settings icon
share icon

Kitabu cha Waamuzi

Mwandishi: Kitabu cha Waamuzi hakimtaji kwa wasi mwandishi wake. Utamaduni ni kwamba nabii Samweli alikuwa mwandishi wa kitabu cha Waamuzi. Ushahidi wa ndani unaonyesha kwamba mwandishi wa Waamuzi aliishi muda mfupi baada ya kipindi cha Waamuzi. Samweli anafaa sifa hizi.

Tarehe ya Kuandikwa: Kitabu cha Waamuzi kuna uwezekano kiliandikwa kati ya enzi za 1045 na 1000 BC

Kusudi la Kuandika: Kitabu cha Waamuzi kinaweza kugawanywa katika sehemu mbili: 1) Sura 1-16 ambayo inarekodi vita vya ukombozi kuanzia Wana Wa Israeli kushinda Wakanaani na kumalizia na kushinda Wafilisti na kifo cha Samson, 2) Sura 17-21 ambayo inajulikana kwetu kama kiambatisho na haina husiano na sura zilizopita. Sura hizi zimenakiliwa kama wakati "wakati hapakuwa na mfalme katika Israeli (Waamuzi 17: 6; 18: 1; 19: 1; 21:25)." Kitabu cha Ruthu awali kilikuwa sehemu ya kitabu cha Waamuzi, lakini katika AD 450 kiliondolewa na kikawa kitabu kivyake.

Mistari muhimu: Waamuzi 2: 16-19: "Kisha BWANA akawainua waamuzi, waliowaokoa na mikono ya watu hao waliowateka nyara. Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakaweuka upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za BWANA bali wao hawakufanya hivyo. Na wakati BWANA alipowainulia waamuzi, ndipo BWANA alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo;maana BWANA alighairi kwa ajili ya kuugua kwao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua. Lakini ikawa, wakati alipokufa mwamuzi huyo, wakarudi nyuma wakafanya maovu kuliko baba zao, kwa kuifuata miungu mingine ili kuitumikia, na kuinama mbele yao; hawakuacha matendo yao, wala njia zao za ukaidi."

Waamuzi 10:15: " Wana wa Israeli wakamwambia BWANA Tumefanya dhambi; utufanyie yote uyaonayo kuwa ni mema; lakini tuokoe, twakusihi, siku hii ya leo, haya tu. ".

Waamuzi 21:25: "Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; kila mtu alifanya yaliyokuwa mema machoni pake mwenyewe ."

Muhtasari Kwa Kifupi: Kitabu cha Waamuzi ni rekodi ya kutisha jinsi Bwana [Mungu] alivyokuwa akichukuliwa kimzaha na watoto wake mwaka baada ya mwaka, karne baada ya karne. Waamuzi ni tofauti ya kusikitisha kwa kitabu cha Yoshua ambacho kimeandika juu ya baraka ambazo Mungu alitawaza juu ya Waisraeli kwa utiifu wao kwa Mungu katika kushinda nchi. Katika Waamuzi, walikuwa waasi na wanaoabudu sanamu, na hivyo kusababisha kushindwa kwao mara nyingi. Hata hivyo, Mungu hajawahi kushindwa kufungua mikono yake katika upendo kwa watu wake wakati wanapotubu njia zao mbaya na kuliita jina lake. (Waamuzi 2:18) Kipindi cha waamuzi 15 wa Israeli, Mungu aliheshimu ahadi yake kwa Ibrahimu ya kulinda na kubariki watoto wake (Mwanzo 12: 2-3).

Baada ya kifo cha Yoshua na rika zake, Waisraeli walirudi kuwahudumia Baali na Maashtorethi. Mungu aliwaruhusu Waisraeli kuteseka kutokana na matokeo ya kuabudu miungu ya uongo. Ilikuwa kwamba watu wa Mungu wangelia kwa Bwana kwa msaada. Mungu akawatumia watoto wake waamuzi kuwaongoza katika utakatifu. Lakini baada ya muda wangeweza kukaidi dhidi ya Mungu na kurudi kwa maisha yao ya uovu. Hata hivyo, kwa kuhifadhi sehemu yake ya agano na Ibrahimu, Mungu angeweza kuwaokoa watu wake kutoka katika kukandamizwa katika kipidi cha miaka 480 ya kitabu cha Waamuzi.

Pengine mwamuzi aliyenakiliwa kwa wengi alikuwa mwamuzi wa 12, Samsoni, ambaye alikuja kuwaongoza Waisraeli baada ya miaka 40 ya kufungwa chini ya utawala katili wa Wafilisti. Samsoni akaongoza watu wa Mungu kwa ushindi juu ya Wafilisti ambapo alipoteza maisha yake mwenyewe baada ya miaka 20 kama mwamuzi wa Israeli.

Ishara: Tangazo kwa mamake Samsoni ya kuwa angezaa mwana aongoze Israeli ni ishara ya tangazo kwa Mariamu ya kuzaliwa kwa Masihi. Mungu alimtuma malaika kwa wanawake hawa wote na kuwaambia wangeweza "kuchukua mimba na kuzaa mtoto" (Waamuzi 13: 7; Luka 1:31), mwenye ataongoza watu wa Mungu.

Huruma yake Mungu kukomboa watu wake licha ya dhambi zao na kumkataa kwake inawakilisha mfano wa Kristo juu ya msalaba. Yesu alikufa ili kuwaokoa watu wake-wote watakaomwamini-kutoka dhambi zao. Ingawa wengi wa wale waliomfuata yeye wakati wa huduma yake hatimaye walianguka na kumkataa yeye, bado alibaki mwaminifu kwa ahadi yake na akaenda msalabani kufa kwa ajili yetu.

Vitendo tekelezi: Kutotii kwa kawaida huleta hukumu. Wana wa Israeli wanawakilisha mfano kamili wa kile sisi hatusitaili kufanya. Badala ya kujifunza kutokana na uzoefu kwamba Mungu kawaida ataadhibu uasi dhidi yake, waliendelea kutotii na kuteseka katika hasira na adabu ya Mungu. Kama tutaendelea katika kuasi, tunakaribisha adhabu ya Mungu, si kwa sababu Yeye anafurahia mateso yetu, lakini kwa maana anaadhibu wale awapendao, na umuadhibu kila mtu anayemkubali kama mwanaye." (Waebrania 12: 6).

Kitabu cha Waamuzi ni uwasia wa uaminifu wa Mungu. Hata "kama hatuna imani, yeye atadumu kuwa mwaminifu" (2 Timotheo 2:13). Ingawa tutaweza kuwa si waaminifu kwake, kama Waisraeli walivyokuwa, bado Yeye ni mwaminifu kutuokoa na kutuhifadhi (1 Wathesalonike 5:24) na kutusamehe wakati tutatafuta msamaha (1 Yohana 1: 9). "Ambaye atawathibitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu. "(1 Wakorintho 1: 8-9).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Waamuzi
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries