settings icon
share icon

Kitabu cha 2 Samweli

Mwandishi: Kitabu cha 2 Samweli hakimtaji mwandishi wake. Hawezi kuwa ni nabii Samweli, kwa vile alikufa katika 1 Samweli. Waandishi ambao huenda waliandika ni pamoja na Nathani na Gadi (tazama 1 Mambo ya Nyakati 29:29).

Tarehe ya kuandikwa: Kiasili, vitabu vya Samweli ya 1 na 2 vilikuwa kitabu kimoja. Watafsiri wakongwe walivitenganisha, nasi tumeweka utengano huo tangu jadi. Matukio ya 1 Samweli yanadumu takriban miaka 100, kutoka c. 1100 KK hadi c. 1000 KK. Matukio ya 2 Samweli yanadumu kipindi kingine cha miaka 40. Tarehe ya kuandika, basi, pengine huenda ikawa baada ya 960 kk

Kusudi la Kuandika: 2 Samweli ni rekodi ya utawala wa Mfalme Daudi. Kitabu hiki kinaweka agano lake na Daudi katika mazingira yake ya kihistoria.

Mistari muhimu: "Na nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitafanywa imara milele "(2 Samweli 7:16). "Mfalme akajifunika uso; na mfalme akalia kwa sauti kuu, Mwanangu Absalomu, Absalomu, mwanangu, mwanangu!" (2 Samweli 19: 4).

"" akasema, Bwana ndiye jabali langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu,naam, wangu; Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na makimbilio yangu; mwokozo wangu, waniokoa na jeuri. Nitamwita Bwana asitahiliye kusifiwa; hivyo nitaokoka na adui zangu"(2 Samweli 22: 2-4).

Muhtasari kwa kifupi: kitabu cha 2 Samweli kinaweza kugawanywa katika sehemu kuu mbili- ushindi wa Daudi(sura 1-10) na matatizo ya Daudi (sura 11-20). Sehemu ya mwisho ya kitabu (sura 21-24) ni wendo usio na kiambatisho ambayo ina maelezo zaidi ya utawala wa Daudi.

Kitabu kinaanza na Daudi kupokea habari za kifo cha Sauli na wanawe. Anatangaza wakati wa maombolezo. Muda mfupi baadaye, Daudi anatawazwa kuwa mfalme wa Yuda, wakati Ishboshethi, mmoja wa wana wa Sauli wanaoishi, anatawazwa kuwa mfalme wa Israeli (sura ya 2). Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinafuata, lakini Ishboshethi anauawa, na Waisraeli wanamuuliza Daudi kuwatawala pia(sura 4-5).

Daudi anaamisha mji mkuu wa nchi kutoka Hebroni hadi Yerusalemu na baadaye kuamisha sanduku la Agano (sura 5-6). Mpango wa Daudi wa kujenga hekalu katika Yerusalemu unakataliwa na Mungu, ambaye kisha anamuahidi Daudi mambo yafuatayo: 1) Daudi atakuwa na mwana ambaye atatawala baada yake; 2) Mwana wa Daudi atajenga hekalu; 3) Kiti cha enzi kinachotawaliwa na ukoo wa Daudi kitakuwa imara milele; na 4) Mungu kamwe hataondoa huruma yake kutoka kwa nyumba ya Daudi (2 Samweli 7: 4-16).

Daudi anaongoza Israeli kwa ushindi juu ya mataifa adui ambayo yaliwazunguka . Pia anaonyesha wema kwa familia ya Yonathani kwa kumchukua ndani Mefiboshethi, mwana mlemavu wa Yonathani (sura 8-10).

Kisha Daudi anaanguka. Yeye anamtamani mwanamke mrembo aitwaye Bathsheba, anazini naye, na kisha anapanga mauaji ya mumewe(sura ya 11). Wakati Nathanieli nabii anamkabili Daudi na dhambi zake, Daudi anakiri, na Mungu kwa neema anamsamehe. Hata hivyo, Bwana anamwambia Daudi kwamba shida itatokana kwa nyumba yake mwenyewe.

Shida inakuja wakati mwana mzaliwa wa kwanza wa Daudi, Amnoni, anambaka dadake wa kambo, Tamari. Katika kulipiza kisasi, ndugu wa Tamari Absalomu anamuua Amnoni. Absalomu kisha anakimbia Yerusalemu badala ya kukabili hasira ya baba yake. Baadaye, Absalomu anaongoza uasi dhidi ya Daudi, na baadhi ya washirika wa zamani wa Daudi wajiunga na uasi (sura 15-16). Daudi analazimishwa kutoka Yerusalemu, na Absalomu anajiweka mwenyewe kama mfalme kwa muda mfupi. Mnyang’anyi anapinduliwa, hata hivyo, na- kinyume na matakwa ya Daudi - anauawa. Daudi anaomboleza kifo cha mwanaye.

Hisia za jumla za mapigo ya mara kwa mara ambayo ni makumbusho ya utawala wa Daudi. Watu wa Israeli wanatishia kujigawanya kutoka Yuda, na Daudi lazima akandamize uasi mwingine (sura ya 20).

kiambatisho cha kitabu kinajumuhisha taarifa kuhusu njaa ya miaka mitatu katika nchi (sura ya 21), wimbo wa Daudi (sura ya 22), rekodi ya mashujaa jasiri werevu zaidi wa Daudi (sura ya 23), na hesabu ya dhambi za Daudi na mapigo yaliyofuata (sura ya 24).

Ishara: Bwana Yesu Kristo anaonekana hasa katika sehemu mbili za 2 Samweli. Kwanza, Agano na Daudi kama ilivyoainishwa katika 2 Samweli 7:16: "Na nyumba yako na ufalme wako vitathibitishwa milele mbele yako; nacho kiti chako kitafanywa imara milele " na inarudiwa katika Luka 1: 3-33 katika maneno ya malaika ambaye alionekania Maria kutangaza kuzaliwa kwa Yesu kwake:" Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake, naye atatawala juu ya nyumba ya Yakobo milele, ufalme wake hautakuwa na mwisho "Kristo ni utimilifu wa Agano la Daudi,. Yeye ni Mwana wa Mungu katika ukoo wa Daudi ambaye atatawala milele.

Pili, Yesu anaonekana katika wimbo wa Daudi mwishoni mwa maisha yake (2 Samweli 22: 2-51). Anaimba juu ya mwamba wake, ngome na mkombozi, kimbilio na mkombozi wake. Yesu ni mwamba wetu (1 Wakorintho 10: 4; 1 Petro 2: 7-9), Mkombozi wa Israeli (Warumi 11: 25-27), ngome ambaye kwake " tumekimbilia kuokolewa kwa kushikilia imara tumaini lililowekwa mbele yetu "(Waebrania 6:18 KJV), na Mwokozi wa kipee (Luka 2:11; 2 Timotheo 1:10).

Vitendo Tekelezi: Mtu yeyote anaweza kuanguka. Hata mtu kama Daudi, ambaye hakika alitamani kumfuata Mungu na ambaye alikuwa amebarikiwa sana na Mungu, aliathirika kwa urahisi na majaribu. Dhambi ya Daudi na Bathsheba inapaswa kuwa onyo kwetu zote ili tulinde nyoyo zetu, macho yetu na akili zetu. Kiburi juu ya ukomavu wetu wa kiroho na uwezo wetu wa kuhimili majaribu kwa nguvu zetu wenyewe ndio hatua ya kwanza ya kuanguka (1 Wakorintho 10:12).

Mungu ni mwenye neema kusamehe hata dhambi za kuchukiza zaidi wakati tunatubu kwa kweli. Hata hivyo, kuponya kidonda kilichosababishwa na dhambi kamwe hakifuti kovu. Dhambi zina madhara ya kawaida, na hata baada ya kusamehewa, Daudi alivuna yale aliyokuwa amepanda. Mwana wake kutoka kwa uhusiano haramu na mke wa mtu mwingine alichukuliwa kutoka kwake (2 Samweli 12: 14-24) na Daudi aliona taabu ya kukatika kwa uhusiano wake wa upendo na Baba yake wa mbinguni (Zaburi 32 na 51). Ni vizuri zaidi kiasi gani kuepuka dhambi kwanza, badala ya kutafuta msamaha baadaye!

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha 2 Samweli
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries