settings icon
share icon

Kitabu cha Amosi

Mwandishi: Amosi 1: 1 inatambua mwandishi wa Kitabu cha Amosi kama nabii Amosi.

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Amosi huenda kiliandikwa kati ya 760 na 753 kk

Kusudi la Kuandika: Amosi ni mchungaji na mwenye anaokota matunda kutoka kijiji cha Tekoa ya Yuda wakati Mungu anamwita, ingawa anakosa elimu au msingi wa kikuhani. Misheni ya Amosi ililengwa kwa jirani yake wa kaskazini, Israeli. Ujumbe wake wa hukumu inayokaribia na kushikwa mateka kwa taifa kwa sababu ya dhambi zake ulikuwa kwa kiwango kikubwa hauna umaarufu na hukutiliwa maanani, hata hivyo, kwa sababu si tangu siku za Sulemani hali imekuwa nzuri katika Israeli. Huduma ya Amosi inafanyika wakati Yeroboamu II anatawala Israeli, na Uzia anatawala Yuda.

Mistari muhimu: Amosi 2: 4, "Haya ndiyo asemayo Bwana; 'Kwa makosa matatu ya Yuda, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; Kwa sababu wameikataa sheria ya Bwana; wala hawakuzishika amri zake; na maneno yao ya uongo yamewakosesha, ambayo baba zao waliyafuata. "

Amosi 3: 7, "Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake."

Amosi 9:14, "Nami nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa, nao wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu katika mashamba, na kunywa divai yake; nao watafanyiza bustani, na kula matunda yake"

Muhtasari kwa kifupi: Amosi anaweza kuona kwamba chini ya mafanikio ya nje na nguvu za Israeli, ndani yake taifa ni haribifu kabisa. Dhambi ambazo Amosi anataadibu watu zilikuwa zimeenda mbali: kupuuza Neno la Mungu, kuabudu sanamu, ibada ya kikafiri, uchoyo, uongozi wa kupotosha na kukandamiza maskini. Amosi anaanza kwa kutangaza hukumu juu ya mataifa yote jirani, kisha juu ya taifa lake mwenyewe la Yuda, na hatimaye hukumu kali inatolewa kwa Israeli. Maono yake kutoka kwa Mungu yanatia mkazo kwa ujumbe huo: hukumu inakaribia. Kitabu kinaisha na ahadi ya Mungu kwa Amosi ya urejesho wa mabaki baadaye.

Ishara: Kitabu cha Amosi kinaisha na ahadi tukufu kwa siku zijazo. "'Nami nitawapanda katika nchi yao, wala hawatang’olewa tena watoke katika nchi yao niliyowapa, asema Bwana Mungu wako" (9:15). Hatimaye kutimiza kwa ahadi ya nchi aliyoahidiwa Ibrahimu na Mungu(Mwa 12: 7; 15: 7; 17: 8) kutatokea wakati wa utawala wa milenia wa Kristo duniani (tazama Yoeli 2: 26,27). Ufunuo 20 inaeleza miaka elfu ya utawala wa Kristo duniani, wakati wa amani na furaha chini ya utawala kamilifu wa Mwokozi mwenyewe. Wakati huo, Israeli inayoamini na Wakristo wa Mataifa watawekwa pamoja katika Kanisa na wataishi na kutawala pamoja na Kristo.

Vitendo Tekelezi: Wakati mwingine tunafikiri sisi ni "tu"! Sisi ni tu-muuzaji, mkulima au mama wa nyumbani. Amosi huenda akatazamiwa ni "tu." Yeye hakuwa nabii au kuhani au mwana wa yeyote kati yao. Yeye alikuwa tu mchungaji, mfanyabiashara mdogo katika Yuda. Nani angemsikiza? Lakini badala ya kutoa visababu, Amosi alitii na akawa sauti ya nguvu ya Mungu kwa mabadiliko.

Mungu ametumia "tu-kama" kama vile wachungaji, maseremala, wavuvi katika Biblia nzima. Chochote ulicho maishani, Mungu anaweza kukutumia. Amosi hakuwa mkuu sana. Alikuwa "tu" "tu-" mtumishi kwa Mungu. Ni vizuri kuwa " ni tu" wa Mungu.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Amosi
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries