Swali
Je! Kiyunani cha Koine ni gani, na ni kwa nini Agano Jipya liliandikwa kwa lugha ya koine?
Jibu
Koine kwa ufupi ni neno la Kigiriki la "kawaida." Watu wengi wanaweza kutambu neno koine kutoka kwa neno Koinonia (ushirika) ambalo humaanisha "ushirika." Ushirika ni na jambo la kufanya kwa pamoja.
Kigiriki cha Koine kilikuwa lugha ya kawaida katika ulimwengu wa Mediterania katika karne ya kwanza. Vile Alexander Mkuu alivyoshinda "ulimwengu uliostaarabika" wa wakati wake, alieneza lugha ya Kigiriki na utamaduni. Hasa kama vile kiingereza kimekuwa hii leo, Kiyunani kilikuwa lugha ya kawaida na kuenea kote "lugha ya kimataifa" ya siku hiyo. Tangu watu wengi wangeelewa koine, ilifaa kueneze injili kipekee ulimwenguni kote.
Kiyunani cha Koine hakikuwa lugha ya kawaida tu kwa namna kuwa kilifurahiya uenezaji katika ngome za Rumi, bali kilikuwa cha kawaida kwa namna kuwa hakikuwa lugha ya wachanganuzi na wasomi. Kiyunani cha kifalsafa kilitumika na wasomi tu pekee. Kiyunani cha koine ilikuwa lugha ya mfanyi kazi, wakulima, wachuuzi, wake wa kukaa nyumbani- hakukuwa na jambo lolote la kujigamba. Ilikuwa lugha ya mama au lugha chafu ya siku hizo. Kazi kubwa za fasihi ya Ugiriki ziliandikwa kwa lugha ya kifalsafa. Hakuna msomi hii leo atajali kusoma chochote kilichoandikwa katika Kiyunani cha koiné, isipokuwa kweli kwamba ni lugha ya Agano Jipya. Mungu alikusudia Neno lake lipatikane kwa kila mtu, ana Alichagua koiné lugha ya kawaida ya siku hizo
"Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi msomi? Yuko wapi mwanafalsafa wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa upumbavu? Kwa kuwa katika hekima ya Mungu, ulimwengu kwa hekima yake haukumjua yeye, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wale walioamini kwa upuzi wa lile neno lililohubiriwa… Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa mlipoitwa. Kwa kipimo cha kibinadamu, si wengi wenu mliokuwa na hekima. Si wengi mliokuwa na ushawishi, si wengi mliozaliwa katika jamaa zenye vyeo. Lakini Mungu alivichagua vitu vipumbavu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye hekima, Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye nguvu. Alivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko, ili mtu yeyote asijisifu mbele zake. Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu, yaani haki, na utakatifu na ukombozi. Hivyo, kama ilivyoandikwa: "Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana'" (1 Wakorintho 1:20-22, 26-31). Paulo hakuwa anarejelea haswa Kiyunani cha Koine, lakini Mungu kutumia lugha ya kawaida ili kuelezea ukweli madhubuti wa injili unaonekana kufaa mtindo huo vyema.
English
Je! Kiyunani cha Koine ni gani, na ni kwa nini Agano Jipya liliandikwa kwa lugha ya koine?