settings icon
share icon

Kitabu cha Matendo

Mwandishi: kitabu cha Matendo hakimtaji wazi mwandishi wake. Kutoka Luka 1: 1-4 na Matendo 1: 1-3, ni wazi kwamba mwandishi mmoja aliandika Luke na Matendo. Utamaduni kutoka siku za mwanzo wa kanisa imekuwa kwamba Luka, rafiki wa mtume Paulo, aliandika Luka na Matendo (Wakolosai 4:14; 2 Timotheo 4:11).

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Matendo huenda kiliandikwa kati ya 61-64 AD

Kusudi la Kuandika: kitabu cha Matendo kiliandikwa kutoa historia ya kanisa la kwanza. Mkazo wa kitabu ni umuhimu wa siku ya Pentekoste na kutiwa nguvu kuwa mashahidi madhubuti wa Yesu Kristo. Matendo yananakili kuwa mitume alikuwa shahidi wa Kristo katika Yerusalemu, Yudea, Samaria, na kwa sehemu zingine za dunia. kitabu kinamwaga mwanga juu ya zawadi ya Roho Mtakatifu, ambaye hutia nguvu, huelekeza, hufundisha, na kuhudumu kama Mshauri wetu. Kusoma kitabu cha Matendo, tunaelimishwa na kutiwa moyo na miujiza mingi ambayo ilifanywa wakati huu na mitume Petro, Yohana, na Paulo. kitabu cha Matendo kinasisitiza umuhimu wa kutii Neno la Mungu na mabadiliko ambayo hutokea kama matokeo ya kumjua Kristo. Pia kuna marejeleo mengi ya wale walikataa ukweli ambao mitume walihubiri juu ya Bwana Yesu Kristo. Uwezo, ulafi, na maovu mengine mengi ya shetani yanathibitishwa katika kitabu cha Matendo.

Mistari muhimu: Matendo 1: 8: "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi"

Matendo 2: 4: "Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka."

Matendo 4:12: "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."

Matendo 4: 19-20: "Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia. "

Matendo 9: 3-6: "Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafla ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda. "

Matendo 16:31: "Wakamwambia, mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako."

Muhtasari kwa kifupi: kitabu cha Matendo kinatoa historia ya Kanisa la Kikristo na kuenea kwa Injili ya Yesu Kristo, pamoja na kujibuka kwa upinzani kwake. Ingawa watumishi wengi waaminifu walitumiwa kuhubiri na kufundisha injili ya Yesu Kristo, Sauli, ambaye jina lake lilibadilishwa kuwa Paulo, alikuwa na ushawishi mkubwa zaidi. Kabla hajabadilishwa, Paulo alifurahia sana kuwatesa na kuwaua Wakristo. Mbadiliko wa kuigiza wa Paulo katika barabara ya Dameski (Matendo 9: 1-31) ni mada kuu katika kitabu cha Matendo. Baada ya kuokoka alimpenda Mungu zaidi na kuhubiri Neno lake kwa nguvu, bidii na Roho wa kweli wa Mungu aliye hai. Mitume waliwezeshwa na Roho Mtakatifu kuwa mashahidi wake katika Yerusalemu (sura 1-8: 3), Yudea na Samaria (sura ya 8: 4-12: 25), na hata kwa mwisho wa dunia (sura ya 13: 1- 28). Safari tatu za Paulo za kimishenari zimejumuishwa katika sehemu ya mwisho (13: 1-21: 16), majaribu yake katika Yerusalemu na Kaisaria (21: 17-26: 32) na safari yake ya mwisho kwenda Roma (27: 1-28: 31) .

Mashirikisho: kitabu cha Matendo kinahudumu kama mpito kutoka Agano la Kale la kuzitii sheria hadi kwa Agano jipya la neema na imani. Mpito huu unaonekana katika matukio kadhaa muhimu katika Matendo. Kwanza, kulikuwa na mabadiliko katika huduma ya Roho Mtakatifu, ambaye kazi yake ya kimsingi katika Agano la Kale ilikuwa "upako" wa watu wa Mungu kimwili, miongoni mwa Musa (Hesabu 11:17), Othnieli (Waamuzi 3: 8-10) , Gideoni (Waamuzi 6:34), na Sauli (1 Samweli 10: 6-10). Baada ya ufufuo wa Yesu, Roho alikuja kuishi katika mioyo ya waumini hasa (Warumi 8: 9-11; 1 Wakorintho 3:16), kuelekeza na kuwezesha kutoka ndani. Roho anayekaa ndani yetu ni zawadi ya Mungu kwa wale ambao huja kwake kwa imani.

Wokovu wa Paulo ulikuwa mfano wa kuigiza wa mpito kutoka Agano la Kale hadi kwa jipya. Paulo alikiri kwamba, kulingana na kukutana na Mwokozi aliyefufuka, alikuwa mwenye raghba zaidi wa Waisraeli na alikuwa mkamilifu "kuhusu haki ya sheria" (Wafilipi 3: 6 NKJV), akizidi hata kuwatesa wale waliofundisha wokovu kwa neema kupitia kwa imani katika Kristo. Lakini baada ya kuokoka kwake, akagundua kuwa uwezo wake wote wa kisheria ulikuwa hauna maana, akisema kuwa aliuchukulia kuwa "takataka, ili nimpate Kristo na kupatikana katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ni ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani "(Wafilipi 3: 8b-9). Sasa sisi pia tunaishi kwa imani, si kwa matendo ya sheria, hivyo hakuna kujisifu (Waefeso 2: 8-9).

Maono ya Petro ya demani katika Matendo 10: 9-15 ni ishara nyingine ya mpito kutoka Agano la kale – katika suala hili sheria ya malazi hasa kwa Wayahudi – kwa umoja wa Agano jipya la Wayahudi na Mataifa mengine katika Kanisa moja. Wanyama "Safi" walioashiria Wayahudi na wanyama "chafu" walioashiria mataifa mengine wote walitangazwa kuwa "wametakaswa" na Mungu kwa kifo cha dhabihu cha Kristo. Pasi na kuwa chini ya Agano la Kale la sheria, wote wamepatanishwa katika agano jipya la neema kupitia kwa imani katika damu iliyomwagika ya Kristo juu ya msalaba.

Vitendo Tekelezi: Mungu anaweza kufanya mambo ya ajabu kupitia kwa watu wa kawaida wakati amewawezesha kupitia kwa Roho wake. Kimsingi Mungu alichukua kundi la wavuvi na kuwatumika kuupindua ulimwengu (Matendo 17: 6). Mungu alichukua muuaji aliyechukia wakristo na kumbadilisha kuwa mwinjilisti mkristo mkuu, mwandishi wa karibu nusu ya vitabu vya Agano Jipya. Mungu alitumia mateso ili kusababisha upanuzi wa haraka wa "imani mpya" katika historia ya dunia. Mungu anaweza kufanya hivyo kupitia kwetu- kubadilisha mioyo yetu, kutuwezesha kwa Roho Mtakatifu, na kutupa mapenzi ya kueneza habari njema ya wokovu kupitia kwa Kristo. Ikiwa tutajaribu kutimiza mambo haya kwa nguvu zetu wenyewe, tutashindwa. Kama mitume katika Matendo 1: 8, tunapaswa kungojea uwezo wa Roho, kisha kwenda katika nguvu zake kutimiza Agizo Kuu (Mathayo 28: 19-20).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Matendo
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries