Kitabu cha 2 Wakorintho
Mwandishi: 2 Wakorintho 1: 1 inatambua mwandishi wa kitabu cha 2 Wakorintho kama mtume Paulo, labda pamoja na Timotheo.Tarehe ya kuandikwa: kitabu cha 2 Wakorintho huenda kiliandikwa mnamo 55-57 BK.
Kusudi la Kuandika: Kanisa katika Korintho ilianza 52 BK wakati Paulo alitembelea huko katika safari yake ya pili ya umishonari. Ilikuwa wakati huo alipokaa mwaka mmoja na nusu, mara ya kwanza yeye aliruhusiwa kukaa katika sehemu moja kwa muda mrefu kama alivyotaka. Rekodi ya ziara hii na uanzishaji wa kanisa inapatikana katika Matendo 18: 1-18.
Katika barua yake ya pili kwa Wakorintho, Paulo anaonyesha kupata nafuu na furaha yake kwamba Wakorintho walipokea barua yake "kali" (sasa iliopotea) kwa msisimko. Barua hiyo ilishughulikia masuala ambayo yalikuwa yanatawanya kanisa, kimsingi kuwasili kwa mitume wa uongo (2 Wakorintho 11:13) ambao walikuwa wanashambulia mwenendo wa Paulo, kupanda utesi/kutopatana miongoni mwa waumini, na kufundisha mafundisho ya uongo. Wanaonekana walikuwa wamehoji ukweli wake (2 Wakorintho 1: 15-17), uwezo wake wa kuzungumza (2 Wakorintho 10:10; 11: 6), na kutokuwa na nia ya kukubali msaada kutoka kwa kanisa la Korintho (2 Wakorintho 11: 7- 9; 12:13). Kulikuwa pia na baadhi ya watu ambao walikuwa hawajatubu tabia zao za usherati (2 Wakorintho 12: 20-21).
Paulo alifurahi sana kujifunza kutoka kwa Tito kwamba wengi wa Wakorintho walitubu uasi wao dhidi ya Paulo (2 Wakorintho 2: 12-13; 7: 5-9). Mtume anawahimiza kwa hili katika usemi wa upendo wake wa kweli (2 Wakorintho 7: 3-16). Paulo pia alitaka kuthibitisha utume wake, kwa kuwa baadhi katika kanisa pengine walikuwa na wasiwasi kuhusu mamlaka yake (2 Wakorintho 13: 3).
Kwa msisimko, Paulo alipata Wakorintho walipokea vizuri barua yake "kali". Mtume anawatia moyo kwa hili katika usemi wa upendo wa kweli wa Paulo (2 Wakorintho 7: 3-16). Paulo pia alitaka kuthibitisha utume wake, kwa kuwa baadhi katika kanisa pengine walikuwa na wasiwasi kuhusu mamlaka yake (2 Wakorintho 13: 3).
Mistari muhimu: 2 Wakorintho 3: 5: "Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu"
2 Wakorintho 3:18: "Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho."
2 Wakorintho 5:17: "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya!"
2 Wakorintho 5:21: "Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye."
2 Wakorintho 10: 5: "tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo"
2 Wakorintho 13: 4: "Maana, alisulubiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; lakini tutaishi pamoja naye kwa uweza wa Mungu ulio kwenu."
Muhtasari kwa kifupi: Baada ya kusalimia waumini katika kanisa la Korintho na kuwaeleza kwa nini hakuwa amewatembelea kama ilivyopangwa hapo awali (mst 1:3-2: 2), Paulo anaeleza asili ya huduma yake. Ushindi kwa njia ya Kristo na usafi mbele ya Mungu ulikuwa vigezo vya huduma yake kwa makanisa (2: 14-17). Yeye analinganisha huduma tukufu ya haki ya Kristo na "huduma ya hukumu" ambayo ni Sheria (mst 3: 9) na kutangaza imani yake katika uhalali wa huduma yake licha ya mateso makali (4: 8-18) . Sura ya 5 inadokekeza msingi wa imani ya kikristo -asili mpya (mst. 17) na kubadilishana dhambi zetu kwa haki ya Kristo (mst. 21).
Sura ya 6 na 7 unapata Paulo akijitetea mwenyewe na huduma yake, akihakikishia Wakorintho bado tena mapenzi yake ya dhati kwa ajili yao na kuwahimiza wakutubu na kuishi maisha matakatifu. Katika sura ya 8 na 9, Paulo anawahimiza waumini wa Korintho kufuata mifano ya ndugu huko Makedonia na kupanua ukarimu kwa mitume wenye mahitaji. Yeye anawafundisha kanuni na malipo ya kutoa kwa neema.
Paulo anamaliza waraka wake kwa kurudia kuwaambia mamlaka yake miongoni mwao (sura ya 10) na kujali kwa uaminifu wao kwake katika upinzani mkali kutoka kwa mitume wa uongo. Anajiita "mjinga" kwa ajili ya kutotaka kujivunia sifa zake na mateso yake kwa ajili ya Kristo (sura ya 11). Anamaliza barua yake kwa kueleza maono ya mbinguni aliyoruhusiwa kuona na "mwiba katika mwili" aliopewa na Mungu ili kuhakikisha unyenyekevu wake (sura ya 12). Sura ya mwisho ina mawaidha yake kwa Wakorintho kujichunguza wenyewe ili kuona kama yale wanakiri ni ukweli, na kumalizia na baraka ya upendo na amani.
Mashirikisho: Katika nyaraka zake, Paulo mara nyingi anarejelea sheria ya Musa, akiilinganisha na ukuu wa injili ya Yesu Kristo na wokovu kwa neema. Katika 2 Wakorintho 3: 4-11, Paulo anatofautiana na sheria ya Agano la Kale na agano jipya la neema, akitaja sheria kama ambayo "inaua" ilhali Roho hutoa uzima. sheria ni "huduma ya mauti, iliyoandikwa na kuchongwa juu ya jiwe" (mst 7; Kutoka 24:12) kwa sababu huleta tu maarifa ya dhambi na laana zake. Utukufu ambao sheria ni kwamba huonyesha utukufu wa Mungu, lakini huduma ya Roho ni tukufu zaidi kuliko huduma ya sheria, kwa sababu inaonyesha huruma yake, neema na upendo katika kutoa Kristo kama utimilifu wa sheria.
Vitendo Tekelezi: Hii barua ni historia ya maisha zaidi na dogo kimafundisho ya nyaraka za Paulo. Inatuambia zaidi kuhusu Paulo kama mtu na kama mtume kuliko yoyote ya zingine. Kwa kuwa hilo limesemwa, kuna mambo machache tunaweza kuchukua kutoka kwa barua hii na kutekeleza katika maisha yetu ya siku hizi. Jambo la kwanza ni utumishi/usimamizi, si tu wa fedha, lakini wa muda pia. Watu wa Makedonia si tu walitoa kwa ukarimu, bali "walijitoa wenyewe kwanza kwa Bwana na kisha kwetu katika kutunza na mapenzi ya Mungu" (2 Wakorintho 8: 5). Kwa njia hiyo hiyo, tunapaswa kutoa si tu vyote tulivyo navyo kwa Bwana, ila vyote vile tulivyo. Yeye kwa kweli haitaji pesa zetu. Yeye ni mwenye kudura! Yeye anataka moyo, ile ambayo inatamani kutumikia na kufurahisha na kupenda. Utumishi na kutoa kwa Mungu ni zaidi kuliko fedha. Ndiyo, Mungu anatuhitaji kutoa fungu la kumi la mapato yetu, na ameahidi kutubariki tunapomtolea. Ingawa kuna zaidi. Mungu anataka asili mia kwa mia (100%). Anatutaka kumpa vyetu vyote. Kila kitu tulicho. Tunapaswa kutumia maisha yetu kuishi kumtumikia Baba yetu. Sisi lazima si tu kumpa Mungu kutoka kwa malipo yetu, lakini maisha yetu hasa yanapaswa kumwangazia yeye. Tunapaswa kujitoa wenyewe kwanza kwa Bwana, kisha kwa kanisa na kazi ya huduma ya Yesu Kristo.
English
Kitabu cha 2 Wakorintho