settings icon
share icon

Kitabu cha Filemoni

Mwandishi: Mwandishi wa kitabu cha Filemoni alikuwa mtume Paulo (Filemoni 1: 1).

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Filemoni kiliandikwa mnamo 60 BK.

Kusudi la Kuandika: Barua kwa Filemoni ndiyo fupi zaidi kwa maandiko ya yote ya Paulo na inashughulikia matendo ya ya utumwa. Barua inapendekeza kwamba Paulo alikuwa gerezani wakati wa kuandika. Filemoni alikuwa mmiliki wa watumwa ambaye pia ni mwenyeji aliyekaribisha kanisa katika nyumba yake. Wakati wa huduma ya Paulo huko Efeso, Filemoni alikuwa pengine amesafiri kwenda mjini, akasikia mahubiri ya Paulo na akawa Mkristo. Mtumwa Onesimo alimwibia bwana wake, Filemoni, na kutoroka, akienda Roma na kwa Paulo. Onesimo alikuwa bado mali ya Filemoni, na Paulo aliandika kwa kulainisha njia ya kurudi kwake kwa bwana wake. Kupitia kwa ushahidi wa Paulo kwake, Onesimo alikuwa amekuwa Mkristo (Filemoni 10) na Paulo alitaka Filemoni kumkubali Onesimo kama ndugu katika Kristo na siyo tu kama mtumwa.

Mistari muhimu: Filemoni 6: "ili kwamba ushirika wa imani yako ufanye kazi yake, katika ujuzi wa kila kitu chema kilicho kwetu, katika Kristo."

Filemoni 16: " tokea sasa, si kama mtumwa, bali zaidi ya mtumwa, ndugu mpendwa; kwangu mimi sana, na kwako wewe zaidi sana, katika mwili na katika Bwana"

Filemoni 18: " Na kama amekudhulumu, au unamwia kitu, ukiandike hicho juu yangu"

Muhtasari kwa kifupi: Paulo alikuwa ameonya wamiliki wa watumwa kuwa walikuwa na wajibu kuelekea kwa watumwa wao na akaonyesha watumwa kama viumbe adilifu vyenye wajibu ambao walipaswa kumwogopa Mungu. Katika Filemoni, Paulo hakulaani utumwa, bali aliwasilisha Onesimo kama ndugu Mkristo badala ya mtumwa. Wakati mmiliki anaweza kutaja mtumwa kama ndugu, mtumwa amefikia kiwango ambacho mada rasmi ya Mtumwa haina maana. Kanisa la kwanza halikushambulia utumwa moja kwa moja lakini liliweka msingi kwa ajili ya uhusiano mpya kati ya mmiliki na mtumwa. Paulo alijaribu kupatanisha Filemoni na Onesimo kwa upendo wa Kikristo ili ukombozi huwe muhimu. Tu baada ya kufumbuliwa kwa mwanga wa injili ndipo taasisi ya utumwa itakufa.

Mashirikisho: Labda hakuna mahali popote katika Agano Jipya ambapo tofauti kati ya sheria na neema imeonyeshwa vizuri. Sheria za Kirumi na Sheria za Musa za Agano la Kale zilimpa Filemoni haki ya kumwaadhibu mfungwa aliyekimbia ambaye alirejelewa kuwa mali ya mmiliki. Lakini agano la neema kwa njia ya Bwana Yesu liliruhusu bwana na mtumwa kushiriki katika upendo kwa misingi sawa katika mwili wa Kristo.

Vitendo Tekelezi: Waajiri, viongozi wa kisiasa, watendaji wa shirika na wazazi wanaweza kufuata roho ya mafundisho ya Paulo kwa kuhudumia wafanyakazi wakristo, wafanyakazi wenza na watu wa familia kama washirika wa Mwili wa Kristo. Wakristo katika jamii ya kisasa si lazima wawaangalie wasaidizi kama madaraja ya kuwasaidia kufikia malengo yao lakini kama ndugu na dada Wakristo ambao lazima wapokee huduma za neema. Aidha, viongozi wote wa Kikristo lazima watambua kuwa Mungu anawawajibisha kwa huduma watoazo kwa wale wanaowafanyia kazi, iwapo wasaidizi ni Wakristo au la. Lazima hatimaye wajibu kwa Mungu kwa matendo yao (Wakolosai 4: 1).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Filemoni
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries