settings icon
share icon

Kitabu cha Isaya

Mwandishi: Isaya 1: 1 inatambua mwandishi wa Kitabu cha Isaya kama nabii Isaya.

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Isaya kiliandikwa kati ya 701 na 681 kk

Kusudi la Kuandika: Nabii Isaya kimsingi aliitwa kutabiri kwa ufalme wa Yuda. Yuda ilikuwa inapitia katika nyakati za uamsho na nyakati za uasi. Yuda ilitishiwa kuharibiwa na Ashuru na Misri, lakini iliokolewa kwa sababu ya huruma ya Mungu. Isaya alitangaza ujumbe wa kutubu dhambi na matarajio ya matumaini ya ukombozi wa Mungu katika siku zijazo.

Mistari muhimu: Isaya 6: 8, "Kisha nikasikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, mimi hapa, nitume mimi! '" Isaya 7:14, "Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara.Tazama bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanaume, naye atamwita jina lake Imanueli"

Isaya 9: 6, "Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. "

Isaya 14: 12-13, "Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande za mwisho za kaskazini"

Isaya 53: 5-6, "Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote, kama kondoo, tumepotea, kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote. "

Isaya 65:25, "Mbwa mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng'ombe, na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema Bwana. "

Muhtasari kwa kifupi: Kitabu cha Isaya kinaonyesha hukumu ya Mungu na wokovu. Mungu ni "Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu" (Isaya 6: 3) na kwa hivyo hawezi kuruhusu dhambi kwenda bila adhabu (Isaya 1: 2; 2: 11-20; 5:30; 34: 1-2; 42:25) . Isaya anaonyesha hukumu ya Mungu itakayokuja kama "moto ulao" (Isaya 1:31; 30:33).

Wakati huo huo, Isaya anaelewa kuwa Mungu ni Mungu wa rehema, neema, na huruma (Isaya 5:25; 11:16; 14: 1-2; 32: 2; 40: 3; 41: 14-16). Taifa la Israeli (Yuda na Israeli) ni kipofu na kiziwi kwa amri za Mungu (Isaya 6: 9-10; 42: 7). Yuda inalinganishwa na shamba la mizabibu ambalo lazima, na itakuwa, litakanyagwa (Isaya 5: 1-7). Tu kwa sababu ya huruma yake na ahadi zake kwa Israeli, Mungu hataruhusu Israeli au Yuda kuangamizwa kabisa. Ataleta marejesho, msamaha, na uponyaji (43: 2; 43: 16-19; 52: 10-12).

Zaidi kuliko kitabu kingine chochote katika Agano la Kale, Isaya anazingatia katika wokovu ambao utakuja kupitia kwa Masihi. Masihi siku moja atatawala katika haki na ukweli (Isaya 9: 7; 32: 1). Utawala wa Masihi utaleta amani na usalama kwa Israeli (Isaya 11: 6-9). Kupitia kwa Masihi, Israeli itakuwa mwanga kwa mataifa yote (Isaya 42: 6; 55: 4-5). Ufalme wa Masihi duniani (Isaya sura ya 65-66) nndio lengo ambalo kuelekea kwake Kitabu kizima cha Isaya kinaangazia. Ni wakati wa utawala wa Masihi ambapo haki ya Mungu itafunuliwa kikamilifu kwa ulimwengu.

Katika ukweli kinzani, Kitabu cha Isaya pia kinaonyesha Masihi kama mmoja ambaye atateseka. Isaya sura ya 53 inaeleza waziwazi Masihi akiteseka kwa ajili ya dhambi. Ni kupitia kwa majeraha yake uponyaji unaafikiwa. Ni kupitia kwa mateso yake maovu yetu yanafutiliwa mbali. Huu mkanganyiko dhahiri unatatuliwa katika utu wa Yesu Kristo. Katika majilio yake ya kwanza, Yesu alikuwa mtumishi wa kuteseka wa Isaya sura ya 53. Katika majilio yake ya pili, Yesu atakuwa mshindi na Mfalme mtawala, Mfalme wa amani (Isaya 9: 6).

Ishara: Kama ilivyotajwa mwanzoni, sura ya 53 ya Isaya inaelezea kuja kwa Masihi na mateso ambayo angeweza kuvumilia ili kulipia dhambi zetu. Katika uhuru wake, Mungu alipanga utaratibu wa kila utondoti wa kusulubiwa kutimiza kila unabii wa sura hii, sawasawa na unabii wote wa kimasihi wa Agano la Kale. Picha ya sura ya 53 ni kali/ya kutia machungu na ya kiunabii na ina taswira kamili ya Injili. Yesu Alidharauliwa na kukataliwa (Mst 3; Luka 13:34; Yohana 1:. 10-11)., Alipigwa na Mungu (Mst.4, Mathayo 27:46), na kudungwa kwa makosa yetu (Mst 5; Yohana 19: 34; 1 Petro 2:24). Kwa mateso yake, Yeye alilipa adhabu tuliyostahili na akawa sadaka kamilifu kwetu ya mwisho(Mst 5;. Waebrania 10:10). Ingawa Yeye hakuwa na dhambi, Mungu aliweka juu yake dhambi zetu, na tukawa wenye haki wa Mungu ndani yake (2 Wakorintho 5:21).

Vitendo Tekelezi: Kitabu cha Isaya kinatoa Mwokozi wetu kwetu kwa undani usiokatalika. Yeye ndiye njia ya pekee ya kwenda mbinguni, njia ya pekee ya kupata neema ya Mungu, Njia ya pekee, ukweli wa pekee, na uzima wa pekee (Yohana 14: 6; Matendo 4:12). Tukijua bei ambayo Kristo alitulipia, ni jinsi gani tunaweza kupuuza au kukataa "wokovu mkuu hivyo"? (Waebrania 2: 3). Tuna tu, miaka mifupi duniani ili tuje kwa Kristo na kupokea wokovu ambao Yeye tu hutoa. Hakuna nafasi ya pili baada ya kifo na milele katika jehanamu ni muda mrefu sana.

Je, unajua watu ambao wanadai kuwa waumini katika Kristo ambao wana nyuso mbili, ambao ni wanafiki? Pengine huo ndio muhtasari bora wa jinsi ambavyo Isaya alitazama taifa la Israeli. Israeli ilikuwa inaonekana ya haki, lakini ilikuwa nafiki. Katika Kitabu cha Isaya, nabii Isaya anaipa changamoto Israeli kumtii Mungu kwa mioyo yao yote, si tu kwa nje. Hitaji la Isaya lilikuwa kwamba wale ambao walisikia na kusoma maneno yake wangeshawishika kugeuke kutoka kwa uovu na kurejea kwa Mungu kupata msamaha na uponyaji.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Isaya
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries