Swali
Je! Twachangia lolote katika wokovu wetu?
Jibu
Kunazo njia mbili za kuangalia swali hili-kutoka kwa mtizamo wa vitendo na kutoka kwa mtazamo wa kibiblia. Kwanza, kutoka kwa mtazamo wa vitendo, hebu tuchukulie kuwa mtu anaweza changia kitu kwa wokovu wake. Ikiwa hiyo ingewezekana, nani angepata pongezi mbinguni? Ikiwa binadamu kwa njia moja wanaweza changia chochote kwa wokovu wao, basi itakuwa kwamba wanadamu wanapata pongezi wenyewe. Na ikiwa wanadamu ndio wanapata pongezi hii basi itapotosha kutoka hali kuwa Mungu anapata pongezi. Kungekuwa na uwezekano wetu kuchangia kitu chochote ndio tufike mbinguni, basi kila pindi tutakapofika atakuwa akijipongeza kwa sababu ya kile walifanya ili kuupata urahia wa mbingu. Watu hawa hawa watakuwa wakiimba, "Sifa kwangu, nilichangakia kwa wokovu wangu mwenyewe." Ni jambo lisilofikirika kuwa mbinguni watu wanajiabudu badala ya kumwabudu Mungu. Mungu alisema, "Sitampa mwingine utukufu wangu" (Isaya 42:8; 42:11).
Kwa mtazamo wa kibiblia, mwanadamu hachangii chochote kwa wokovu wake. Shida ya mwanadamu ni dhambi yake. Wanatheolojia kwa kawaida hurejelea hili kama "uharibifu kabisa." Uharibifu kabisa ni imani kwamba mwanadamu ni mwenye dhambi kote na hakuna kitu atafanya yeye mwenyewe ili kupata kibali cha Mungu. Kwa sababu ya hali hii ya dhambi, mwanadamu hataki chochote kinachoambatana na Mungu (angalia hasa Warumi 1:18-32). Ni salama kusema kwamba kwa sababu mwanadamu ni mwaribifu kabisa, mwanadamu aliamua kutenda dhambi, kuipenda dhambi, kuitetea, na kuitukuza dhambi.
Kwa sababu ya shida ya dhambi ya mwanadamu, mwanadamu anahitaji Mungu mwenyewe kuingilia kati. Uingiliaji huu umetolewa na Yesu Kristo, mpatanishi kati ya mwanadamu mwenye dhambi na Mungu mwenye haki (1 Timotheo 2:5). Kama vile ilivyokwisha elezwa, mwanadamu hati chochote kinachohusiana na Mungu, lakini Mungu anahitaji kila kitu kinachohusiania na mwanadamu. Hii ndio sababu alimtuma Mwanawe Yesu Kristo kufa kwa ajili ya dhambi za mwanadamu-dhabihu mbadala kamilifu ya Mungu (1 Timotheo 2:6). Kwa sababu Yesu alikufa, kwa imani mwanadamu anaweza tangazwa kuwa halali, kutangazwa kuwa mwenye haki (Warumi 5:1). Kwa Imani mtu amekombolewa, kununuliwa kutoka kwa utumwa wa dhambi, na kuwekwa huru kutoka kwayo (1 Petro 1:18-19).
Vintendo hivi vilivyotajwa-mbadala, uhalalishaji, ukombozi- ni chache tu ambazo zilipeanwa na Mungu mwenye, na havina chochote kinachohusiana na binadamu. Biblia ii wazi kwamba mwanadamu hawezi kuchangia chochote kwa wokovu wake. Wakati wowote mtu anafikiria anaweza changia, kwa hakika anajaribu kufanyia wokovu kazi, ambayo ni kinyume na kauli mbiu ya Biblia (angalia Waefeso 2:8-9). Hata imani yenyewe ni karama kutoka kwa Mungu. Wokovu ni karama ya bure kutoka kwa Mungu (Warumi 6:23), na jinsi ni karama, hakuna kitu unaweza kufanya ili uipokee karama hiyo. Kile unachohitajika kufanya ni kuchukua karama hiyo. "Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake" (Yohana 1:12).
English
Je! Twachangia lolote katika wokovu wetu?