settings icon
share icon
Swali

Yesu alimaanisha nini aliposema, 'Kizazi hiki hakitapita?'

Jibu


Nukuu hii ya Yesu kuhusiana na nyakati za mwisho hupatikana katika Mathayo 24:34; Marko 13:30; na Luka 21:32. Yesu akasema, "Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia." Mambo ambayo Yesu alikuwa akiyazungumzia — kuinuka kwa Mpinga Kristo, uharibifu wa mahali patakatifu, na jua kuwa giza-hayakutokea wakati wa maisha ya watu walioishi wakati wa Yesu. Kwa kawaida, Yesu alimaanisha kitu tofauti wakati alipokuwa akisema "kizazi hiki."

jambo kuu kwa kuelewa kile Yesu alimaanisha kwa kusema " kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia" ni mkudhadha; yaani, tunapaswa kuelewa aya zinazozunguka Mathayo 24:34, hasa aya kabla yake. Katika Mathayo 24: 4-31, Yesu kwa wazi anatoa unabii; Anazungumzia matukio ya baadaye. Yesu alikuwa amewaambia wale walioishi wakati wa huduma yake duniani kwamba ufalme ulikuwa umeondolewa kutoka kwao (Mathayo 21:43). Kwa hivyo, ni muhimu kwamba Mathayo 24-25 ionekane mambo ya wakati ujao. Kizazi ambacho Yesu anasema kuwa "hakitapita" hadi atakaporudi ni kizazi cha baadaye, yaani, watu wanaoishi wakati wa matukio yaliyotajwa yatatokea. Neno Kizazi linarejelea watu wanaoishi wakati ujao wakati wa matukio ya Mathayo 24-25 yatatokea.

Hoja ya Yesu katika maneno yake, " kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia," ni kwamba matukio ya nyakati za mwisho yatatokea haraka. Pindi ishara za mwisho wa dunia zitakapoanza kuonekana, mwisho vile vile uu njiani-ujio wa mara ya pili na hukumu zitatokea katikati mwa kizazi hiki cha mwisho. Yesu aliimarisha maana hii kwa mfano katika Mathayo 24: 32-33: "Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa mavuno umekaribia. Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo haya yote yakitendeka, jueni kwamba yuko karibu." Ishara ya kweli ya majira ya joto ni majani kumea; ishara ya kweli ya mwisho wa dunia ni kwamba "mambo haya yote" (ya Mathayo 24) yanatokea. Wale ambao wanaoishi duniani basi muda umebaki utakuwa mfupi.

Ufafanuzi mwingine ni kwamba unabii wa Yesu katika Mathayo 24 una "utimilifu mara mbili." Katika mtazamo huu, "kizazi hiki" ni watu ambao Yesu alikuwa akizungumza nao wakati ule — baadhi ya yale aliyotabiri yalikuwa yatatokee wakati wao. Hivyo, wakati Warumi waliharibu Yerusalemu mwaka wa 70 Kabla Yesu kuzaliwa, unabii wa Yesu ulitimiwa kwa sehemu; kuanguka kwa Yerusalemu kulipisha uharibifu wa mambo mabaya yatakayo tokea. Hata hivyo, mambo mengi ya unabii wa Yesu hayakutokea katika AD 70; kwa mfano, ishara za mbinguni za Mathayo 24: 29-31.Tatizo kuu na tafsiri ya "utimifu uwili" ni kwamba hailingani na maneno ya Yesu kuwa mambo haya "yote" yatatokea katika "kizazi hiki." Kwa hivyo, ni bora kuelewa kwamba neno "kizazi hiki" kurejelea kizazi kitakacho kuwa hai wakati wa matukio ya nyakati za mwisho yatakapotokea.

Kwa kweli, Yesu anasema kuwa, mara tu matukio ya nyakati za mwisho yatakapoanza, yatatokea kwa haraka. Muda wa neema umeendelea kwa muda mrefu sana. Lakini wakati wa hukumu hatimaye unakuja, mambo yote yatatamatishwa. Dhana hii ya Mungu kupelekea mambo yote kuwa na kikomo inarejelewa katika vifungu vingi vya Maandiko (Mathayo 24:22, Marko 13:20, Ufunuo 3:11; 22: 7, 12, 20).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Yesu alimaanisha nini aliposema, 'Kizazi hiki hakitapita?'
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries