settings icon
share icon

Kitabu cha Yona

Mwandishi: Yona 1: 1 hasa inabainisha nabii Yona kama mwandishi wa Kitabu cha Yona.

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Yona huenda kiliandikwa kati ya 793 na 758 kk

Kusudi la Kuandika: Kutotii na ufufuaji ndizo mada muhimu katika kitabu hiki. Uzoefu wa Yona katika tumbo la nyangumi unampea fursa ya kipekee ya kutafuta ukombozi wa kipekee, kama anapotubu wakati huu sawa wa kipekeewa wa kurudi nyuma. Uasi wake wa awali unasababisha sio tu ufufuaji wake binafsi, bali pia wa watu wa Ninawi. Wengi waainisha/wanatabakisha ufufuaji ambao Yona anauleta Ninawi kama mojawapo wa juhudi kubwa zaidi ya uinjilisti kwa wakati wote.

Mistari muhimu: Yona 1: 3, "Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa Bwana…."

Yona 1:17, "Bwana akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku."

Yona 2: 2, "Akasema, nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, naye akaniitikia; katika tumbo la kuzimu naliomba, nawe ukasikia sauti yangu."

Yona 3:10, "Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighahiri neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende."

Muhtasari kwa kifupi: Uhofu wa Yona na kiburi vinamsababisha kukimbia kutoka kwa Mungu. Yeye hataki kwenda Ninawi kuhubiri toba kwa watu, kama Mungu alivyoagiza, kwa sababu anahisi wao ni maadui wake, na anashawishika kwamba Mungu hawezi kutekeleza tishio lake la kuharibu mji. Badala yake anaabiri meli kwenda Tarshishi, ambayo iko katika upande mwingine. Mara dhoruba kali inawasababisha wafanyakazi wa meli kupiga kura na kutambua kwamba Yona ndiye alikuwa tatizo. Walimtupa kutoka kwa meli, na anamezwa na samaki mkubwa. Katika tumbo lake kwa siku 3 na usiku 3, Yona alitubu dhambi zake kwa Mungu, na samaki inamtapika juu ya nchi kavu (tunastaajabu ni nini kilimchukua muda mrefu kutubu). Kisha Yona anaenda safari ya maili 500 kwenda Ninawi na kuongoza mji katika ufufuaji mkubwa. Lakini nabii hakufurahishwa (anabibidua midomo hakika) badala ya kushukuru wakati Ninawi inatubu. Yona anasoma funzo lake , hata hivyo, wakati Mungu anatumia upepo, kibuyu na minyoo kumfunza kwamba Yeye ni mwenye huruma.

Ishara: Kwamba Yona ni mfano wa Kristo ambao ni wazi kutokana na maneno ya Yesu mwenyewe. Katika Mathayo 12: 40-41, Yesu anatangaza kwamba atakuwa katika kaburi kiasi cha muda sawa na ule ambao Yona alikuwa tumboni mwa nyangumi. Anaendelea kwa kusema kuwa wakati watu wa Ninawi walitubu katika uso wa mahubiri ya Yona, Mafarisayo na walimu wa Sheria ambao walimkataa Yesu walikuwa wakimkataa yule ambaye ni mkuu zaidi kuliko Yona. Tu kama Yona alileta ukweli wa Mungu kuhusu toba na wokovu kwa watu wa Ninawi, hivyo ndivyo pia Yesu analeta ujumbe sawa na huo (Yona 2: 9; Yohana 14: 6) wa wokovu wa na kupitia kwa Mungu peke yake (Warumi 11:36).

Vitendo Tekelezi: Hatuwezi kujificha kutoka kwa Mungu. Apendacho kukamilisha kupitia kwetu lazima kitimie, licha ya pingamizi zetu zote na kufuta nyuma. Waefeso 2:10 inatukumbusha kuwa ana mipango kwa ajili yetu na atahakikisha kwamba tumepatana na mipango hiyo. Jinsi gani itakuwa rahisi ikiwa, tofauti na Yona, tutajiwasilisha kwake bila kuchelewa!

Upendo wa Mungu unajidhihirisha katika upatikanaji wake kwa wote, bila kujali sifa zetu, utaifa au tabaka. Toleo la bure la Injili ni kwa watu wote katika nyakati zote. Kazi yetu kama Wakristo ni kuwa njia ambayo kwayo Mungu anaambia dunia kuhusu matoleo na kufurahi katika wokovu wa wengine. Huu ni uzoefu ambao Mungu anataka tushiriki pamoja naye, si kuwa na wivu au wenye chuki kwa wale ambao wanakuja kwa Kristo katika "wokovu wa dakika ya mwisho" au ambao wanakuja kupitia kwa hali zisizo sawa na zetu wenyewe.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Yona
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries