Swali
Ni jinsi gani Mungu anagagwa vipaji vya kiroho? Je, Mungu atanipa kipaji ninachomwitisha?
Jibu
Warumi 12:3-8 na 1 Wakorintho sura ya 12 huiweka wazi kwamba kila Mkristo amepewa vipaji vya kiroho kulingana na uchaguzi ya Bwana. Karama za kiroho zimetolewa kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo (1 Wakorintho 12:7, 14:12). Muda halisi wa utoaji wa karama hizo haijatajwa. Watu wengi hudhani kwamba vipaji vya kiroho vinatolewa wakati wa kuzaliwa kiroho (wakati wa wokovu). Hata hivyo, kuna baadhi ya mistari pia ambayo inaweza kuonyesha kuwa Mungu anatoa vipaji vya kiroho baadaye. 1 Timotheo 4:14 na 2 Timotheo 1:6 zarejelea karama ambayo Timotheo alikuwa ameipokea wakati aliwekwa wakuku "kwa unabii." Hii inaweza onyesha kwamba mmoja wa wale wazee walio mtia Timotheo wakuvu alizungumzia juu ya karama ya kiroho ambayo Timotheo angekuwa nayo yakumwezesha katika huduma yake ya baadaye.
Pia tunaambiwa katika 1 Wakorintho 12:28-31 na katika 1 Wakorintho 14:12-13 kwamba ni Mungu (si sisi) ambaye anachagua karama za kupeana. Vifungu hivi pia vinaonyesha kwamba si kila mtu kuwa na kipaji fulani. Paulo anawaambia waumini Wakorintho kwamba kama wanaenda kuwa na tamaa au kuwa na hamu ya vipaji vya kiroho, wanapaswa kujitahidi kupokea vile vipaji vya kuwajenga, kama vile unabii (kuongea neno la Mungu kwa ajili ya kuwajenga wengine). Sasa, ni kwa nini Paulo anawaambia kwa nguvu watamanie karama "kuu" kama tayari walikwisha pewa karama zote, na hakukua na nafasi zaidi ya kupata karama zaidi? Inaweza kusababisha mmoja kuamini kwamba hata kama Suleimani alitaka hekima kutoka kwa Mungu ili kuwa kiongozi mzuri juu ya watu wa Mungu, hivyo Mungu utupa karama tunazohitaji ili kuwe na faida kubwa kwa kanisa lake.
Baada ya kusema hayo, bado karama hizi hugagwa kulingana na vile Mungu anaamua, si vile tunataka wenyewe. Kama kila Mkorintho alitaka kwa hamu sana karama fulani, kama vile unabii, Mungu hangeweza kumpa kila mtu karama hiyo kwa sababu waliitamani sana. Kama angefanya hivyo, kisha nani ambaye angetumika katika kazi zote nyingine za mwili wa Kristo?
Kuna jambo moja liko wazi amri ya Mungu ni Mungu kuwezesha. Ikiwa Mungu anatuamrisha kufanya kitu (kama vile shahidi, kupendo wasio pendeza, mkawafanye watu wa mataifa kuwa wanafunzi, nk), Yeye atatuwezesha kufanya hivyo. Baadhi wanaweza kuwa hawana kipaji cha uinjilisti kama wengine, lakini amri ya Mungu kwa Wakristo wote ni kushuhudia na kuwafanya wanafunzi ( Mathayo 28:18-20; Matendo 1:8). Sisi zote tumeitwa kuinjilisha kama tuko na au hatuna karama ya kiroho ya uinjilisti. Mkristo mwenye bidii ambaye inajitahidi kujifunza neno la Mungu na kuendeleza uwezo wake wa kufundisha anaweza kuwa mwalimu bora zaidi kuliko youleambaye ako na karama ya kiroho ya ualimu, lakini anapuuza karama hiyo.
Je! tunavipokea vipaji vya kiroho tunapompokea Kristo, au vinajengwa ndani yetu katika hali yetu ya kutembea na Mungu? Jibu ni hali zote mbili. Kwa kawaida, karama za kiroho hutolewa wakati wa kuokoka, lakini pia zinaihitaji kutunzwa kwa njia ya ukuaji wa kiroho. Je, hamu katika moyo wako inaweza kufuatwa na kufanywa kuwa karama yako ya kiroho? Je, unaweza kutafuta karama fulani ya kiroho? Wakorintho wa Kwanza 12:31 inaonekana kuonyesha kwamba hii ina uwezekano: "kwa bidii kuwa na tamaa ya kupata vipaji bora." Unaweza kutafuta karama za kiroho kutoka kwa Mungu na kuwa na bidii kwa kutafuta na kuendeleza hiyo karama. Wakati huo huo, ikiwa si mapenzi ya Mungu, huwezi kupokea ile karama fulani ya kiroho, haijalishii ni jinsi gani utaitafuta baada. Mungu ni mwenye hekima milele, na anajua ni kupitia kwa karama ip utakuwa wa msaada zaidi kwa ufalme wake.
Haijalishi ni kiasi gani sisi tumejaliwa na vipawa na zawadi moja au nyingine, sisi wote tumeitwa kuendeleza baadhi ya vipaji vilivyotajwa katika orodha ya vipawa vya kiroho: kuwa na ukarimu , ili kuonyesha matendo ya huruma, kuwatumikia watu wengine, kuinjilisha, nk. Tunapotafuta kumtumikia Mungu kwa sababu upendo kwa lengo la kujenga wengine kwa ajili ya utukufu wake, Yeye huleta utukufu kwa jina lake, kufanya kanisa lake likue, na kutuzawadia (1 Wakorintho 3:5-8, 12:31 -14:1). Mungu anatuahidi kwamba kama sisi tunamfanya Yeye furaha yetu, atatupa maitaji ya mioyo yetu (Zaburi 37:4-5). Hii bila ya shaka ni pamoja na kutuandaa tumtumikie katika njia ambayo inatuletea lengo na kuridhika.
English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili
Ni jinsi gani Mungu anagagwa vipaji vya kiroho? Je, Mungu atanipa kipaji ninachomwitisha?