settings icon
share icon
Swali

Je, tunapaswa kumwabudu Roho Mtakatifu?

Jibu


Tunajua kwamba ni Mungu pekee anayepaswa kuabudiwa. Mungu pekee anadai kuabudiwa, na Mungu peke yake anastahili kuabudiwa. Swali la kwamba tunapaswa kumwabudu Roho Mtakatifu linajibiwa tu kwa kutambua kama Roho ni Mungu. Kinyume na mawazo ya ibada fulani, Roho Mtakatifu si tu "nguvu," lakini nafsi. Anatajwa kwa maneno binafsi (Yohana 15:26; 16: 7-8, 13-14). Anatenda kama Kiumbe chenye nafsi kitaezafanya-Anasema (1 Timotheo 4: 1), Anapenda (Warumi 15:30), Anafundisha (Yohana 14:26), Anaombea (Warumu 8:26), na kadhalika .

Roho Mtakatifu anamiliki asili ya uungu — Anashiriki sifa za Mungu. Yeye si malaika wala mwanadamu kwa asili. Yeye ni wa milele (Waebrania 9:14). Yeye yuko kila mahali (Zaburi 139: 7-10). Roho anajua yote, yaani, anajua "vitu vyote, hata mambo ya kina ya Mungu" (1 Wakorintho 2: 10-11). Aliwafundisha mitume "vitu vyote" (Yohana 14:26). Alihusika katika mchakato wa uumbaji (Mwanzo 1: 2). Roho Mtakatifu anasemwa katika ushirika wa karibu na Baba na Mwana (Mathayo 28:19; Yohana 14:16). Kama Mtu, anaweza kudanganywa (Matendo 5: 3-4) na kuombolezwa (Waefeso 4:30). Zaidi ya hayo, vifungu vingine katika Agano la Kale vinavyohusishwa na Mungu vinatumika kwa Roho katika Agano Jipya (angalia Isaya 6: 8 na Matendo 28:25, na Kutoka 16: 7 na Waebrania 3: 7-9).

Mtu wa Mungu anastahili kuabudiwa. Mungu "anastahili sifa" (Zaburi 18: 3). Mungu ni mkuu "anastahili sifa zaidi" (Zaburi 48: 1). Tumeamriwa kumwabudu Mungu (Mathayo 4:10, Ufunuo 19:10; 22: 9). Ikiwa basi, Roho ni mungu, Mtu wa tatu katika utatu wa Mungu, Yeye anastahili kuabudiwa. Wafilipi 3: 3 inatuambia kwamba waumini wa kweli, wale ambao mioyo yao imetahiriwa, wanamwabudu Mungu kwa Roho na utukufu na kufurahi katika Kristo. Hapa kuna picha nzuri ya ibada ya wanachama wote watatu wa Uungu.

Tutamwabudu Roho Mtakatifu aje? Njia ile ile tunayoabudu Baba na Mwana. Ibada ya Kikristo ni ya kiroho, inayotokana na kazi ya ndani ya Roho Mtakatifu ambayo tunasikia kwa kutoa maisha yetu kwake (Warumi 12: 1). Tunamwabudu Roho kwa kutii amri zake. Kurejelea Kristo, Mtume Yohana anaelezea kwamba "Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa "(1 Yohana 3:24). Tunaona hapa uhusiano kati ya kumtii Kristo na Roho Mtakatifu anayeishi ndani yetu, kutuhukumu kwa vitu vyote-hasa mahitaji yetu ya kuabudu kwa utii-na kutuwezesha kuabudu.

Kuabudu kwenyewe ni shughuli ya Roho. Yesu anasema kwamba "tuabudu kwa roho na kwa kweli" (Yohana 4:24). Wale ambao ni wa kiroho ni wale ambao Roho anaishi ndani yao ambaye hutuhakikishia kwamba sisi ni wa Yeye (Warumi 8:16). Kuwepo kwake katika mioyo yetu kunatuwezesha kurudisha ibada kwake kwa Roho. Sisi tuko ndani yake vile yeye yuko ndani yetu, kama vile Kristo yuko ndani ya Baba na Baba yuko ndani yetu kupitia Roho (Yohana 14:20, 17:21).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, tunapaswa kumwabudu Roho Mtakatifu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries