Swali
Ina maana gani kwamba Mkristo ni kiumbe kipya (2 Wakorintho 5:17)?
Jibu
Kiumbe kipya kimeelezewa katika 2 Wakorintho 5:17: "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya" Neno"kwa hiyo" linatuelezea kwenye mstari wa 14-16 ambapo Paulo anatuambia kwamba waumini wote wamekufa pamoja na Kristo na hawaishi kwa wao wenyewe. Maisha yetu si tena ya kidunia; sasa ni wa kiroho. "Kifo" chetu ni kile cha asili ya dhambi ya zamani ambayo ilikuwa imefungwa msalabani na Kristo. Ilizikwa pamoja Naye, na kama vile alivyofufuliwa na Baba, ndivyo tunavyofufuliwa "kutembea katika uzima upya" (Warumi 6: 4). Mtu mpya ambaye alifufuliwa ndiye Paulo anamsema katika 2 Wakorintho 5:17 kama "kiumbe kipya."
Ili kuelewa kiumbe kipya, kwanza lazima tuelewe kwamba ni kweli uumbaji, kitu kilichoumbwa na Mungu. Yohana 1:13 inatuambia kwamba uzao huu mpya uliletwa na mapenzi ya Mungu. Sisi hatukurithi asili mpya, wala hatukuamua kujiumba upya tena, wala Mungu hakusafisa asili yetu ya kale; Aliumba kitu kipya kabisa na cha pekee. Kiumbe kipya ni kipya kabisa, kilichotolewa kutoka utubu, kama ulimwengu wote ulivyoumbwa na Mungu kutoka utubu. Muumba pekee ndiye anayeweza kufanikisha tendo la ajabu kama hilo.
Pili, "mambo ya kale yamepita." "Kale" inahusu kila kitu ambacho ni sehemu ya asili yetu ya asili-kiburi cha asili, upendo wa dhambi, kutegemea kazi, na maoni yetu ya zamani, tabia na tamaa. Kwa maana zaidi, kile tulichokipenda kimepita, hasa upendo mkuu wa nafsi na kwa kuwa haki ya kujitegemea, kujiinua, na kujitakaza wenyewe. Kiumbe kipya kutoka kinamtazamia Kristo badala ya kujitizamia nafsi yao ya ndani. Mambo ya zamani yalikufa, yalisulibiwa msalabani pamoja na asili yetu ya dhambi.
Pamoja na ukale kupita, "upya umekuja!" Mambo ya kale, yaliyokufa yamebadilishwa na mambo mapya, kamili ya maisha na utukufu wa Mungu. Wazaliwa wachanga hufurahia mambo ya Mungu na huchukia mambo ya ulimwengu na mwili. Madhumuni yetu, hisia, tamaa, na fahamu ni safi na tofauti. Tunaona ulimwengu njia tofauti. Biblia inaonekana kuwa kitabu kipya, na ingawa tunaweza kuwa tuliisoma mbeleni, kuna uzuri juu yake ambao hatujawahi kuuona hapo awali, na ambao tunastaajabia kuwa hatujaujua. Tabia nzima ya asili inaonekana kwetu kubadilishwa, na tunaonekana kuwa katika ulimwengu mpya. Mbingu na dunia zinajazwa na maajabu mapya, na vitu vyote vinaonekana sasa kuongea sifa ya Mungu. Kuna hisia mpya kwa watu wote-aina mpya ya upendo kwa familia na marafiki, huruma mpya kamwe hatujawai kuihisi mbeleni kwa adui zetu, na upendo mpya kwa watu wote. Dhambi ambayo wakati mmoja tuliyoishikilia, sasa tunataka kuikoma milele. "mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake" (Wakolosai 3: 9), na kuvaa "utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli" (Waefeso 4:24).
Je! Itakuaje kwa Mkristo anayeendelea kutenda dhambi? Kuna tofauti kati ya kuendelea kutenda dhambi na kuendelea kuishi katika dhambi. Hakuna mtu anayefikia ukamilifu usio na dhambi katika maisha haya, lakini Mkristo aliyekombolewa anajitakasa (alifanywa mtakatifu) siku baada ya siku, anapunguza dhambi anayofanya na kuchukia kila wakati anapoanguka. Ndiyo, bado tunatenda dhambi, lakini si kwa kupenda na kuipunguza mara kwa mara tunapokua. Ubinafsi wetu mpya huchukia dhambi ambayo bado imetuchukua. Tofauti ni kwamba utu upya hauko tena chini ya utumwa wa dhambi, kama tulipokuwa zamani. Sasa tuna huru kutoka kwa dhambi na hauna nguvu juu yetu (Warumi 6: 6-7). Sasa tuna nguvu na kwa haki. Sasa tuna uchaguzi wa "kuruhusu dhambi kututawala" au kujihesabu wenyewe "jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu" (Warumi 6: 11-12). Bora zaidi, sasa tuna uwezo wa kuchagua Maisha mapya.
Uumbaji mpya ni jambo la kushangaza, linaloundwa katika akili ya Mungu na kuumbwa kwa nguvu zake na kwa utukufu wake.
English
Ina maana gani kwamba Mkristo ni kiumbe kipya (2 Wakorintho 5:17)?