settings icon
share icon
Swali

Mimi ni mzazi; ninawezaje kuwaachilia watoto wangu wazima?

Jibu


Kuwaachalia watoto wazima ni mapambano kwa wazazi wote, wote Wakristo na wasio Wakristo. Tunapozingatia kwamba karibu miaka ishirini ya maisha yetu imewekezwa katika kulea, kukuza, na kumtunza mtoto, ni rahisi kuona kwa nini kuachilia jukumu hilo ni kazi ya kutisha. Kwa wazazi wengi, kulea mtoto hutumia muda, nguvu, upendo, na wasiwasi wetu kwa miongo miwili. Tunawekeza mioyo, mawazo na roho zetu katika ustawi wao wa kimwili, kihisia, kijamii na kiroho, na inaweza kuwa ngumu sana wakati sehemu hiyo ya maisha yetu inafikia tamati. Wazazi ambao wanajikuta katika "kiota tupu" mara nyingi wanajitahidi kupata usawa sahihi wa upendo na wasiwasi kwa watoto wao wazima huku wakipinga msukumo wa kuendelea kudhibiti.

Kibiblia, tunajua kwamba Mungu huchukua jukumu la mzazi kwa umakini sana. Maonyo ya uzazi mzuri yamesheheni katika Maandiko. Wazazi wanapaswa kulea watoto katika "adabu na maonyo ya Bwana," sio kuwafadhaisha au kuwaghadhibisha (Waefeso 6:4). Tunapaswa "kumlee mtoto katika njia impasayo" (Mithali 22:6), kumpa zawadi nzuri (Mathayo 7:11), kumpenda na kumuadhibu kwa ajili yake (Mithali 13:24), na kukimu mahitaji yake (1 Timotheo 5:8). Kwa kinaya, mara nyingi ni wazazi wanaochukua majukumu yao ya uzazi kwa uzito sana na ambao wanayafanyia kazi kubwa ndio wanajitahidi zaidi kuachilia. Mama wengi kuliko baba wanaonekana kuwa na ugumu, labda kwa sababu ya hamu kubwa ya mama kukuza na kuwahudumia watoto na kiasi cha muda ambao hutumia nao wakati wanavyokua.

Katika moyo wa ugumu wa kuwaachilia watoto wetu ni kiasi fulani cha hofu. Dunia ni eneo la kutisha, na hadithi nyingi za mambo ya kutisha yanayotokea huongeza hofu zetu. Wakati watoto wetu ni wachanga, tunaweza kufuatilia kila wakati wao, kudhibiti mazingira yao, na kulinda usalama wao. Lakini wanapokua na kukomaa, wanaanza kuingia ulimwenguni peke yao. Hatuna tena udhibiti wa kila hatua yao, yule wanaona, wapi wanaenda, na kile wanachokifanya. Kwa mzazi Mkristo, hapa ndio ambapo imani inaingia kwenye picha. Labda hakuna chochote hapa duniani cha kujaribu imani yetu zaidi kuliko wakati ambapo watoto wetu wanaanza kuvunja vifungo ambavyo vilikuwa vimewashikilia karibu nasi. Kuwaachilia watoto haimaanishi tu kuwaachilia katika ulimwengu kujilisha wenyewe. Ina maana ya kuwaachilia kwa Baba yetu wa mbinguni ambaye anawapenda zaidi kuliko sisi tulivyoweza, na ambaye anawaongoza na kuwalinda kulingana na mapenzi Yake kamilifu. Ukweli ni kwamba wao ni watoto Wake; ni wa Yeye, sio wetu. Amewakopesha kwetu kwa muda kidogo na kutupa maelekezo juu ya jinsi ya kuwajali. Lakini hatimaye, tunapaswa kuwarejesha Kwake na kuamini kwamba Yeye atawapenda na kulea roho zao kwa njia ile ile tuliyowalea kimwili. Tukiwa na imani zaidi ndani yake, tutakuwa na uoga kidogo na tutakuwa tayari zaidi kuwaachilia watoto wetu Kwake.

Kama ilivyo na vitu vingi katika maisha ya Kikristo, uwezo wa kufanya hivyo inategemea jinsi tunavyojua Mungu wetu na muda gani tunayotumia katika Neno Lake. Hatuwezi kumwamini mtu ambaye hamtujui, na hatuwezi kumjua Mungu isipokuwa kupitia Maandiko. Wakati Mungu anaahidi kutotujaribu zaidi ya uwezo wetu wa kuibeba (1 Wakorintho 10:13), tunawezaje kuamini hilo isipokuwa kujua katika mioyo yetu kwamba Yeye ni mwaminifu? Kumbukumbu la Torati 7:9 linasema, "Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kusha amri zake, hata vizazi elfu." Kumbukumbu la Torati 32:4 inafikiana:" Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; maana njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili." Ikiwa sisi ni Wake, atakuwa mwaminifu kwetu na kwa watoto wetu, na zaidi tunavyomjua na kumwamini, zaidi tunaweza kuweka watoto wetu katika mikono Yake yenye uwezo. Ukosefu wa imani ndani yake na madhumuni Yake kwa watoto wetu itasababisha kutokuwa na uwezo au kutokuwa na hamu ya kuwaachilia watoto wetu.

Kwa hivyo nini jukumu la wazazi kama watoto wanakuwa watu wazima? Hakika hatuwezi 'kuwaachilia' wao kwa maana ya kuwatelekeza. Sisi bado ni wazazi wao na daima tutakuwa. Lakini wakati sisi hatuwezi kuwalea tena na kuwalinda kimwili, bado tunajihusisha na ustawi wao. Ikiwa sisi tuko katika Kristo na watoto wetu pia, wao pia ni ndugu na dada zetu katika Kristo. Tunajihusisha nao kama tunavyofanya marafiki zetu wengine katika Bwana. Muhimu zaidi, tunawaombea. Tunawahimiza katika safari yao na Mungu, kutoa shauri wakati unahitajika. Tunatoa msaada ikiwa unahitajika na kukubali uamuzi wao wa kupokea au kukataa. Mwishowe, tunaheshimu faragha yao kama vile tunavyoweza kuwa na mtu mwingine mzima. Wakati wazazi hatimaye wanaachalia watoto wazima, mara nyingi hupata uhusiano wenye nguvu, kina, na unaotimiza zaidi kuliko walivyoweza kufikiria.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mimi ni mzazi; ninawezaje kuwaachilia watoto wangu wazima?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries