Swali
Kuchachawa katika ibada-je! Biblia inasema nini?
Jibu
Dansi imetajwa katika matuko mengi katika Maandiko. Mara ya kwanza watu wa Mungu wanaonekana wakichachawa kama tendo la ibada linapatikana katika Kutoka 15:20: "Kisha Miriamu yule nabii mke, ndugu yake Aroni, akachukua matari mkononi mwake na wanawake wote wakamfuata na matari yao wakicheza." dansi hii ya furaha kwa Bwana, iliyoongozwa na Miriamu, ilifuata kuvuka Bahari Nyekundu kwa Israeli na kusherehekea uhuru mpya wa Israeli kutoka kwa utumwa.
Walakini, sio kila wakati dansi kwa njia nzuri katika Biblia. Mara tu baada ya chacho ya sifa ya Miriamu, Waisraeli walipatikana wakicheza mbele ya ile sanamu ya dhahabu katika ibada. "Mose alipoikaribia kambi na kuona yule ndama na ile michezo, hasira yake ikawaka, akatupa vile vibao vilivyokuwa mikononi mwake, akavipasua vipande vipande pale chini ya mlima" (Kutoka 32:19). Katika hafla hii kuchachawa ilikuwa sehemu ya sherehe ovu ya ibada ya sanamu. Kwa hivyo, kudansi ni njia ya kuonyesha hisia ambazo zinaweza kutumika kwa uzuri au kwa ubaya.
Matukio mengine ya kuchachawa katika Biblia ni pamoja na 2 Samweli 6:16, ambayo Daudi "akirukaruka na kucheza mbele za Bwana." Pia, Waamaleki walicheza katika sherehe baada ya kuipora Yuda na Filistia (1 Samweli 30:16); kulikuwa dansi iliyodumu kwa muda mfupi, hata hivyo, pindi Daudi na watu wake walipowashinda (aya ya 17-20).
Zaburi inatoa taswira ya kipekee kwa densi kama tendo la ibada. Katika Zaburi 30:11, mtunga-zaburi anasema, "Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza." Zaburi 149: 3 inahimiza matumizi ya dansi katika kumwabudu Mungu: "Na walisifu jina lake kwa kucheza!" Vivyo hivyo, Zaburi 150: 4 inahimiza, "Msifuni kwa matari na kucheza!" kama vile Miriamu alifanya.
Wengine wamehoji kuwa densi ni njia ya kujieleza ya Agano la Kale. Kwa kuwa densi haikutajwa kama njia ya kuabudu katika Agano Jipya, Wakristo hawapaswi kuabudu kwa njia hii. Walakini, hii ni hoja kutoka kwa mtazamo wa ukimya msingi wake si mafundisho ya wazi ya kibiblia. Wakristo wengi wa kwanza katika Biblia walikuwa Wayahudi na labda wangejumuisha aina za ibada za Kiyahudi katika sifa zao kwa Masihi aliyefufuka.
Jambo linguine la kusingatia ni kuwa densi imekuwa ikihuzishwa na matendo maovu. Wazo ni kwamba, ikiwa uchachawa unatumiwa katika ibada, inaweza kuonekana kuwa densi imeidhinishwa katika hali zingine ambazo hazimheshimu Mungu. Walakini, hii hasa sio hali. Uchezaji wa Waamaleki katika 1 Samweli haukumzuia Daudi kucheza katika 2 Samweli. Wakristo wanaweza na wanapaswa kutumia densi kama wanavyofanya katika aina nyingine yoyote ya sanaa kama vile muziki, uchoraji, uigizaji, au utengenezaji wa filamu. Maadamu densi ni ya kuabudu, iliyo na malengo ya Mungu, na inayostahili kusifiwa, inaweza kuwa na nafasi inayofaa katika ibada. Densi ya kuabudu hii tofauti ombi la bintiye Herodia (Marko 6: 17-28).
Hatimaye, ni muhimu kuelewa kuwa densi katika muktadha wa ibada sio elezo la binafsi. Lazima ifanyike katika namna ambayo ni ya manufaa kwa kanisa zima. Paulo aliandika kuwa katika kanisa "kila kitu kitendeke kwa heshima na kwa utaratibu" (1 Wakorintho 14:40). "Kila kitu" itajumuisha utumiaji wa densi katika ibada. Chochote kinafanyika katika kipindi cha ibada na kinawafanye wasimliwaze Yesu lazima kiachwe nje. Kila kanisa lina jukumu la kupanga ibada yake katika namna ambayo inamweshimu Mung una kuwahimiza wote waliomo.
Uchachawa unatumika kama tendo la kuabudu katika Maandiko na unaweza kuendelea kutumika katika njia hiyo hii leo. Walakini, makanisa yanafaa kuwa waangalifu ili waepuke aina ya densi ambayo inawaongoza baadhi kwa majaribu au dhambi, na lengo lapaswa kuwa lile la kumwabudu Mungu badala ya kutaka kuwa wa mfutio. Ikijaribiwa siku hizi densi ni Sanaa nzuri sana ambayo inaweza wasiliza ukweli, kumletea Mungu utukufu na kuwahimiza wengine.
English
Kuchachawa katika ibada-je! Biblia inasema nini?