settings icon
share icon
Swali

Wapi/jinsi gani unaweza kochora mstari kati ya kumsaidia mtu na kuruhusu mtu kujinufaisha?

Jibu


Luka 6:30, 35-36 inatuambia "mpe kila akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie." "Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu. Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma." Aya hizi na zingine nyingi katika Biblia hutufundisha kwamba Wakristo wanapaswa kuwa na upendo, huruma, na kujitoa wenyewe. Tunapoona mahitaji ya watu wote walio karibu nasi, mioyo yetu inapaswa kuwa na huruma tu kama Baba yetu wa Mbinguni alivyo na hurumia kwa watu wote. "Bwana ni mwema kwa wote, na rehema zake zi juu ya kazi zake zote" (Zaburi 145:9).

Ni sawa kuwa na moyo ambao utaendelea kuwapa wengine, na humpendeza Mungu kuona tabia hii nzuri katika maisha yetu. Hata hivyo, katika eneo hili la kutoa na kusaidia, Biblia pia inafundisha kwamba tunapaswa kuwa na utambuzi wa hekima (Mathayo 10:16). Mungu anatupa viwango fulani ambavyo tunapaswa kuzingatia wakati inapokuja kutoa muda wetu na fedha kwa wengine. Wakati Biblia inatuambia tuwasaidie wengine, kusudi sio kamwe kwetu sisi kufanya hivyo hadi kiwango ambapo inakuwa na madhara. Ni vizuri kufanya kile tunaweza kufanya, lakini 2 Wathesalonike 3:10 pia hutukumbusha, "Ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula." Kuna watu ambao wanataka kuishi maisha yasiyo ya kujali na bila uwajibikaji kabisa. Hivyo lazima kuwe na mipaka; tutamsaidia mtu aliye na hitaji, lakini ikiwa tunaona kwamba imekuwa mkondo wa maisha ya kudumu, ni mbaya kwetu kuendelea kuhimiza hilo. Ni ya kudhuru sana kwa wengine kuchangia katika utepetevu wao, uvivu, na ukosefu wa juhudi. Msemo wa zamani "Mpe mtu samaki na akule kwa siku moja, mfundishe kuvua samaki na akule kwa maisha yake yote" ni kweli. Almradi tunaona kwamba mtu anafanya juhudi kwa kweli, tunapaswa kuwa pale kumsaidia kwa njia yoyote ile Mungu anaongoza.

Mara nyingi, njia bora zaidi ya kuwasaidia wengine ni kuja pamoja nao ili kutoa halmashauri ya kibiblia, kanuni na kutia moyo. Ikiwa wako tayari kusikiliza na kujaribu, wanapaswa kuwa na uwezo, kupitia uwezo wa Roho Mtakatifu ndani yao, ili kugeuza mkondo huu wa kutegemea wengine. Hii inaanza, bila shaka, kwa uwasilishaji wazi wa Injili ya Yesu Kristo, bila uwezeshaji wake, mabadiliko ya maisha ya ukubwa huu haziwezekani.

Pia tunapaswa kuzingatia yale ambayo Biblia inatuambia kuhusu kuwa wasimamizi wazuri. Tunapoweka imani yetu kwa Mungu na kutembea pamoja Naye, Anaahidi kutoa mahitaji yetu (Wafilipi 4:19). Kile ambacho Bwana hutupa, tunapaswa kukitumia kwa busara. Tunapaswa kumrudishia Bwana sehemu ya kile Anatupa sisi; tunapaswa kutoa kwa mahitaji ya familia zetu; na tunapaswa kulipia gharama zetu. Jinsi tunayvotumia muda wetu pia huhusishwa katika usimamizi; usawa wa ibada, kazi na familia ni muhimu. Haya ni mambo makuu ya usimamizi na hayawezi kupuuzwa, hivyo ni lazima yazingatiwe katika uamuzi wa jinsi na nini tunaweza kufanya katika kuwasaidia wengine. Ikiwa, kwa kumsaidia mtu mwingine kifedha, hatuwezi kushughulikia madeni na majukumu yetu, basi hatufanyi sawa katika jitihada zetu za kusaidia.

Kuna njia nyingi ambazo watu wanaweza kujinufaisha. Ni muhimu kwamba tufanye hili suala la sala, kumwomba Bwana kutuonyeshea kile anataka tufanye. Atatupa hekima ya kutambua haja halisi na kutambua kati ya nafasi na mashaka (Yakobo 1:5). Wakati mwingine, watu hushindwa na majaribio ya maisha na kutofaulu ambao wanaohitaji mtu ambaye ako tayari kuwa rafiki wa muda mrefu kwao. Huu unaweza kuwa uhusiano unaojaribu, lakini pia unaweza kuwa moja yenye malipo sana. Makanisa ya mahali pale yanaweza kuwa na msaada mkubwa kwa wale walio na mzigo kwa wale wanaohitaji. Hata hivyo, kujaribu kumsaidia mtu ambaye hayuko tayari tu kuchukua hatua zozote kuelekea suluhisho katika suala hilo inaweza kuwa sababu isiyo na matumaini. Tena, kuomba kwa hekima ya Mungu na kutumia utambuzi Anaotupa ni muhimu katika hali hizi.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Wapi/jinsi gani unaweza kochora mstari kati ya kumsaidia mtu na kuruhusu mtu kujinufaisha?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries