settings icon
share icon
Swali

Biblia inasemaje kuhusu kusimamia / kudhibiti hisia?

Jibu


Wanadamu wangekuwa wapi kama hatungekuwa na hisia, ikiwa tulikuwa na uwezo wa kudhibiti hisia wakati wote? Pengine tungekuwa kama wakala, tuitikia hali zote kwa mantiki na kamwe si hisia. Lakini Mungu alituumba kwa mfano wake, na hisia za Mungu zinafunuliwa katika Maandiko; Kwa hivyo, Mungu alituumba viumbe vya kihisia. Tunahisi upendo, furaha, uheri, hatia, hasira, kukata tamaa, hofu, nk. Wakati mwingine hisia zetu ni nzuri kwa uzoefu na wakati mwingine sio. Wakati mwingine hisia zetu zinatokana na ukweli, na wakati mwingine hisia "hudanganya" kwa kuwa zinategemea ahadi za uongo. Kwa mfano, ikiwa tunaamini uongo kwamba Mungu hawezi kudhibiti hali ya maisha yetu, tunaweza kupata hisia za hofu au kukata tamaa au hasira kulingana na imani hiyo ya uwongo. Bila kujali, kama hisia ni za nguvu na halisi kwa mtu anayehisi. Na hisia zinaweza kuwa viashiria vya manufaa ya kile kinachoendelea ndani ya mioyo yetu.

Hayo kusemwa, ni muhimu kwamba tujifunze kuhusu kudhibiti hisia badala ya kuruhusu hisia zetu kutudhibiti. Kwa mfano, tunapopatwa na hamaki, ni muhimu kuweza kuacha chenye tunafanya na kutambua kwamba tuna hasira, kuchunguza mioyo yetu kuamua ni kwa nini tuna hasira, na kisha kuendelea kwa njia ya Biblia. Hisia sizizodhibitika huwa hazizalishi matokeo ya kumheshimu Mungu: "Kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu" (Yakobo 1:20).

Hisia zetu, kama vile akili na miili zetu, huathiriwa sana na kuanguka kwa wanadamu katika dhambi. Kwa maneno mengine, hisia zetu zimeharibiwa na asili yetu ya dhambi, na ndiyo sababu zinahitaji kudhibitiwa. Biblia inatuambia kwamba tutaongozwa na Roho Mtakatifu (Warumi 6, Waefeso 5: 15-18, 1 Petro 5: 6-11), si kwa hisia zetu. Ikiwa tunatambua hisia zetu na kuzileta kwa Mungu, tunaweza kuwasilisha mioyo yetu kwake na kumruhusu kufanya kazi Yake mioyoni mwetu na kuelekeza matendo yetu. Wakati mwingine, hii inaweza kumaanisha Mungu kutufariji tu, kutuhakikishia, na kutukumbusha kuwa hatuhitaji kuogopa. Wakati mwingine, Yeye anaweza kutusukuma kusamehe au kuomba msamaha. Zaburi ni mfano mzuri wa kudhibiti hisia na kuleta hisia zetu kwa Mungu. Maandiko mengi yamejaa hisia za ghafla, lakini hisia hizo huletwa kwa Mungu kwa jitihada za kutafuta ukweli na haki yake.

Kushiriki hisia zetu na wengine pia kunaweza kusaidia kudhibiti hisia. Maisha ya Kikristo hayakupangiwa kuishi kipeke. Mungu ametupa zawadi ya waumini wengine ambao wanaweza kutubebea mizigo yetu na ambao tunaweza kuwabebea mizigo yao (Warumi 12, Galatia 6: 1-10, 2 Wakorintho 1: 3-5; Waebrania 3:13). Waamini wenzetu wanaweza kutukumbusha ukweli wa Mungu na kutoa mtazamo mpya. Tunapofadhaika au kuogopa, tunaweza kufaidika kutokana na faraja, ushauri, na uhakikisho wa waamini wengine. Mara nyingi, tunapowahimiza wengine, sisi wenyewe tunahimizwa. Vivyo hivyo, tunapofurahi, furaha yetu huongeza wakati tunaposhiriki.

Kuruhusu hisia zetu kutudhibiti sio Uungu. Kukataa au kufuta hisia zetu sio uungu, ama. Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa uwezo wetu wa kujihisi hisia na kuzidhibiti hisia zetu kama zawadi kutoka kwa Mungu. Njia ya kudhibiti hisia zetu ni kukua katika safari yetu na Mungu. Tunabadilishwa kupitia upyaji wa akili zetu (Warumi 12: 1-2) na nguvu za Roho Mtakatifu-Yeye anayefanya ndani yetu kuzidhibiti (Wagalatia 5: 22-23). Tunahitaji pembejeo ya kila siku ya kanuni za maandiko, tamaa ya kukua katika ufahamu wa Mungu, na wakati wa kutafakari juu ya sifa za Mungu. Tunapaswa kutafuta kumjua Mungu zaidi na kuwazilisha yaliyo mioyoni mwetu kwa Mungu kupitia sala. Ushirika wa Kikristo ni sehemu nyingine muhimu ya ukuaji wa kiroho. Tunatembea na waamini wenzetu na kusaidiana kukua katika imani na katika ukomavu wa kihisia.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasemaje kuhusu kusimamia / kudhibiti hisia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries