Swali
Ilichukua muda mgani Biblia kuandikwa?
Jibu
Vitabu vya Biblia viliandikwa katika nyakati tofauti na waandishi tofauti katika kipindi cha takribani miaka 1,500. Lakini hiyo sio kusema kwamba ilichukua miaka 1,500 kuiandika Biblia, ni kwamba ilichukua muda mrefu kuikamilisha kanoni ya Maandiko vile Mungu alivyozidi kujifunua katika Neno Lake. Kitabu cha kwanza cha Biblia, kulingana na wasomi wa Biblia wengi, ni Mwanzo au Ayubu, vitabu hivi vinakisiwa kuandikwa naye Musa na karibu 1400 KK na karibu miaka 3,400 iliyopita. Kitabu cha mwisho kabisa kuandikwa ni Ufunuo ambacho kiliandikwa 90 Baada ya Kristo (BK).
Vitabu vya Biblia havikuandikwa kwa mfululizo. Kwa mfano, miaka 400 ilipita kati ya kukamilika kwa kitabu cha mwisho cha Agano la Kale, Malaki, na mwanzo wa Agano Jipya na Injili ya Mathayo. "Miaka 400 ya ukimya" ilitokea kwa sababu Roho wa Mungu hakuvuvia Andiko lolote wakati huo. Ijapokuwa injili ya Mathayo imewekwa ya kwanza katika Agano Jipya, inaaminika kwamba kitabu cha kwanza cha Agano Jipya kilichoandikwa kilikuwa nyaraka ya Yakobo, iliyoandikwa takriban BK 44-49. Agano Jipya lote liliandikwa kwa takriban miaka 50, kutoka BK 44 hadi 90 au 95.
Ni vigumu kujua ilimchukua kila mwandishi muda mgani kuandika kitabu chake. Musa aliandika vitabu vitano vya kwanza vya Agano la Kale katika kipindi cha miaka 40 (1445-1405 KK). Je! Hiyo inamaanisha kwamba Musa alikuwa akiandika kwa mfululizo katika kipindi cha miaka 40? Hatujui jibu. Nyaraka za Paulo kwa makanisa ya Agano Jipya, haswa ile fupi kama vile Filemoni, huenda ziliandikwa katika kikao kimoja. Vivyo hivyo inaweza kusemwa juu ya barua ya Pili ya Yohana na Waraka wa tatu wa Yohana, ambazo ni barua fupi sana zilizoandikwa kwa watu maalum.
Tunajua kwamba kila mmoja wa waandishi wa Biblia aliandika kadri na jinsi walivyoongozwa kufanya hivyo. Kila mwandishi aliandika kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu ambaye "aliwavuvia" Maandiko kwao. Petro anaelezea mchakato huu: "Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya mwanadamu, bali watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu" (2 Petro 1:21; taz. 2 Timotheo 3:16).
English
Ilichukua muda mgani Biblia kuandikwa?