Swali
Ni njia gani nzuri ya kumhubiria mtu aliye katika dhehebu au dini ya uongo?
Jibu
Kitu cha muimu kabisa tunaweza kufanya kwa wale wamejiuzisha na madhehebu au dini za uongo ni kuwaombea. Tunahitaji kuomba kuwa Mungu azibadilishe nyoyo zao na kuyafungua macho yao kwa ukweli (2 Wakorintho 4:4). Tunastahili kuomba kwamba Mungu awathibitishie hitaji lao la wakovu kupitia Yesu Kristo (Yohana 3:16). Bila nguvu zake Mungu na uthibitisho wa Roho Mtakatifu, hatuwezi kufanikiwa katika kuwathibitishia ukweli wowote (Yohana 16:7-11).”
Pia tunastahili kuishi maisha ya Kikristo, ili wale wamenaswa katika madhehebu na dini waweze kuona ubadilisho ambao Mungu ameufanya katika maisha yetu (1Petero 3:1-2). Tunahitajika kuomba hekima jinsi ya kuwahubiria kwa njia ya nguvu (Yakobo 1:5). Baada ya haya yote, lazima tuwe wajasiri katika kushiriki kwetu injiri. Lazima tuutangaze ujumbe wa wokovu kupitia Yesu Kristo (Warumi 10: 9-10). Kila wakati twaitajika kuwa tayari kuitetea imani yetu (1 Petero 3:15), lakini lazima tufanye hivyo kwa ukarimu na kwa heshima. Tunaweza kuitangaza kanuni vile inavyostahili, kuvishinda vita vya maneno, na bado tuzuie tukio la nia ya hasira ya utawala.
Hatimaye, lazima tuachie wokovu wa wale tunaowashuhudia kwa Mungu. Ni nguvu ya Mungu na neema yake ambayo yaokoa watu, sio juhudi zetu. Huku ikiwa vyema na jambo la busara kuwa tayari kuutoa utetezi wetu na kuwa na ufahamu wa kuwepo kwa imani potovu, hamna kitu cho chote kati ya hivi vitakavyo jitokeza wakati wa mazungumzo na wale ambao wamenaswa katika madhehebu na dini potovu. Kizuri tutakacho kifanya ni kuwaombea, kuwashuhudia, na kuishi maisha ya Kikristo mbele yao, tukiamini kwamba Roho Mtakatifu atafanya kazi ya kuwavuta, kuwathibitishia na kuwageuza.
English
Ni njia gani nzuri ya kumhubiria mtu aliye katika dhehebu au dini ya uongo?