settings icon
share icon
Swali

Tutaweza kuwaona na kuwajua marafiki wetu na washirika wa jamii huko Mbinguni?

Jibu


Watu wengi wanasema kitu cha kwanza wangetaka kufanya wakati watafika mbinguni ni kuwaona marafiki wao, wapendwa wao waliolala mbeleni. Mbinguni kuna muda mwingi wa, kuona, kujua, na kuwa na muda wa kukaa na marafiki wetu na watu wa familia. Ingawa, hilo halitakuwa jambo letu kuu la kufanya. Tutahusika na kumwabudu Mungu na kufurahia maajabu ya mbinguni. Upatanisho wetu na wapendwa wetu unatazamiwa kujazwa na kuhesabu neema na utukufu wa Mungu katika maisha yetu, upendo wake mkuu wa ajabu, matendo yake makuu. Tutafurahi zaidi kwa sababu tutamtukuza na kumwabudu Bwana Mungu tukujumuishwa na Wakristo wengine, hasa wale tuliowapenda duniani.

Bibilia inasema nini kuhusu kama tutaweza kuwatambua watu katika maisha ya baadaye? Mfalme Sauli alimtambua Samueli wakati mchawi wa Endori alimtoa Samueli kutoka ulimwengu wa wafu (1 Samueli 28: 8-17). Wakati mtoto mchanga wa Daudi alifariki, Daudi akasema, “Mini nitakwenda kwake lakini yeye hatanirudia mimi” (2 Samueli 12:23). Daudi akadhani kuwa ataweza kumtambua mwanawe mbinguni, mbali na yeye kukufa akiwa mtoto. Katika Luka 16:19-31, Ibrahimu, Lazaro na yule mtu tajiri wote walitambulika baada ya kifo. Katika ugeuzo wa sura wa Yesu, Musa na Eliya walitambulika (Mathayo 17:3-4). Katika mfano huu, Bibilia haionekani kuonyesha kwamba tutambulika baada ya kifo.

Bibilia yasema kuwa wakati tutafika mbinguni, “tutafanana naye [Yesu]; kwa kuwa tutamwona vile alivyo” (1 Yohana 3:2). Kama vile mwili wetu wa dunia ulikuwa wa yule Adamu wa kwanza, vivyo ndivyo ufufuo wa miili yetu utakuwa kama wa kristo (1 Wakorintho 15:47). “Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tataichukua sura yeke yeye aliye wa mbinguni. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa” (1 Wakorintho 15:49,53). Watu wengi walimtambua Yesu baada ya kufufuka (Yohana 20:16; 20; 21:12; 1 Wakorintho 15:4-7). Kama Yesu alitambuliwa katika mwili wake wa utukufu, na sisi pia tutambuliwa kwa mili yetu ya utukufu. Kuweza kuwaona wapendwa wetu ni jambo la utukufu mbunguni, lakini zaidi ya yote mbunguni yote ni juu ya Mungu na sio juu yetu kujuana. Itakuwa furaha iliyoje tukiunganishwa na wapendwa wetu mbinguni na kumwabudu Mungu pamoja nao milele yote.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tutaweza kuwaona na kuwajua marafiki wetu na washirika wa jamii huko Mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries