Kitabu cha Waefeso
Mwandishi: Waefeso 1: 1 inatambua mwandishi wa kitabu cha Waefeso kama mtume Paulo.Tarehe ya kuandikwa: kitabu cha Waefeso huenda kiliandikwa kati ya 60-63 BK.
Kusudi la Kuandika: Paulo alitazamia kwamba wote ambao wanatamani ukomavu wa kikristo watapokea maandiko haya. Iliyoambatanishwa ndani ya kitabu cha Waefeso ni nidhamu inayohitajika kukua ili kuwa watoto wa kweli wa Mungu. Aidha, utafiti katika Waefeso utasaidia kuimarisha na kuanzisha muumini ili aweze kutimiza kusudi na wito ambao Mungu amepeana. Lengo la waraka huu ni kuthibitisha na kuhami kanisa linalokomaa. Linatoa mtazamo sawasawa wa mwili wa Kristo na umuhimu wake katika uwekevu/ukabidhi wa Mungu.
Mistari muhimu: Waefeso 1: 3: "Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo"
Waefeso 2: 8-10: "Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo. "
Waefeso 4: 4-6: "Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja; Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote. "
Waefeso 5:21: "hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo."
Waefeso 6: 10-11: "Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shetani."
Muhtasari kwa kifupi: Mafundisho yanachukuwa sehemu kubwa ya kitabu cha Waefeso. Nusu ya mafundisho katika waraka huu yanahusiana na msimamo wetu katika Kristo, na mafundisho yaliosalia yanaathiri hali zetu. Mara nyingi sana wote wale wanaofundisha kutoka kwa kitabu hiki hupita mafundisho yote ya kimsingi na kwenda moja kwa moja kwa sura ya kumalizia. Ni sura hii ambayo inasisitiza vita au mapambano ya mitume. Hata hivyo, kufaidika kamili kutoka kwa vigezo vya waraka huu, ni lazima mtu kuanzia mwanzoni mwa mafundisho ya Paulo katika barua hii.
Kwanza, kama wafuasi wa Kristo, lazima tuelewe kikamilifu Mungu anatutangazia kuwa yeye ni nani. Ni lazima pia tuwekwe kwa msingi wa maarifa ya ukamilifu wa Mungu kwa wanadamu wote. Lingine, uwepo wetu wa sasa na kutembea lazima kutekelezwe na kuimarishwa. Haya lazima yaendelee mpaka tusiyumbeyumbe tena au kuyumbayumba kurudi nyuma na mbele na kila roho ya mafundisho na watu waovu.
Maandiko ya Paulo yanajigawa kwa makundi matatu makuu. (1) Sura ya kwanza hadi ya tatu zinadokeza kanuni kulingana na ukamilifu wa Mungu. (2) Sura ya nne na tano zinaonyesha kanuni kuhusu uwepo wetu wa sasa. (3) Sura ya sita inadokeza kanuni kuhusu mapambano yetu ya kila siku.
Mashirikisho: Kipatanisho cha msingi kwa Agano la Kale katika Waefeso ni katika kwezi (kwa Wayahudi) dhana ya kanisa kama mwili wa Kristo (Waefeso 5:32). Siri hii ya ajabu (ukweli ambao awali haukufunuliwa) ya kanisa, ni "ya kwamba mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya injili" (Waefeso 3: 6). Hii ilikuwa siri ambayo ilifichwa kabisa kutoka kwa mitume wa Agano la Kale (Waefeso 3: 5, 9). Waisraeli ambao walikuwa wafuasi wa kweli wa Mungu siku zote waliamini kuwa wao pekee ndio walikuwa wateule wa Mungu (Kumbukumbu 7: 6). Kukubali Mataifa kuwa kwa hali sawa katika kielelezo hiki kipya kulikuwa vigumu sana na kulisababisha migogoro mingi miongoni mwa waumini Wayahudi na Mataifa waliookoka. Paulo pia anazungumzia siri ya kanisa kama "bibi harusi wa Kristo," kauli ambayo awali haikusikika katika Agano la Kale.
Vitendo Tekelezi: Labda zaidi kuliko kitabu kingine chochote cha Biblia, kitabu cha Waefeso kinasisitiza uhusiano kati ya mafundisho ya kweli na mwenendo wa haki katika maisha ya Kikristo. Mbali watu wengi mno hupuuza "teolojia" na badala yake wanataka tu kujadili mambo ambayo ni "tekelezi." Katika Waefeso, Paulo anahimiza kuwa teolojia ni tekelezi. Ili kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu kwa ajili yetu katika maisha yetu tendaji, ni lazima kwanza tuelewe sisi ni nani katika Kristo kimafundisho.
English
Kitabu cha Waefeso