Kitabu cha Zaburi
Mwandishi: Maelezo mafupi yanayoanzisha zaburi yanaorodhesha David kama mwandishi katika matukio 73. Utu na utambulisho wa Daudi umenakiliwa katika Zaburi hizi. Wakati ni wazi kwamba Daudi aliandika zaburi nyingi zake binafsi, dhahiri yeye si mwandishi wa mkusanyiko mzima. Zaburi mbili(72) na (127) zinahusishwa na Sulemani, mwana na mrithi wa Daudi. Zaburi 90 ni maombi yanayohusishwa na Musa. Kundi kingine cha Zaburi 12 (50) na (73-83) kimehusishwa kwa familia ya Asafu. Wana wa Kora waliandika Zaburi 11 (42, 44-49, 84-85,87-88). Zaburi 88 imehusishwa na Hemani, wakati (89) imehusishwa na Ethani Mwezrahi. Kando na Sulemani na Musa, waandishi hawa wote wa ziada walikuwa makuhani au Walawi ambao walihusika na kutoa muziki kwa ibada madhabahuni wakati wa utawala wa Daudi. Zaburi hamsini hazimuhusishi mtu maalum kama mwandishi.Tarehe ya kuandikwa: Uchunguzi wa kina wa swali la uandishi, vile vile masuala yaliyoshughulikiwa na zaburi zenyewe, unaonyesha kuwa zilichukua muda wa takribani karne nyingi. Zaburi kongwe zaidi katika mkusanyiko pengine ni maombi ya Musa (90), kulingana na hali ya akili ya mtu ikilinganishwa na Mungu wa milele. Zaburi ya nyuma kabisa pengine ni(137), wimbo wa kuomboleza ulioandikwa wazi wakati wa siku ambazo Waebrania walikuwa wameshikwa mateka na Wababeli, tangia 586-538 kk
Ni wazi kwamba zaburi 150 za kibinafsi ziliandikwa na watu wengi mbalimbali katika kipindi cha miaka elfu katika historia ya Israeli. Lazima zilikuwa zimekusanywa na kuwekwa pamoja katika hali yao ya sasa na baadhi ya waahariri wasiojulikana muda mfupi baada ya utumwa kuisha karibu 537 kk
Kusudi la Kuandika: Kitabu cha Zaburi ndicho kitabu kirefu zaidi katika Biblia, kikiwa na zaburi 150 za kibinafsi. Pia ni mojawapo cha anuwai, kwa vile zaburi zinzshughulikia mada kama vile Mungu na uumbaji wake, vita, ibada, hekima, dhambi na uovu, hukumu, haki, na kuja kwa Masihi.
Mistari muhimu: Zaburi 19: 1 "Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, na anga laitangaza kazi ya mikono yake. "
Zaburi 22: 16-19, "Kwa maana mbwa wamenizunguka; kusanyiko la waovu wamenisonga; wamenizua mikono na miguu. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; wao wananitazama na kunikodolea macho. Wanagawanya nguo zangu, na vazi langu wanalipigia kura. Nawe, Bwana, usiwe mbali, ee nguvu zangu, fanya haraka kunisaidia. "
Zaburi 23: 1, "Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Zaburi 29: 1-2, ". Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu, mpeni Bwana utukufu na nguvu. Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu ."
Zaburi 51:10, "Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu."
Zaburi 119: 1-2, "Heri walio kamili njia zao, waendao katika sheria ya Bwana. Heri wazitiio shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wote."
Muhtasari kwa kifupi: Kitabu cha Zaburi ni mkusanyiko wa maombi, mashairi na nyimbo ambazo zinalenga mawazo ya mwenye anaabudu Mungu katika sifa na kuabudu. Sehemu za kitabu hiki zilitumika kama nyimbo katika ibada ya Israeli ya kale. urithi wa kimuziki wa zaburi umeonyeshwa na mada yake. Inatokana na neno la Kigiriki ambalo linamaanisha "wimbo unaoimbwa na vyombo vya kimuziki."
Ishara: Mungu kutoa Mwokozi kwa watu wake ni mada inayorudiwa rudiwa katika Zaburi. Picha za kinabii za Masihi zinaonekana katika zaburi nyingi. Zaburi 2: 1-12 Inaonyesha ushindi na ufalme wa Masihi. Zaburi 16: 8-11 inaashiria kifo na ufufuo wake. Zaburi 22 inatuonyesha Mwokozi anayeteseka msalabani na inatoa unabii wa kina wa kusulubiwa, ambao wote ulitimilizwa kikamilifu. Utukufu wa Masihi na bibi arusi wake umedhihirishwa katika Zaburi 45: 6-7, wakati Zaburi 72: 6-17, 89: 3-37, 110: 1-7 na 132: 12-18 zinawasilisha utukufu na umoja wa utawala wake.
Vitendo Tekelezi: Mojawapo ya matokeo ya kujazwa na Roho au neno la Kristo ni kuimba. Zaburi ni "kitabu cha nyimbo" cha kanisa la kwanza ambalo lilionyesha ukweli mpya katika Kristo.
Mungu ndiye Bwana mmoja katika zaburi zote. Lakini tunaitikia wito wake kwa njia tofauti, kulingana na hali maalum ya maisha yetu. Nini Mungu wa ajabu vipi tunayemwabudu, mtunzi wa zaburi anatangaza, Yule aliye juu sana na aliyeinuliwa juu zaidi ya uzoefu wetu wa kibinadamu lakini pia mmoja ambaye yu karibu sana kwa kugusa na ambaye anatembea kando yetu sambamba na njia ya maisha.
Tunaweza kuleta hisia zetu zote kwa Mungu- haijalishi ni hasi kiasi gani au ni za kulalamika na tunaweza kupumzika tukiwa na hakika kwamba Yeye atasikia na kuelewa. Mtunzi wa zaburi anatufundisha kwamba sala yenye maana zaidi ya zote ni kilio ili kupata msaada tunapojipata tumezidiwa na matatizo ya maisha.
English
Kitabu cha Zaburi