settings icon
share icon

Kitabu cha 2 Yohana

Mwandishi: Kitabu cha 2 Yohana hakimtaji moja kwa moja mwandishi wake. Utamaduni kutoka siku za mwanzo za kanisa unasema kwamba mtunzi alikuwa mtume Yohana. Kumekuwa na kudhania kwa miaka kwamba mtume mwingine wa Kristo aitwaye Yohana huenda akawajibika kwa barua hii. Hata hivyo, ushahidi wote unaonyesha mwandishi kama Yohana mwanafunzi mpendwa ambaye pia aliandika Injili ya Yohana.

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha 2 Yohana huenda kiliandikwa karibu wakati sawa na wa barua zingine za Yohana, Yohana ya 1 na 3, pengine kati ya 85-95 BK.

Kusudi la Kuandika: Kitabu cha 2 Yohana ni ombi la ghafla kwamba wasomaji wa barua ya Yohana wanapaswa kuonyesha upendo wao kwa Mungu na mwana wake Yesu kwa kutii amri kupendana na kuishi maisha yao kwa kutii maandiko. Kitabu cha 2 Yohana pia ni onyo kali kuwa mwangalifu kwa wadanganyifu ambao walikuwa wakisema kwamba Kristo hakufufuka katika mwili.

Mistari muhimu: 2 Yohana 6: "Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo."

2 John 8-9: "Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu. Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia."

Muhtasari kwa kifupi: Kitabu cha 2 Yohana kimelengwa kwa 'mwanamke mteule na watoto wake.' Hii huenda pengine alikuwa mwanamke wa cheo muhimu katika kanisa au kanuni ambayo inarejelea kanisa la mtaa na washirika wake. Katika siku zile wakati Wakristo walikuwa wanateswa mkusanyiko wa salamu kama huo ulitumika mara nyingi.

Kitabu cha 2 Yohana kwa kiasi kikubwa kinashughulikia onyo la ghafla kuhusu Wadanganyifu ambao hawakuwa wanafundisha mafundisho halisi ya Kristo na ambao walishikilia kuwa Yesu hakika hakufufuka katika mwili bali tu kiroho. Yohana anatamani kwamba waumini wa kweli wanapaswa kuwa na ufahamu wa walimu hawa wa uongo na kutokuwa na kitu chochote cha kufanya na wao.

Mashirikisho: Yohana anafafanua upendo si kama mhemuko/jazba au hisia, lakini kama kutii amri za Mungu. Yesu alirudia umuhimu wa amri, hasa "amri kuu ya kwanza," upendo kwa Mungu (Kumbukumbu 6: 5) na ya pili-kupendana (Mathayo 22: 37-40, Mambo ya Walawi 19:18). Mbali na kukomesha sheria ya Agano la Kale ya Mungu, Yesu alikuja kuitimiza kwa kutoa njia ya utimilifu wake ndani yake mwenyewe.

Vitendo Tekelezi: Ni muhimu sana kwamba tuchunguze kila kitu tunaona, tunasikia, na kusoma ambacho kinadai kuwa cha "kikristo" na maandiko. Hili haliwezi kusisitizwa kwa nguvu kwa sababu moja ya silaha kuu ya Shetani ni udanganyifu. Ni rahisi sana kuchukuliwa katika na mafundisho mapya na ya kusisimua ambayo yanaonekana kuwa na misingi katika maandiko lakini ambayo, ikiwa yatachunguzwa kwa makini, kwa kweli ni kuondoka kutoka kwa Neno la Mungu. Ikiwa kinachooneka kufanyika hakilingani kikamilifu na maandiko, basi hicho ni cha uongo na si cha Roho, na tunapaswa tusiwe na chochote cha kufanya nacho.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha 2 Yohana
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries