Kitabu cha Ezra
Mwandishi: Kitabu cha Ezra hakimtaji wazi mtunzi wake. Utamaduni ni kwamba nabii Ezra aliandika kitabu cha Ezra. Inavutia kutambua kwamba mara Ezra anapoonekana kwenye mandhari katika sura ya 7, mwandishi wa Kitabu cha Ezra anabadilisha kutoka kuandika katika nafsi ya tatu hadi kwa nafsi ya kwanza. Hili pia linaweza kuchangia kuwa Ezra ndiye alikuwa mwandishi.Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Ezra huenda kiliandikwa kati ya 460 na 440 kk
Kusudi la Kuandika: Kitabu cha Ezra kimeangazi kwa matukio yanayotokea katika nchi ya Israeli wakati wa kurudi kutoka utumwa wa Babeli na miaka iliyofuata, kikichukua kipindi cha takriban karne moja, kuanzia mwaka wa 538 kk. Msisitizo katika Ezra huko katika kulijenga upya Hekalu. kitabu kina rekodi ya nasaba ya kina, hasa kwa lengo la kuanzisha madai ya ukuhani kwa upande wa ukoo wa Haruni.
Mistari muhimu: Ezra 3:11 "Wakaimbiana, wakimhimidi Bwana, na kumshukuru, wakasema, kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele. Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi Bwana, kwa sababu msingi wa nyumba ya Bwana umekwisha kuwekwa."
Ezra 7: 6, "... huyo Ezra akakwea kutoka Babeli; naye alikuwa mwandishi mwepesi katika sheria ya Musa, aliyokuwa ameitoa Bwana, Mungu wa Israeli, naye mfalme akamjalia matakwa yake yote, kama mkono wa Bwana, Mungu wake, ulivyokuwa pamoja naye. "
Muhtasari kwa kifupi: kitabu kinaweza kugawanywa kama ifuatavyo: Sura ya 1-6- Kurudi kwa mara ya Kwanza chini ya Zerubabeli, na Ujenzi wa Hekalu la Pili. Sura ya 7-10- Huduma ya Ezra. Kwa kuwa zaidi ya nusu ya karne ilipita kati ya sura ya 6 na 7, wahusika wa sehemu ya kwanza ya kitabu walikuwa wamekufa kwa wakati Ezra alianza huduma yake katika Yerusalemu. Ezra ndiye mtu mmoja ambaye ni maarufu katika vitabu vya Ezra na Nehemia. Vitabu hivi vyote vinaisha kwa maombi ya kukiri (Ezra 9; Nehemia 9) na mfululizo wa utengano wa watu kutokana na mazoea ya dhambi ambayo walikuwa wanafanya. Baadhi ya dhana ya asili ya ujumbe wa kutia moyo wa Hagai na Zekaria, ambao wametambulishwa katika masimulizi haya (Ezra 5: 1), inaweza kuonekana katika vitabu vya unabii ambavyo vina majina yao.
Kitabu cha Ezra kinashughulikia kurudi kutoka utumwani ili kujenga upya Hekalu hadi kwa amri ya Artashasta, tukio lililoshughulikiwa katika mwanzo wa kitabu cha Nehemia. Hagai alikuwa nabii mkuu katika siku za Ezra, na Zekaria alikuwa nabii katika siku za Nehemia.
Ishara: Tunaona katika Kitabu cha Ezra maendelezo ya mada ya mabaki wa kibibilia. Kila wakati maafa au hukumu inatokea, Mungu daima anaokoa mabaki wachache kwa ajili yake-Nuhu na familia yake kutokana na uharibifu wa mafuriko, Familia ya Loti kutoka Sodoma na Gomora, Manabii 7000 waliohifadhiwa katika Israeli licha ya mateso ya Ahabu na Yezebeli. Wakati Waisraeli walichukuliwa mateka katika Misri, Mungu alikomboa mabaki wake na kuwapeleka katika nchi ya ahadi. Baadhi ya watu elfu hamsini wanarudi katika nchi ya Yudea katika Ezra 2: 64-67, na bado, wanapojilinganisha na idadi yao katika nchi ya Israeli wakati wa siku zake za mafanikio chini ya Mfalme Daudi, usemi wao ni, " Tumeachwa leo kama mabaki " mandhari ya mabaki inapelekwa katika Agano Jipya ambapo Paulo anatueleza kwamba "kwa wakati huu wa sasa kuna mabaki waliochaguliwa kwa neema "(Warumi 11: 5). Ingawa watu wengi wa siku za Yesu walimkataa, walibakia watu maalumu ambao Mungu alikuwa amewatenga na kuwahifadhi katika Mwana wake, na katika agano la neema yake. Katika vizazi vyote tangu Kristo, kuna mabaki ya waaminifu ambao miguu yao ipo katika njia nyembamba inayoongoza hadi kwenye uzima wa milele (Mathayo 07:13:14). Mabaki Hawa watahifadhiwa kwa nguvu za Roho Mtakatifu ambaye amewatakaza na ambaye atawawasilisha kwa usalama katika siku ya mwisho (2 Wakorintho 1:22; Waefeso 4:30).
Vitendo Tekelezi: Kitabu cha Ezra ni kumbukumbu la matumaini na marejesho. Kwa Mkristo ambaye maisha yake yametiwa kovu na dhambi na uasi dhidi ya Mungu, kuna tumaini kubwa kwamba Mungu wetu ni wa kusamehe, Mungu ambaye hatatuacha wakati tunamtafuta katika toba na unyenyekevu (1 Yohana 1: 9 ). kurudi kwa waisraeli Yerusalemu na kujenga upya Hekalu kunarudiwa katika maisha ya kila Mkristo ambaye anarudi kutoka utumwani mwa dhambi na uasi dhidi ya Mungu na hupata ndani yake kukaribishwa kwa upendo nyumbani. Haijalishi ni kwa muda mrefu kiasi gani tumekuwa mbali, Yeye ako tayari kutusamehe na kutupokea kwa familia yake. Yeye anahitaji kutuonyesha jinsi ya kujenga upya maisha yetu na kufufua mioyo yetu, ambamo ndani yao ni hekalu la Roho Mtakatifu. Kama vile kujengwa upya kwa hekalu Yerusalemu, Mungu anakusudia kazi ya kukarabati na kujitolea kwa maisha yetu kwa huduma yake.
Upinzani wa maadui/washindani wa Mungu kwa kujengwa upya kwa hekalu unaonyesha mtindo ambao ni sawa na ule wa adui wa roho zetu. Shetani anatumia wale ambao wanaonekana kuwa katika patano na makusudi ya Mungu kutudanganya na kujaribio kuzuia mipango ya Mungu. Ezra 4: 2 inaelezea kuhusu usemi wa udanganyifu wa wale wanaodai kuabudu Kristo lakini ambao kweli nia yao ni kubomoa, wala si kujenga. Tunapaswa kuwa macho dhidi ya wadanganyifu kama hao, tuwajibu kama vile waisraeli walivyofanya, na kukataa kubumbazwa na maneno yao matamu na fani ya imani ya uongo.
English
Kitabu cha Ezra