Kitabu cha Maombolezo
Mwandishi: Kitabu cha Maombolezo hakimtaji wazi mwandishi wake. Utamaduni ni kwamba Nabii Yeremia aliandika Maombolezo. Mtazamo huu una uwezekano mkubwa sana kwa kuzingatia kuwa mwandishi alikuwa shahidi watu wa Babeli walipoharibu Yerusalemu. Yeremia anafuzu hitaji hili (2 Mambo ya Nyakati 35:25; 36: 21-22).Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Maombolezo huenda kiliandikwa kati ya 586 na 575 KK, wakati au muda mfupi baada ya kuanguka kwa Yerusalemu.
Kusudi la Kuandika: Kutokana na Yuda kuendelea kuabudu sanamu bila kutubu, Mungu aliwaruhusu Wababeli kuzingira, kuteka nyara, kuuchoma, na kuuharibu mji wa Yerusalemu. Hekalu la Sulemani, ambalo lilikuwa limesimama kwa takriban miaka 400, liliteketezwa kwa moto kabisa. Nabii Yeremia, aliyeshuhudia kwa macho yake matukio hayo, aliandika kitabu cha Maombolezo kama maombolezo kwa yaliyotokea kwa Yuda na Yerusalemu.
Mistari muhimu: Maombolezo 2:17, "Bwana ameyatenda aliyoyakusudia; amelitimiza neno lake, aliloliamuru siku za kale; ameangusha hata chini, wala hakuona huruma; naye amemfurahisha adui juu yako, ameitukuza pembe ya watesi wako. "
Maombolezo 3: 22-23, "Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu. "
Maombolezo 5: 19-22, "Wewe, Bwana, unadumu milele; kiti chako cha enzi ni tangu kizazi hata kizazi. Mbona watusahau siku zote; na kutuacha muda huu mwingi? Ee Bwana, utugeuze kwako, nasi tutageuka; zifanye mpya siku zetu kama siku za kale. Isipokuwa wewe umetukataa kabisa; nawe una hasira nyingi sana juu yetu. "
Muhtasari kwa kifupi: Kitabu cha Maombolezo kimegawanywa katika sura tano. Kila sura inawakilisha shairi tofauti. Katika asili ya Kiyahudi, mistari ni kama aina ya chemshabongo, ambayo kila mstari unaanzia na herufi inayofuata katika alfabeti ya Kiyahudi. Katika kitabu cha Maombolezo, nabii Yeremia anaelewa kuwa Wababeli walikuwa chombo cha Mungu kwa kuleta hukumu juu ya Yerusalemu (Maombolezo 1: 12-15; 2: 1-8; 4:11). Maombolezo inaweka wazi kwamba dhambi na uasi vilikuwa sababu ya kumwagwa kwa ghadhabu ya Mungu (1: 8-9; 4:13; 5:16). Kuomboleza kunafaa wakati wa taabu, lakini kwa haraka kunapaswa kutoa njia kwa majuto na kutubu (Maombolezo 3: 40-42; 5: 21-22).
Ishara: Yeremia alikuwa anajulikana kama "Nabii anayelialia" kwa ajili ya hamaki kali aliyokuwa nayo kwa watu wake na mji wao (Maombolezo 3: 48-49). Hii huzuni sawa juu ya dhambi za watu na kumkataa Mungu ilionyeshwa na Yesu alipokaribia Yerusalemu na kutazama mbele kwa uharibifu wake katika mikono ya Warumi (Luka 19: 41-44). Kwa sababu ya wayahudi kumkataa Masihi wao, Mungu alitumia kuzingira kwa Warumi kuwaadhibu watu wake. Lakini Mungu hafurahishwi kuwaadhibu watoto wake na toleo lake la Yesu Kristo kama utoaji kwa ajili ya dhambi linaonyesha huruma yake kubwa juu ya watu wake. Siku moja, kwa sababu ya Kristo, Mungu atayafuta machozi yote (Ufunuo 7:17).
Vitendo Tekelezi: Hata katika hukumu ya kutisha, Mungu ni Mungu wa tumaini (Maombolezo 3: 24-25). Haijalishi ni umbali gani tumekwenda kutoka kwake, tuna matumaini kwamba tunaweza kurudi kwake na kumpata mwenye huruma na mwenye kusamehe (1 Yohana 1: 9). Mungu wetu ni Mungu mwenye upendo (Maombolezo 3:22), na kwa sababu ya upendo wake mkuu na huruma, alimtuma mwana wake ili tusiangamie katika dhambi zetu, bali tuweze kuishi pamoja naye milele (Yohana 3:16). Uaminifu wa Mungu (Maombolezo 3:23) na ukombozi (Maombolezo 3:26) ni sifa ambazo zinatupa matumaini makubwa na faraja. Yeye si mungu hasiyependelea na kigeugeu, bali Mungu atakayeokoa wale wote watakaomgeukia, wakubali hawawezi kufanya chochote kupata neema zake, na tuombe huruma ya Bwana ili tusiangamie (Maombolezo 3:22 ).
English
Kitabu cha Maombolezo