settings icon
share icon

Kitabu cha Nahumu

Mwandishi: Mwandishi wa Kitabu cha Nahumu anajitambulisha kama Nahumu (kwa Kiebrania "mfariji" au "Msaidizi") Mwelkoshi (1: 1). Kuna nadharia nyingi za kuelezea mahali ambapo mji huo ulikuwa ingawa hakuna ushahidi wa kuhitimiza. Mojawapo ya nadharia hizo ni ile inayorejelea ambayo baadaye iliitwa Kafarnaumu (ambayo kihalisi linamaanisha "kijiji cha Nahumu") katika Bahari ya Galilaya.

Tarehe ya kuandikwa: Kutokana na kiasi kidogo cha habari tunayojua kumhusu Nahumu tunachoweza kufanya bora ni kupunguza muda wa kuandikwa kwa kitabu cha Nahumu hadi kati ya 663 na 612 kk. Matukio mawili yametajwa ambayo yanatusaidia kuamua tarehe hizi. Kwanza Nahumu anataja Thebes (No Amon) katika Misri kuanguka kwa Waashuri (663 kk) katika wakati uliopita, hivyo ilikuwa tayari imefanyika. Pili, salio la unabii wa Nahumu ulikuja kuwa kweli katika 612 kk

Kusudi la Kuandika: Nahumu hakuandika kitabu hiki kama onyo au "kuwaita watubu" kwa ajili ya watu wa Ninawi. Mungu alikuwa tayari amewatumia nabii Yona miaka 150 iliyopita na ahadi yake ya kitakachotokea ikiwa waliendelea katika njia zao mbaya. watu wakati huo walikuwa wametubu lakini sasa waliishi tu vibaya kama si vibaya zaidi kuliko walivyokuwa awali. Waashuri walikuwa wamekuwa katili kabisa katika utawala wao (kuning’inisha miili ya mateka wao juu ya miti na kuweka ngozi zao juu ya kuta za hema zao miongoni mwa maovu mengine). Sasa Nahumu alikuwa akiwaambia watu wa Yuda, wasikate tamaa kwa sababu Mungu alikuwa ametangaza hukumu na Waashuri karibuni watapata kile wanachostahili.

Mistari muhimu: Nahumu 1: 7, "Bwana ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao. "

Nahumu 1: 14a. "Tena Bwana ametoa amri katika habari zako, Ninawi: ya kwamba asipandwe tena mtu awaye yote mwenye jina lako.'"

Nahumu 1: 15a, "Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani" Angalia pia Isaya 52: 7 na Warumi 10:15.

Nahumu 2: 13a, "Tazama mimi ni juu yako, asema Bwana wa majeshi."

Nahumu 3:19, "Jeraha yako haipunguziki; jeraha yako ni nzito sana; wote wasikiao habari zako wapiga makofi juu yako; kwa maana ni nani ambaye uovu wako haukupita juu yake daima?"

Muhtasari kwa kifupi: Ninawi walikuwa wameitikia wito wa mahubiri ya Yona na wakageuka kutoka kwa njia zao mbaya kumtumikia Bwana Mungu Yehova. Lakini miaka 150 baadaye, Ninawi ikarudi kuabudu sanamu, vurugu na kiburi (Nahumu 3: 1-4). Kwa mara nyingine tena Mungu akatuma mmoja wa manabii wake Ninawi kuhubiri hukumu katika uharibifu wa mji na kuwaonya watubu. Cha kusikitisha, watu wa Ninawi hawakutilia maanani onyo za Nahumu na mji ukawekwa chini ya utawala wa Babeli.

Ishara: Paulo anarudia Nahumu 1:15 katika Warumi 10:15 kuhusiana na Masihi na huduma yake, kama vile mitume wa Kristo kwa wakati wake. Pia inaweza kueleweka kwa mtumishi yeyote wa Injili ambaye wajibu wake ni 'kuhubiri Injili ya amani. " Mungu amefanya amani na wenye dhambi kwa damu ya Kristo, na amewapa watu wake amani ambayo "ipitayo fahamu zote" (Wafilipi 4: 7). kazi ya mhubiri pia ni "kuleta habari njema za mambo mema" (KJV), kama vile maridhiano, haki, msamaha, uzima, na wokovu wa milele kwa Kristo aliyesulubiwa. Mahubiri ya Injili kama hiyo, na kuleta habari kama hizo, hufanya miguu yao kuwa mizuri. picha hapa ni ya mtu ambaye hukimbia kwa wengine, akiwa na hamu na furaha kutangaza Habari Njema.

Vitendo Tekelezi: Mungu ni mvumilivu na si mwepesi wa hasira. Anatoa wakati kwa kila nchi kumtangaza kama Bwana wao. Lakini yeye hadhihakiwi. Wakati wowote nchi inageuka kutoka kwake ili kutumikia nia zake yenyewe, anaingilia kati na hukumu. Karibu miaka 220 iliyopita Amerika iliundwa kama Taifa inayoongozwa na kanuni zilizo katika Biblia. Katika miaka 50 iliyopita hilo limebadilika na wanaendelea kugeuka kila siku katika upande mwingine. Kama Wakristo ni wajibu wetu kusimama kwa kanuni za kibiblia na ukweli wa maandiko kwa kuwa Ukweli ni tumaini la kipekee la nchi yetu.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Nahumu
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries