Swali
Nitawezaje kuwahubiria marafiki na jamii yangu bila kuwakashirisha au kuwafukuza mbali?
Jibu
Kwa wakati mwingine, kila Mkristo amekuwa na jamii, marafiki, mnaofanya kazi nao, au kujuana na mtu ambaye sio Mkristo. Kushiriki injili na wengine inaweza kuwa ngumu, itakuwa ngumu zaidi wakati inahuzisha mtu ambaye mko na uhusiano wa karibu naye. Bibilia inatuambia kuwa watu wengine watachukizwa na injili (Luka 12:51-53). Ingawa, tumeamuriwa kuihubiri injili na hakuna sababu yoyote ya kutofanya hivyo (Mathayo 28:19-20; Matendo Ya Mitume 1:8; 1 Petero 3:15).
Sasa, tutawezaje kuwahubiria watu wa jamii, marafiki, tunaofanya nao kazi au watu wenye tumejuana? Kitu cha muimu tutaweza kufanya ni kuwaombea. Muombe Mungu abadilishe nyoyo zao na ayafungue macho yao (2 Wakorintho 4:4) kwa ukweli wa injili. Omba kuwa Mungu atawathibitishia upendo wake kwao na hitaji lao la wokovu kupitia kwa Yesu Kristo (Yohana 3:16). Omba hekima vile unaweza kuwahudumia (Yakobo 1:5). Zaidi ya maombi, lazima tuishi maisha ya kumcha Mungu (1 Petero 3:1-2). Mtakatifu Francis wa Assisi alisema wakati mmoja, “huburi injili wakati wote na ikihitajika tumia maneno.”
Mwisho, lazima tuwe karibu na wajaziri katika kushiriki injili. Itangaze habari ya wokovu kupitia Yesu Kristo kwa marafiki zako, na jamii yako (Warumi 10:9-10). Kila wakati kuwa tayari kuinena imani yako (1 Petero 3:15), kwa kufanya hivyo kwa ukarimu na heshima. Hatimaye tumwachie Mungu mambo ya wokofu wa wengine. Ni nguvu za Mungu ambazo zinaokoa, sio nguvu zetu. Chenye tunaweza kufanya na cha muimu ni kuwaombea, na kuwashuhudia, na kuisha maisha ya kikristo mbele zao.
English
Nitawezaje kuwahubiria marafiki na jamii yangu bila kuwakashirisha au kuwafukuza mbali?