settings icon
share icon

Kitabu cha Hagai

Mwandishi: Hagai 1: 1 Inatambua mwandishi wa Kitabu cha Hagai kama Nabii Hagai.

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Hagai huenda kiliandikwa kwa takriban 520 kk

Kusudi la Kuandika: Hagai alitaka kuwapa changamoto watu wa Mungu kuhusu vipaumbele vyao. Aliwaita kwa unyenyekevu na kumtukuza Mungu kwa kujenga Hekalu licha ya upinzani kichini chini na rasmi. Hagai aliwaita wasitamaushwe kwa sababu Hekalu hili halitapambwa sana kama lile la Sulemani. Aliwasihi kugeuka kutoka uovu wa njia zao na kuamini katika nguvu kuu za Mungu. Kitabu cha Hagai ni kumbukumbu ya matatizo ya watu wa Mungu yaliyowakabili wakati huu, jinsi watu walimwamini Mungu kwa ujasiri na jinsi Mungu alivyotozelesha mahitaji yao.

Mistari muhimu: Hagai 1: 4, "Je, huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?"

Hagai 1: 5-6, "Basi sasa, Bwana wa majeshi asema hivi, zitafakarini njia zenu. Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeyr apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka."

Hagai 2: 9, "Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, 'asema Bwana wa majeshi; na katika mahali hapa niwapa amani, asema Bwana wa majeshi."

Muhtasari kwa kifupi: Je, watu wa Mungu wataangazia upya vipaumbele vyao, wawe jasiri, na kutenda kulinga na ahadi za Mungu? Mungu alitaka kuwaonya watu watilie maanani maneno yake. Si tu kwamba Mungu aliwaonya, lakini pia alitoa ahadi kupitia kwa mtumishi wake Hagai ili kuwatia moyo kumfuata. Kwa sababu watu wa Mungu walivionelea vipaumbele vyao na kushindwa kuweka Mungu katika nafasi ya kwanza katika maisha yao, Yuda ilitumwa uhamishoni Babeli. Katika kujibu maombi ya Danieli na kutimiza ahadi za Mungu, Mungu alimuagiza Koreshi, mfalme wa Uajemi awaruhusu Wayahudi waliokuwa uhamishoni kurejea Yerusalemu. Kundi cha Wayahudi walirudi katika nchi yao wakiwa na furaha kubwa, wakamweka Mungu kwanza katika maisha yao, wakamsujudia na kuanza kujenga upya hekalu la Yerusalemu bila msaada wa watu walioishi katika Palestina. Imani yao ya ujasiri ilipingwa na watu wenyeji vile vile na utawala wa Kiajemi kwa takriban miaka 15.

Ishara: Kama ilivyo kwa vitabu vingi vya manabii wadogo, Hagai kinaishia na ahadi za marejesho na baraka. Katika mstari wa mwisho, Hagai 2:23, Mungu anatumia nada bainifu ya kimasiya kumrejelea Zerubabeli, "Mtumishi wangu" (Linganisha 2 Samweli 3:18; 1 Wafalme 11:34, Isaya 42: 1-9; Ezekieli 37:24 , 25). Kupitia kwa Hagai, Mungu ameahidi kumfanya kama pete yenye muhuri, ambayo ilikuwa ni ishara ya heshima, mamlaka, na nguvu, kiasi fulani kama fimbo ya mfalme inayotumika kwa kutia muhuri nyaraka na amri. Zerubabeli, kama pete yenye muhuri wa Mungu, anawakilisha nyumba ya Daudi na mwanzo wa ukoo wa kimasihi uliokatizwa na uamisho. Zerubabeli aliimarisha tena ufalme wa watu wa Daudi ambao utaishia katika utawala wa miaka elfu wa Kristo. Zerubabeli anaonekana katika ukoo wa Kristo katika upande wa Yusufu (Math. 1:12) na upande wa Mariamu (Lk 3:27).

Vitendo Tekelezi: Kitabu cha Hagai kinazingatia sana matatizo ya kawaida watu wengi ukumbana nayo hata siku hizi. Hagai anatutaka: 1) kuchunguza vipaumbele vyetu kuona kama tunavutiwa katika raha zetu wenyewe kuliko kufanya kazi ya Mungu; 2) kukataa tabia za kushindwa tunapoingia kwa upinzani au hali za kuvunja moyo 3) kukiri makosa yetu na kutafuta kuishi maisha takatifu mbele za Mungu; 4) kutenda kwa uhodari kwa Mungu kwa sababu tuna uhakika kwamba Yeye ako nasi siku zote na anadhibiti hali zetu kikamilifu, na 5) kupumzika salama katika mikono ya Mungu tukijua kwamba Yeye atatubariki kwa wingi tunapomtumikia kwa uaminifu.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Hagai
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries