settings icon
share icon
Swali

Je! Kuna umuhimu gani wa koo katika Biblia?

Jibu


Biblia ina wingi wa kumbukumbu za nasaba. Wengi wetu hupitia sehemu hizo au pengine huzipifuka, huku wanazipata kutokuwa na umuhimu au pengine ya kuchosha. Walakini, hii ni sehemu ya Maandiko, na jinsi Maandiko yote ni pumzi ya Mungu (2Timotheo 3:16), lazima ziwe na umuhimu fulani. Lazima kuwe na kitu tunaweza kujifunza kutoka kwa orodha hii.

Kwanza, nasaba hutusaidia kuthibitisha usahihi wa historia ya Biblia. Orodha hii inathibitisha kuwepo halisi kwa wahusika wa Biblia. Kwa kujua historia ya familia, tunaelewa kwamba Biblia ni zaidi ya hadithi ya kawaida au mifano ya jinsi tunastahili kuishi maisha yetu. Ni ukweli thabiti wa historia. Mtu halisi aliyeitwa Adamu alikuwa na ukoo halisi (na kwa hivyo, dhambi yake halisi ilikuwa na madhara halisi).

Nasaba pia unathitisha unabii. Masiha alitabiriwa kutoka katika ukoo wa Daudi (Isaya 11:1). Kwa kunakili kizazi chake katika Maandiko, Mungu anathibitisha kuwa Yesua alikuwa uzao wa Daudi (ona Mathayo 1:1-17 na Luka 3:23-38). Ukoo ni mojawapo ya ushuhuda kuwa Yesu Kristo alitimiza unabii wa Agano la Kale.

Orodha hiyo pia inadhihirisha asili tendeti ya Mungu na vile ana haja na mtu binafsi. Mungu hakuiona Israeli kwa waziwazi, kama wingu la kundi la watu; aliwaona kwa bayana, ufasaha na utendeti. Hakuna chochote kilichojitenga kuhusu nasaba. Zote zinaonyesha jinsi Mungu alivyohusika. Neno lililo na pumzi ya Mungu linataja watu kwa majina yao. Watu halisi walio na historia halisi na hatima halisi. Mungu anamjali kila Mutu na maisha yao kwa undani (Mathayo 10:27-31; Zaburi 139).

Mwisho, tunaweza kujifunza kutok kwa watu anuwai walioorodheshwa kwenye nasaba. Baadhi ya orodha zina zehemu za simulizi ambazo hutupa muhtasari wa maisha ya watu. Kwa mfano, sala ya Yabesi inapatika katika nasaba (1 Mambo ya Nyakati 4:9-10). Kutoka kwa hili, tunajifunza juu ya tabia ya Mungu na hali ya maombi. Nasaba zingine zinafunua kwamba Ruth una Rahabu wako katika ukoo wa Kimasihi (Ruthu 4:21-22; Mathayo 1:5). Tunaona kuwa Mungu hudhamini maisha ya watu hao, hata kama walikuwa watu wa mataifa na sio sehemu ya watu wake wa agano.

Huku nasaba kwa mwangalio wa kwanza zinaweza kuonekana kuwa hazima umuhimu wowote, lakini zinachukua nafasi muhimu katika Maandiko. Nasaba uunga mkono uhistoria wa Maandiko, unathibitisha unabii, na kutupa utambuzi wa tabia ya Mungu na maisha ya watu Wake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kuna umuhimu gani wa koo katika Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries