine." Hii ni kidogo sana ikilinganishwa na kile Kristo aliteseka kwa ajili yetu msalabani. Simama kwa kile unajua na kuamini ni haki na kufurahi wakati ulimwengu na Shetani wanalenga kukuumiza.
English
Kitabu cha 1 Petro